hivi kukoroma ni ugonjwa? maana nimeona madawa mengi ya kutibu mtu anayekoroma na kama niugonjwa husababishwa na nini? na kwanini watu wengi hukoroma na wengine hukoroma kwa taratibu na wengine kwanguvu sana..
kama kunasiku moja niliwahi kwenda kwenye msiba mmoja, sasa tukaamua kulala msibani wanaume hulala kivyao na wanawake hulala kivyao sasa pale tulipokuwa tumelala wanawake kuna mama alikuwa amelala pembeni yangu jamani yule mama alikuwa anakoroma halafu kwanguvu mpaka tulishindwa kulala ikabidi tuondoke tukalale nyumbani na kugeuza asubuhi...
hebu tuliongelee hili swala na je iweje mtu aweze kuacha kukoroma?
pole na kazi, kukoroma mara nyingi unakuta mtu analala chali halafu mdomo wazi huyo lazima atakoroma pia watu wenye presha asilimia kubwa huwa wanakoroma, muhimu unatakiwa umuangalie huyo anayekoroma amelala vipi, kama ni chali muamshe taratibu ili alale ubavu au kifudifudi, mimi sijawahi sikia kama kukoroma kuna dawa zaidi ya maelezo hayo
ReplyDelete