mwanamke kusutwa sunna babu lakini mwanamke haipendezi ukiwa mmbea kila mara majumbani mwa watu kutafuta umbea, mara leo unawasema watu fulani wanaringa sana wale, mara wanajifanya wanapendana wale, mara kila siku wale kwao wala vinono wanajifanya watu wa juu sana, mara fulani kapendeza huachi kumsema hivi wewe tatizo lako nini?
huyu mama wanandugu kwa umbea mpaka siku moja akawa amealikwa nyumba fulani kwani walishamjuwa kwa umbea kama kawaida yake alivyofika akaanza kumwaga umbea wake looooo mwanamke unaongea kama umemeza kanda? wakaamua kumtolea uvivu haya akakaribishwa chakula akaingia na kupaka chakula tele na mchuzi na nyama kibao huku anaendelea kuongea umbea si akala kile chakula looooooooooooooo....
kumbe mwanzo wa kumsuta wakawa wamemuwekea pilipili kwenye mboga, alidhani lile rosti la nyama akalipakuwa kwa ushambenga mama huyo akaumbuka jamani anabaki kujipuliza na kulalamika akaambiwa kama unavyokuwa hodari kuwasema wenzako kila kukicha leo adhabu yako ndio hiyo....
yule mama akaacha chakula kwa aibu na kuondoka kwake nadhani atakuwa amejifunza umbea haufai..
No comments:
Post a Comment