Wednesday, July 14, 2010

SIMTAMANI MUME WANGU KABISA.....

"ROSE" mimi ni dada wa makamu na nimeolwa nina miaka mitatu kwenye ndoa sasa, na nilikuwa namapenzi mengi sana kwa mume wangu mwanza lakini kwa sasa nashangaa nini kimeingia sina tena mapenzi naye kabisa.
yani nadhani nipo naye kwa sababu ya watoto tu maana nina watoto naye watatu wawili wakiwa mapacha, yani hata mume wangu akinitaka kimapenzi huumpa ilimradi afike yeye tu lakini mimi sina hamu kabisa na mara nyingi huwa nafunga macho ili asije kunigundua kama sina hisia naye.
naishi naye kwasababu ya watoto wetu, kwa mapenzi sina kabisa kwake, lakini kila mara nikifikiria kuwa na mpenzi wa nje nashindwa nikiogopa magonjwa na hasa baada ya kusoma topic yako ya saratani ya kizazi (ndio imenichanganya kabisa) maana alisha niambia kama ikitokea tukagombana na nikaondoka na watoto basi nisitegemee msaada wowote kutoka kwake.
simtaki kabisa wandugu naombeni mnishauri nifanyaje?
RAILA

5 comments:

  1. pole sana dada kwa yaliyokupata. mimi nakushauri kama unaweza kwenda kwenye haya makanisa ya kiroho ukaombewa, ninachokiona hapa ni kwamba humpendi mumeo bila sababu yoyote.inawezekana una jini mahaba ambalo kazi yake ni kufanya mapenzi kwa njia ya ndoto,huyu jini mahaba mara nyingi huwa kama mtu mrefu sana na huwa kwenye sura ya mtu unayemfahamu na unakuwa kama unaonata ndoto.ukiwa nae lazima umchukie sana mumeo ili yeye aendelee kuwa wewe. YESU ANAPONYA NA ANAOKOA.ukiombewa utampenda tena mumeo ambaye umeweza kupata nae watoto wawili.huyo ni mume wako uliyepewa na mungu, alilounganisha mungu mwanadamu asitangue.

    ReplyDelete
  2. dada pole sana ndoa yako ni muhimu sana katika maisha yako, muombe mungu na ujiulize nini kimetokea, maana umeishi nae muda mrefu mpaka mmepata watoto.Hebu kaa nae muongee, pengine mtoke kabisa hapo nyumbani kwenda hata hotel kwa maongezi, ninaamini mtapata suluhisho kwani kila mmoja atakuwa muwazi kwa mwenzake.Mungu awasaidie muinusuru hiyo ndoa hasa kwa wototo wenu.

    ReplyDelete
  3. dada pole sana huyo ni jini mahaba kazi yake kuvuruga ndoa za watu ili yeye aendelee kunufaika.
    Nakushauri ukaombewe dada.
    YESU ANAPONYA.

    ReplyDelete
  4. Pole dada kwani ulisha wahi kumfumania? MAOMBI NI SIRAHA KATIKA NDOA YAKO MUOMBE SANA MUNGU USIKU NA MCHANA

    ReplyDelete
  5. hapo dada swala ni simple huyo mume ni vile tu umemzoea ila amini nakuambia siku utakayo mwacha ndo utajua kuwa huyo ndiye umpendae.. kwa msingi hapo la kufanya ni kuongeza vionjo.. jaribuni kwenda out.. mueleze kuwa hujisikii raha.. akuandae vizuri.. akusisimue au mjaribu namna mbali mbali za kujiandaa na tendo au hata mumeo abadili namna anayo vaa, manukato anayo tumia.. nakadhalika... hiyo itasaidia.. mimi naona tatizo ;lako ni la kiakili a.k.a kisaikolojia zaidi na wala siyo kama umemchoka mumeo............ mungu akubaliki

    ReplyDelete