Wednesday, July 14, 2010

NATAMANI NDOA LAKINI......

Rose kwa kweli hii blog yako haiwezi pita siku bila kuiangalia maana inaelimisha na kufurahisha na pia wachangiaji mada humu wanafurahisha sana, sasa mimi ni msichana mrembo na sinaumri mkubwa sana ila nipo tayari kuolewa boyfriend wangu atakapotaka kunioa.
ila kinachonitatiza ni kwamba kila ninayemuuliza kuhusu ndoa ananipa jibu nisilopenda hata kusikia, na mambo ambayo yanatisha sana mpaka nakata tamaa kabisa kuingia kwenye ndoa na ndio maana na leo nimeamua kuandika humu ili wewe na wengine mnisaidie juu ya ndoa hebu niambie dada yangu kweli ndoa ni ngumu kama wanavyosema?
MAMU

JIBU.....

mpenzi ngoja nikwambie kila ndoa ina raha zake na tabu zake, asikuambie mtu kwamba ndoa ni ngumu sana na usiingie ama akwambie ndoa ni rahisi sana ingia hapana, watu wengi wanavyopanga kuoana mara nyingi hufikiria zile sherehe zinazokuja kwamba watu wanakusanyika wakiwaangalia nyie, mara unataka kushona gauni zuri kuliko yote uliyokuwa nayo (sawa haya pia sio mabaya) lakini unapokubali kuolewa je unafikiria maisha mtakayoishi huko mbele? maana maisha ya uchumba ni tofauti na ya ndoa, ndoa mnalala pamoja, ukienda chooni ukitoka utamkuta, ukiingia jikoni ukitoka utamkuta, mtagombana mpaka kupigana utaenda kutembea upunguze hasira ukirudi nyumbani bado utamkuta, na mara nyengine unakuja hata kugundua vitu ambavyo hukuvijuwa kabisa kuhusu mpenzi wako (labda duh hivi kumbe wewe ukila unakula vibaya hivi) kwani hilo hukuliona tokea mwanzo?
kunawakati mwengine kasheshe zinaanza ukipigiwa simu usiku inakuwa balaa na yeye akipigiwa simu usiku linakuwa balaa zaidi mpaka mnataka kupigana, na mara nyengine mnachokana tu kimapenzi lakini sio kwamba hampendani, mara message za wanaume kwenye simu yako ambao ndio wanakutaka labda wewe huwataki ama upo nao na yeye pia hivyovivyo..
na wakati mwengine mnakuwa na furaha sana na mapenzi tele mpaka unahisi hamna watu wengine duniani mkiacha nyinyi, mnaelewana, mnapeana ushauri mzuri mnapanga kuhusu maisha yenu na mambo tele..
NDOA SIO NGUMU NA WALA ASIKUTISHE MTU, NA MANENO YA WATU YASIKUVUNJE MOYO MPENZI NDOA ZAO NI ZAO NA YAKO NI YAKO...

1 comment:

  1. maisha yote ya mwanadamu asikudanganye mtu, utoto una changamoto, ujana una changamoto na ndoa nayo ina changamoto. huwezi kuikimbia stage Mungu aliyokupangia eti kwa sababu ya kuogopa changamoto/matatizo ni lazima ukubali kupambana na hali zote unazokutana nazo na ushindi upo. Mungu aliweka ndoa kwa kusudi jema kabisa na ni lazima upite huko kote kwa sababu kuna umuhimu wake. Wewe jitose kwenye ndoa na utafurahia tu wala usivunjike moyo kwa kuangalia walioshindwa. Siku zote huendi vitani ukiwa na mentality ya kushindwa, unaenda vitani ukiwa na imani ya kushinda. Weka mtazamo mzuri kuhusu ndoa and you will enjoy it

    ReplyDelete