Thursday, July 15, 2010

KUMZIDI UMRI MUME WANGU IMEKUWA BALAA NDANI YA NDOA...



naitwa Mary, mimi na mpenzi wangu David tulikuwa pamoja kwa miezi saba kabla ya kuamua kuoana, kiukweli nimemzidi miaka nane mume wangu huyo wazazi na ndugu zake mume wangu hawakunipenda kabisa na wala hawakutaka sisi kuoana wakisema ujana huyo dada kala na nani na uzee amalizie na wewe kwakweli ilikuwa ngumu sana lakini namshukuru Mungu kwa mapenzi tuliyokuwa nayo kati yetu hatukuyajali hayo na tukaoana..
huu ni mwaka wa tatu sasa kwenye ndoa yetu na hatujabahatika kupata watoto, ndoa sasa imekuwa chungu maana ninavyosimangwa na ndugu wa mume wangu pamoja na mama mkwe wangu. yani imefikia mpaka mama mkwe wangu kumlazimisha mume wangu aoe mke mwengine ili amzalie watoto kwa kweli inauma sana maana ndoa haina raha tena kukikucha mama kaja anataka mtoto, jioni mawifi wanaingia, yaani nimechoka kabisa.
imefika kipindi sasa mume wangu kweli anataka mtoto, jamani njia gani nifanye ili nipate mtoto maana tukienda kwenye shughuli za kifamilia naumia sana kuona wake wenzangu wanawatoto lakini mimi sina, japo mume wangu ananipa moyo kwamba ipo siku Mungu atatufungulia baraka za watoto.
kwakweli nimekonda sana mpaka ndugu zangu wananishangaa na kunishauri bora nimruhusu mume wangu aoe mke mwengine ama nikubali tu tuachane nitulie maana nitakuja kufa kwa mawazo.
nishaurini mwenzenu nifanyeje jamani?

1 comment:

  1. pole mpenzi,jamani unakilio kama changu dada,ila usichoke kumuomba mungu ye nu muweza wayote!

    ReplyDelete