Thursday, May 13, 2010

TABASAMU TOKA MOYONI

ROSEMARY MIZIZI

watu husema ukitabasamu ama kucheka unaongeza siku zako za kuishi duniani..

tabasamu katika nyumba nikitu muhimu sana sio tu hukufanya upendeze bali huongeza upendo katika familia na watu wanaokuzunguka ndio maana mara nyingi huwa tunajitahidi kufanya ama kuongea mambo ambayo yatafurahisha watu tulio kuwa nao karibu.

tabasamu la mpenzi wako ni tofauti na la rafiki yako, ukiwa na mpenzi wako ni vyema ukafurahi kutoka moyoni, kwani ni ndani ya moyo ndio upendo wenu huanzia, hatakama watu wametukwaza, hatakama mpenzi amekukwaza, kumbuka ukimpuuzia na kutabasamu huwa ile hali ya hasira hutoweka kabisa.

mke hupenda kumuona mume wake akitabasamu na mume pia hivyo hivyo, basi tusinyimane furaha ya tabasamu.


1 comment:

  1. ahsante rose kwa ushauri mamii... nimeipenda hiyo pic yako tho'
    bless u mamii.. leyla

    ReplyDelete