Thursday, May 13, 2010

KUNYONYESHA MTOTO



ROSEMARY AND KHLOE MIZIZI

hakuna jambo zuri kama kumnyonyesha mtoto wako, haswa kwa mara ya kwanza kuna kama uoga na furaha kwa wakati mmoja, mwanangu khloe nakumbuka nilivyoanza kumnyonyesha mara ya kwanza nililia kwasababu alikuwa anajitahidi kula kwani alikuwa na njaa na akilia muda wote.
kwa wamama na wadada wenye watoto wengine huogopa kunyonyesha kuhofia maziwa yako kulala na kuhisi yakiwa yamelala hautakuwa na mvuto, nataka nikujulishe ni mvuto gani utakuwa nao wewe mzuri zaidi ya mvuto wa watu kujua unamtoto!!!!!
sasa wewe unayekataa kumnyonyesha mwanao hebu fikiria kuna watu ambao wanalia na kunyanyasika kwasababu tu hawajahimili maumivu na kuwa na huyo mtoto wa kumnyonyesha basi tujitahidi katika kuwapa watoto wetu afya kupitia ziwa la mama..
huyo aliyekupa mimba atakuthamini zaidi utakapomkuza mwanae vyema, kwasababu miili yetu baadae itanyauka kwa uzee lakini watoto wetu siku zote watatuletea furaha, upendo na amani nyumbani..

No comments:

Post a Comment