MKE MWENZAKO AU WAKE WENZAKO SIO DADA ZAKO KWAMBA WATAKUPENDA NA KUKUJALI KWA YOTE, NA WALA SIO WIFI ZAKO KWAMBA WATAKUPENDA KWASABABU UNAMTUNZA KAKA YAO..HAPANA
WAKE WENZIO KAMA NI MBIO ZA KUKIMBIA PIA HAWA NI WASHINDANI WENZAKO KATIKA KUSHINDANA NA KUJIONESHA KATI YA WAO AMA YEYE NA WEWE NANI ANAWEZA KUMTUNZA MUMEWE VIZURI KATIKA KUWANIA UKE BORA KWA WAKWE ZENU
KUNA AMBAO WATAKUPENDA KWA UKWELI WAKIKUCHUKULIA KAMA MDOGO WAO AMA MKUBWA WAO NA KUKUONGOZA VYEMA KATIKA MAISHA YA NDOA (ILA HAWA NI WASOMI MARA NYINGI)
NA KUNA WALE AMBAO KAZI YAO NI KUKUCHUNGUZA TU, NA KUKUCHUKIA BILA SABABU, KUTWA WATAKAA KUKUONGELEA MABAYA KWA NDUGU NA WAKWE (HAWA WENGI HUWA HAWAJASOMA SANA NA HAWANA SHUGHULI ZA KUFANYA)
SUMU YAO WAKE WENZA NI KUBWA KULIKO SUMU YA MAWIFI KWAKUA WAO NAO WAMEOLEWA INAAMA WAKIKUSAMBAZIA MANENO MABAYA KWELI UTAONEKANA MBAYA HATA KAMA NI UONGO, MAANA BORA WIFI AKUSINGIZIE UTASEMA WANAGUBU HAYA HAWA AMBAO NA WAO WAMEOLEWA UTAAMBIWA WAKUONEE WIVU KWA NINI??
BILA KUJUA SISI WANAWAKE BWANA HATUPENDANI, YANI WANAWAKE HATUPENDANI HATUPENDANI, UTAKUTA TU MTU KWAVILE ANAMAISHA MAZURI KULIKO WAO BASI MANENO OOHHOO ANARINGA, OOHH OANAJIFANYA ANAHELA, OOHH ANAJIFANYA MSOMI, OOHH ANAJIONA MZURI BASI TU WAKUKEREHESE TENA WAKIKUTANA NA YULE WIFI AISYEKUPENDA SHOGA UTAJUTA..LAKINI WEWE SIKUZOTE JIBU LAKO LA KUWAUMIZA NI KUKAA KIMYA TU
NA PIA KAMA MKE HATA KAMA WAO WATAKUONGELEA VIBAYA HATA KAMA MANENO YAUME VIPI HAKIKISHA MAHUSIANO YAKO WEWE NA WAME ZAO YAPO SAWA SIKU ZOTE, YANI USIGOMBANE NA MASHEMEJI ZAKO HATA KAMA WAMEAMBIWA NINI KUHUSU WEWE USITAFUTE UGOMVI NAO USIJE KUONEKANA KWELI WEWE NI MBAYA ACHA WAO WAJIONGELESHE NA KUJISEMESHA WEWE SAMBAZA UPENDO..WAUE KIZUNGU
WENGINE WATAKUCHUKIA TU KWASABABU LABDA WEWE UMEZAA YEYE HAJAZAA BASI KOSA, WENGINE KWASABABU WEWE UMETOKA FAMILIA YA WAOJIWEZA BASI KOSA, TENA BORA HATA KAMA HUKAI NAO SASA WANAKUUMIZA KICHWA CHA NINI
MIMI NAKAA NA MASHEMEJI NA WAKE WENZANGU TUNAPISHANA MILANGO TU WOTE TUPO KWENYE KIWANJA KIMOJA, BASI HIYO MINENO SASA NA HIVI WAO KAZI HAWAFANYI SINA MUDA WA KUANZA KUFIKIRIA KAMA WANANISEMA HATA KAMA NAJUA LAZIMA WATAKUA WANANISEMA MAANA NISHASIKIA MENGI ILA MUDA SINA
SALAMU NDANI, NAWAPENDA KAMA NDUGU ZANGU LAKINI LAZIMA UJUE MIPAKA YAKO SIO TENA NDIO UJIACHIE KILA KITU KAMA MMEZALIWA TUMBO MOJA, MAANA UTAKAPOJIACHIA TU UKIDHANI UNAWAAMINI SHOGA AKIJIFUNGIA CHUMBANI NA MUMEWE NA STORY HANA UTATETWA..NA MUMEO YATAMFIKIA
MIYE NISEME, NIIMBIE TAARABU, NICHAMBUE, NITUKANE, NINYALI MPAKA SHINGO IKATIKE, NA NIKIKUJAA NITAPIKE USIKU HUYO NAJIFUNGIA CHUMBANI NA MUME WANGU, MATOKEO KWENYE MAISHA MAAANA UKIMTAKIA MWENZIO MABAYA MUNGU NAYE ANAZIDI KUMPANDISHA WEWE NITAKIE YANGU MABAYA KWA MUNGU YEYE ANANIPANGIA MAZURI ZAIDI YAKO..MALIPO HUMUHUMU DUNIANI MBINGUNI KUHESABIWA TUUU
HILI BIBI LAKO KAMA SIO LAKO LA JIRANI YAKO MWENYE TABIA HIZI..MFYUUUUU HUNA HAYA MWANAMKE MZIMA SHOGA WOTE TUMEOLEWA HAKUNA ALIYEAMIA KISA CHA KUPIGANA VIKUMBO NINI, HUYO WAKO ANAKUSHINDA UKIPEWA WANGU UNADHANI UTAMUWEZA..AHAHA HALOOOOOOOOO NIACHE NINENEPE MTOTO WA MWANAMKE MWENZIO NA RAHA NIZIPATE KWENYE KUTA ZA MUME WANGU, LAAZIZI WANGU INI MKALIA NYONGA YANGU..NITAKUPANDISHA NITAKUSHUSHA NA KUKUTUPA KWENYE DUSTBIN
****END*****
Monday, August 4, 2014
Haya tuongelee wake wenzetu wake za mashemeji zetu tunaokutana nao tukiolewa...
4:47 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment