kuna jambo ambalo limekuwa linanitatiza sana kuna msichana ninamjuwa yeye ni jirani yangu wa karibu sana huyu dada sasa hivi yupo mbioni kuwa mke wa mtu maandalizi ya harusi ndio yameanza na anaolewa na mtoto wa mjomba wake na dada huyu sio kwamba ni mhindi ama muarabu ni mafrika mweusi tena mtu wa kigoma....
wazazi wake hawa wawili wamewaonya kutofunga ndoa hiyo lakini hawasikii kabisa na sasa wametishia kwamba ndoa isipofungwa watafanya jambo baya, wazazi wao hawa ikabidi tu wawaruhusu kufunga ndoa hiyo ya kindugu....
linalonishangaza mimi ni kwamba hawa ni ndugu jamani kwani ni halali ndugu kuoana si damu moja wengine wanasema eti kwa sababu ni upande wa mama basi haina nguvu sana huo undugu wao, wewe je msomaji unasemaje kuhusu hili jambo ni sahihi?
No comments:
Post a Comment