SIKU ZOTE TUKAE KUTAMBUA BABA NI KICHWA CHA FAMILIA LAKINI MAMA NDIO KIONGOZI WA HIYO FAMILIA, MAMA WEWE NDIO CHUMVI KATIKA FAMILIA
NA KAMA TUNAVYOJUA CHUMVI IKIZIDA SANA NI BALAA, NA IKIPUNGUA CHAKULA HAKINOGI, BALI CHUMVI INATAKIWA KUWA YA WASTANI TU KUNOGESHA CHAKULA
MKE LAZIMA UKAWE CHUMVI KWA MUMEO TENA UKAWE CHUMVI KILA IDARA UKAWE CHUMVI KWENYE MAPATO, KWENYE AFYA, KWENYE UPENDO, KWENYE AMANI, KWENYE KULEA WATOTO,KWA NDUGU WA MUME,KWA WAKWE,KWA MARAFIKI WA MUMEO,NA KWA MUMEO MWENYEWE
NACHAMBUA SASA HAPA NDIO TUSIKILIZANE NA KUSOMA KWA MAKINI SANA
CHUMVI KWENYE MAPATO, JAMANI HATA KAMA TUMEOLEWA NDOA ZA KUFANANA LAKINI KILA NDOA INAUTOFAUTI WAKE, ANGALIA NDOA YAKO KIPATO CHAKO KIKOJE, CHA MUMEO KIKOJE, JE WEWE UMEOLEWA NA MWANAUME TAJIRI, MWANAUME ANAYEJIWEZA KWENYE BIASHARA, UMEOLEWA NA MWANAUME WA KIPATO CHA KAWAIDA (SIO KIKUBWA NA WALA SIO KIDOGO) AMA UMEOLEWA NA MWANAUME MWENYE KIPATO KIDOGO WEWE UNAPATA ZAIDI YAKE AMA UMEOLEWA NA MWANAUME AMBAYE WEWE NDIO KILA KITU CHAKE UNAMUHUDUMIA KWA KILA JAMBO
UKISHAJUA WEWE UMEANGUKIA KWENYE KIPATO GANI CHANGANUA KAMA CHUMVI NAINGIAJE HUMO, JE NATUMIAJE HELA ZETU ZA FAMILIA, JE KUNAMABADILIKO YOYOTE MEMA YAMETOKEA TOKEA NIMEOLEWA, JE TUMEONGEZA BIASHARA ZA KUTUINGIZIA KIPATO TOKEA NIMEOLEWA, JE NAHAKIKISHA KAMA MAMA HELA ZA FAMILIA ZINAHUDUMIA VYEMA WATOTO NA WANAOHITAJI MISAADA YETU AMA KWAVILE HELA ZIPO WEWE TENA UNAJIONA NDIO WEWE HUTAKI KUSAIDIA AMBAO WANAHITAJI KISA NI ZAKO NA MUMEO, AMA KWAKUA WEWE NDIO UNAMUHUDUMIA HUYO BABA BASI UKOO MZIMA NA KILA MTU ATAJUA BARABARANI KWAMBA WEWE NDIO WEWE BILA WEWE HAKUNA LINALOKWENDA, AMA KWAVILE UNAPOKEA HELA NYINGI KWA MWEZI KUMZIDI BASI UTABADNIKA MPAKA BANGO, NA AKIKUKOSEA KIDOGO TU UNAMCHAPIA HIYO FIMBO..MMHH
KWENYE AFYA SASA, KAMA MKE NI JUKUMU LAKO WEWE KAMA KIONGOZI WA FAMILIA UTAMBUE NI VITU GANI KWANZIA CHAKULA MPAKA USAFI VINATAKIWA KUWEPO KWAKO AMBAVYO HAVITAWAFANYA KUUMWA MARA KWA MARA, JE MUMEO AU WATOTO WAKO NI WATU WA ALLERGIES, UNACHUKUA HATUA GANI KAMA MKE KUHAKIKISHA WANAKAA NA KULA VITU VYEMA AMBAVYO HAVITAWAFANYA KUUMWA, AU UNAKUA MBINAFSI KWASABABU UNAHAMU YA KULA KITU FULANI HATA KAMA HAWATAKIWI KULA UNAWALISHA, AMA KWASABABU YA UVIVU UNASHINDWA KUFANYA USAFI MWENYEWE KUHAKIKISHA NYUMBA YAKO HAINA VUMBI, AMA KWAKUA TUNAWASICHANA WA KAZI BASI KILA KITU WAFANYE WAO, HATA KAMA WAKIFANYA WEWE KAMA MAMA UNACHUKUA JUKUMU GANI LA KUSIMAMIA NA KUKAGUA KILA KITU KIWE SAFI NA SALAMA AU MPAKA BABA AANZE KUONGEA JAMANI MBONA HAPA HIVI, PALE VILE
CHUMVI KWENYE AMANI, JAMANI TUKUBALIANE KITU HAKUNA WATU WENYE MDOMO NA GUBU DUNIANI KAMA WANAWAKE, YANI SISI WENYEWE NDIO CHANZO CHA KUHARIBU NDOA NA KUIJENGA MUNGU NAYE ALIJUA HILI NDIO MAANA AKAANDIKA MWANAMKE MPUMBAVU ATAIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE, ANAJUA KABISA KWAMBA SISI WANAWAKE KWANZA HATUNA SUBIRA, HATUNA KIFUA, NA MDOMO UKIFUNGUKA HUWA NI BALAA...WANAWAKE WENGI TUNATABIA YA KUONGEA PASIPO TAKIWA KUONGEA, YANI SAWA AMEFANYA KOSA MUMEO BASI WEWE UTALIONGEA JANUARY MPAKA DECEMBER, HATA AKIOMBA MSAMAHA TENA ASIJILOGE HAPO KATI AKAKOSEA TENA UNAANZA KUMJUMLISHIA MAKOSA YAKE YOTE YA KWANZIA JANUARY MPAKA HAPO JUNE ALIPOKESA TENA, JAMANI HAIPENDEZI
TUNATAKIWA KUJIFUNZA KUSAMEHE NA KUISHI KWA AMANI NDIO KUNAVITU NAKUBALI VINAUMA YANI VINAUMA HATARI HAKUNA MSAMAHA AMBAO UNAWEZA KUFUTA ULE UCHUNGU WA HILO KOSA, LAKINI TAFUTA NJIA NYENGINE YA KUONGELEA LAKINI SIO KUKUMBUSHIA YA NYUMA HATA KAMA YEYE ANATABIA HIYO UNAJUA JAMBO MOJA MWANAUME ANAJIFUNZA KUTOKANA NA WEWE, UKIACHA KUFANYA KITU NA YEYE TARATIBU ATAJIFUNZA KUACHA..UKIACHANA NA WALE WANAUME WENYE HULKA
WANAUME WENGI WAO KUKOSA SIO KUKOSA NI KUTELEZA TU ILA WEWE UKIKOSA NDIO KOSA, NA HILI LIMETOKEA TOKEA ENZI ZA MABABU ZETU LAKINI NAAMINI IPO SIKU WANAUME WATABADILIKA TU, NA NI SISI PAMOJA NA KUOMBA NDIO TUNAUWEZO WA KUWAREKEBISHA WANAUME WETU, TUNATAKIWA KUWA WAVUMILIVU HASWA KATIKA HAYA SIO KAZI RAHISI
KUNA HII TABIA NYENGINE YA WANAWAKE JAMANI KWAKUA WEWE NDIO UMEOLEWA TENA BASI HAKUNA ANAYETAKIWA AISHI KWENYE MAISHA YA MUMEO, BIBI INAHUSU INGEKUA SIO HAO NDUGU ZAKE UNGEMKUTA HIVYO HUYO, MTOTO WA KIKE UKIONA NDUGU WA MUME UNABINUA MDOMO KAMA UNAMIMBA CHANGA, ULIMZAA WEWE HUYO UKAMLEA MPAKA HAPO ALIPOKUA..HUNA HAYA
BASI MWANAMKE UTAJISHEBEDUA ILIMRADI TU, WEWE TENA MUME WANGU HIVI, HUYO NDUGU YAKO VILE MIYE SITAKI AJE KWANGU, SIJUI WANANICHUKIA BIBI WANAKUCHUKIA KWA HAYO MASHAUZI YAKO YASIOKUA NA MAANA KAMA TEMBELE CHANGA, UKIKAA NA KUA KWA ADABU HATA KAMA HUYO MUMEO UKAJUA MUDA WA KUONGEA NA MUMEO NA MUDA WA MUMEO KUWA NA NDUGU ZAKE UTAPATA HASARA GANI, MTIE BASI KWENYE POCHI UWE UNATEMBEA NAYE KILA MAHALA....ALAAAA
MWANAMKE TOKEA UMEOLEWA KWENYE UKOO STORY NI MOJA YAKO TU, UNAVYOMFANYA MTOTO WA WATU, UNAVYODHARAU NDUGU ZAKE, LOOOHH LAANA NYENGINE HUJA KWA KUTAMKIWA TU MAANA UNAZUNGUKA MIDOMONI MWA WATU KAMA MATE KILA MARA YAPO CHAGUO LAKO KUYATEMA AMA KUYAMEZA, SHOGA HAIPENDEZI MPAKA MUME MWISHO ATAKOSA AMANI KWENYE NDOA MAANA NDUGU ZAKE WATAMNYIMA RAHA MTOTO WA WATU ACHANGANYIKIWE KISA KUSHINDWA KUCHAGUA AMTETEE NANI KATI YA MKEWE AMA NDUGU ZAKE
MARAFIKI WA MUMEO UNAWAJUA?? KUNA WALE WA MBALI NA WALE WA KARIBU UNAHESHIMANA NAO VIPI KAMA MKE, AMA NDIO KWASABABU WANAKUJAGA KWENU LABDA WEEKENDS AU MNAKUTANA MARA KWA MARA UKIWA NA MUMEO BASI MTOTO WA KIKE UNATAKA KULETA MAZOEA KAMA MARAFIKI ZAKO, UTAWAZOEAAAA WEEE MPAKA KUPITILIZA, UTAJICHEKESHA KAMA UNATAFUTA BWANA, WANAUME NI WADHAIFU UNAWEZA MCHEKEA AKAKUKULA VILEVILE, HEBU TUWE NA KIASI JAMANI KWENYE KILA JAMBO
UKAWE MKE TEGEMEO KWA MUMEO YANI AFURAHI KUWA NA WEWE UKAMPE AMANI HATA PALE ANAPOKUA HANA KABISA AJISIKIE ANACHO KWAKUA UNAMPA NGUVU KAMA MKE, UKAMUONGOZE VYEMA NA UKAJIHESHIMU NA MUNGU ATAZIDI KUWABARIKI.
***END***
Tuesday, September 16, 2014
kua tegemeo na amani yake...
1:12 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment