sisi wanawake kwa kweli tunamatatizo sana, sasa wewe umealika mashoga zako nyumbani kwako kwani haitoshi kukaa nao sebleni kwenu mpaka ukawaonyeshe chumbani kwako na mumeo? unaona sifa kwenda kuonyesha uzuri wa chumba huoni aibu kama mashoga zako wataona nguo za ndani za mumeo ama ujui kama hizo ni nguo sio za kuonekana na kila mtu?
mara umewapeleka huko chumbani mmoja akaingia na irizi na kuitupa chini ya kitanda, mwishoe hampatani kabisa na mumeo ama hataki kabisa kukugusa kimwili hivi lawama utamtupia nani?mwishoe utaanza kumshtumu kwa umalaya mumeo kumbe wala wewe ndio uliye sababisha..
haipendezi jamani kama urafiki uishie sebleni chumbani auwahusu, kwako na mumeo ni siri yako sio kila mtu aone shuka analojifunika mumeo jamani...
wenye tabia hizi nadhani mtakuwa mmeelewa.
No comments:
Post a Comment