jamani naombeni mawazo yenu, mimi ni msichana na ninampenzi wangu tumekuwa wote kwa miaka miwili sasa na tunapendana sana tena sana, kinachotukwamisha ni kwamba wazazi wangu mimi hawataki tuwe pamoja kwasababu ya maneno ya uongo waliyoyasikia kutoka kwa watu kuhusu huyu mpenzi wangu tena maneno mazito..
wazazi wangu wakaniwekea kikao cha kutaka kumuacha mpenzi wangu japo nilikataa lakini walinilazimisha wakisema wasingekuja kwenye harusi nitakapo muoa huyo kaka na kama kwenye ndoa nikiwa natatizo hata kidogo kati yangu na mume wangu wala nisiwaendee kabisa kwa lolote..
niliendelea kuwaambia wazazi wangu ninavyo mpenda mpenzi wangu na kwamba siwezi kabisa kumuacha ndipo wakaamua kunipeleka nchi nyengine ili nisiendelee kabisa kuonana na mpenzi wangu kwa muda waliotaka niwe huko wakitegemea nitamsahau ndio walinifanya nizidi kumpenda kwani nilikuwa simuoni ikanifanya nizidi kumfikiria sana..
baada ya muda nikarudi nyumbani na nikaendelea kumuona mpenzi wangu japo bado wazazi hawakupenda, wakaniletea mpaka watu wengine waniseme ili nielewe kwa heshima ya wazazi nikakubali kumuacha mpenzi wangu japo nilimpenda sana na baada ya muda nikapata mchumba na kuolewa..
japo niliolewa lakini mapenzi yangu yote yalikuwa kwa mpenzi wangu, ni muda sasa tangu nimeolwa na mazoea yamenifanya nijifunze kumpenda mume wangu, lakini cha ajabu kutwa tunakorofishana na mume wangu ama mama mkwe wangu na mara nyengine mpaka mawifi..
baba mkwe amejitahidi kutupatanisha na mwanae lakini hatuwezi kukaa miezi mitatu bila kugombana mpaka kuama chumba ama nyumba, hii mara nyingi hunifanya kupata uchungu kwanini sikuolewa tu na mtu tuliyependana kwa dhati hata tungeamua kuhama nchi na kukaa sehemu ambayo hamna mtu anayetujuwa..
nimechoka na sijui tena lakufanya kunusuru ndoa yangu maana kutwa hatuachi kugombana...
No comments:
Post a Comment