Thursday, July 8, 2010

SOCKS ZILIZOCHANIKA........



haileti picha nzuri kabisa kwa kaka ama dada uwe umevaa nguo nzuri lakini socks chini zikawa zimetoboka, na mara nyingi watu huwa hawajali kama socks zao zimetoboka ama la kwa kisingizio cha kwamba hakuna mtu anayeweza kuona chini ya kiatu...
lakini je pale inapotokea dharula labda ya msiba ama umeenda kutembelea sehemu ambayo ni lazima viatu vivuliwe utajisikiaje? aibu ama utaipotezea?
na je ni kiasi gani cha socks mtu hutakiwa kuwa nazo kwasababu ninaamini kwa watu wanaovaa socks ambazo zimetoboka hawa hawana socks nyingi za kubadilisha, ama ni uvivu ama nikutokujali kama nilivyosema mwanzo?
nitaongelea upande wa wanandoa nadhani kwa wanaume wao kuchukuwa muda na kufikiri kwamba sasa muda wa kununua socks umefika ni mchache sana kwa hiyo sisi kama wakina mama tuwe na juhudi za kuwavisha wame zetu sio tu kwenye mashati na suruali pa muhimu pia ni socks na hata nguo za ndani kwani leo mumeo akionekana amevaa socks za kuchanika aibu kubwa itakuwa kwako inakuwaje unamuacha anavaa hivyo ama ndio muda wa kumkagua wewe mama unakuwa huna utakuta mume kavaa vizuri yani kapendeza kila jicho lamwangalia yeye lakini akivua viatu loooohhh aibu....
chako ni chako tu umuhimu ni ukitunze vizuri, ili asipendeze nje tu bali hata pale pasipoonekana awe mda wote ameng'ara..

1 comment:

  1. ushauri wako ni mzuri, nitaufikisha kwa maiwife wangu maana kwa soksi mtoboko sijamboz

    ReplyDelete