Thursday, July 15, 2010

UFUPI WANGU NI KERO KWA WANAWAKE.....



kwa muda mrefu nimetamani sana kuwa na mpenzi na baadae hata kufunga naye pingu za maisha, mimi nikijana mtanashati ninayefanya kazi katika benki moja maarufu sana hapa mjini. nina nyumba, gari na pesa yakuweza kumtunza mke.
tatizo langu kubwa sipati mwanamke kwasababu ya ufupi wangu wakati sijavaa sare za kazi unawedha kuzani mimi ni mwanafunzi, mpaka marafiki zangu mara nyengine hunitania kwamba nafaa kuwa shule na sio kazini eti bado umri wangu hauniruhusu.
kila nikijaribu kutongoza mwanamke hunikatalia nawengine hata kunikejeli, kwa maneno ya ajabu kama "wewe si ukiingia nikikohoa utatoka" na wengine huniambia "hivi nitapita wapi na wewe nitawaambia vipi watu wewe ni mdogo wangu ama mpenzi wangu"
maneno yao kweli yananikosesha amani na raha hivi mwenzenu nifanyaje?

1 comment:

  1. pole sana kaka, kitu cha kwanza muombe mungu akupatie mwenzi wako, ni yeye tu atakupa yule atakaye kupenda kama wewe na jinsi ulivyo. kweli maneno wanayokwambia si mazuri na kama binadamu yeyeote yule yatakukosesha raha, ila kwa upande mwingine shukuru mungu mtu anapokua mkweli ( japo huo wao unavuka mpaka kwani always jaribu kuangalia kutomkwaza binadamu mwenzio kwa makusudi)kwani wangeweza kukubali kua na wewe wakutumie then mwishoni waende zao wakuache na majonzi bure!

    i believe kaka yangu utampata tu wa kwako kua na uvumilivu.mumgu akubariki upate chaguo la moyo wako.

    ReplyDelete