Thursday, May 13, 2010

BARAKA ZA WATOTO




KHLOE MIZIZI


watoto hutupa baraka nyingi sana katika nyumba, nikupitia hao watoto familia zetu husimama imara, watoto hufuta ugomvi unapotokea kati ya wazazi, watoto hukaa nasi kutupatia tabasamu tunapokasirishwa, watoto hutuuguza wakati hakuna mtu mwengine wakutuuguza tukiumwa, watoto hutupa heshma pindi wanapo oana, watoto hutupa furaha zaidi wanapotuletea wajukuu, ni mambo mengi sana naweza kusema kuhusu watoto yasitoshee kwenye blog hii..

natambua maumivu ya watu wasio na watoto, vilio vyao wakinyanyaswa iwe na wakwe ama mawifi, japo huweza kuchukua muda kwakuwa Mungu ndio hutupa watoto basi tusichoke kumuomba watoto..

kwenye vitabu vya Mungu tunaambiwa mke wa Abraham alipata mtoto wake akiwa na miaka 80 basi nasi tusikate tamaa bado tumaini lipo.

kwa muda wake, na wakati wake Mungu atatupatia tusinyanyasane, wala tusichekane pindi watu tunaowafahamu wanapoishi muda mrefu bila watoto..

No comments:

Post a Comment