MIMI HUWA NI MSIKILIZAJI SANA WA NENO LA MUNGU IWE KWENYE TV AMA RADIO MAANA NAAMINI NI MUNGU TU NDIYE ANAYEWEZA ONGOZA MAISHA YANGU NA YA FAMILIA YANGU
NA WAPO RADIO NDIO HUWA IPO ON MUDA WOTE NIKIWA NYUMBANI NI 98.1 KAMA UTAPENDA NA WEWE KUSIKILIZA HUWA WANAKUAGA NA MAHUBIRI MAZURI SANA YA KUTUJENGA KATIKA MAISHA NA FAMILIA KWA UJUMLA
KUNA SOMO LIKAWA LINATOLEWA IKAFIKA SEHEMU MUUBIRI AKAONGELEA MAISHA YA MWANZO NA CHANZO KWANINI LEO TUPO HAPA TULIPO NI BAADA YA EVA KUMSHAWISHI ADAM KULA TUNDA WALILOKATAZWA NA MUNGU ALIPOMUULIZA ADAM KWANINI IMEKUWA HIVYO AKAMJIBU SI HUYU MWANAMKE ULIYENIPA
KUNA SOMO LIKAWA LINATOLEWA IKAFIKA SEHEMU MUUBIRI AKAONGELEA MAISHA YA MWANZO NA CHANZO KWANINI LEO TUPO HAPA TULIPO NI BAADA YA EVA KUMSHAWISHI ADAM KULA TUNDA WALILOKATAZWA NA MUNGU ALIPOMUULIZA ADAM KWANINI IMEKUWA HIVYO AKAMJIBU SI HUYU MWANAMKE ULIYENIPA
NIKAKA NA KUTAFAKARI MAISHA YA LEO KATIKA NDOA ZETU AMA MAHUSIANO YETU WEWE AU MIMI TUMEKUA WANAWAKE WA AINA GANI KATIKA KUMJENGA MUMEO
UNAISHIJE KATIKA NDOA YAKO, UNATAMBULIKAJE NJE WANAPOMUONA MUMEO WAKO
WEWE NI MWANAMKE WA AINA GANI, UNAIONGOZAJE NDOA YAKO JE WEWE NI MFANO WA KUIGWA?? JE WANAWAKE WENZIO AMBAO HAWAJAOLEWA WANASEMA WAKIOLEWA WANATAMANI KUWA KAMA WEWE KWA UHODARI WA KUIONGOZA NDOA YAKO NA FAMILIA YAKO???
JE WEWE UMEKUA MKE WA AINA GANI TUNAWEZA KUKUAMINI KUJA KUKULETEA MATATIZO YETU YA NDOA ZETU TUKIJUA MAWAZO YAKO YATATUSAIDIA KUTATUA MATATIZO YETU??
NDOA YAKO TOKEA UMEOLEWA IMESIMAMAJE, IMARA, IMELALA UBAVU, AU IMEDONDOKA KABISA...
MWANAMKE AMEPEWA NGUVU KUBWA SANA KATIKA KUONGOZA NDOA NA KUONGOZA FAMILIA UNATUMIAJE NGUVU ZAKO AMA UNAJICHUKULIA POAPOA TU
AMA KWASABABU UNAJUA BABA NI KICHWA CHA FAMILIA BASI UMEKAA TU KUSUBIRI YEYE NDIO AONGOZE FAMILIA, HATA IKIYUMBA KWAKUA UNAJUA NI KICHWA WEWE UMEKAA TU UNAYUMBA NAE
MUME WAKO ANAKUONGELEAJE WEWE, ANASEMA WEWE NI MKE WA IANA GANI, UMESHAWAHI KUSIKIA ANASHUKURU WEWE KUWA KATIKA MAISHA YAKE, UMESHAWAHI KUSIKIA ANAKUSIFU HUYU MWANAMKE KANILETEA BARAKA KWANGU, UMESHAWAHI KUMSIKIA ANAKUSIFIA NA KUAMBIA KILA MTU JINSI ANAVYOKUPENDA KWA YOTE UNAYOMFANYIA KWENYE NDOA??
NA SIO TU MUMEO, NDUGU WA MUME, NDUGU ZAKO, MARAFIKI ZENU, MAJIRANI WANAKUONGELEAJE WEWE KAMA MKE
KAMA ULIKUA HUJUI KWAMBA NGUVU ZA NDOA KUIJENGA NA KUIBOMOA ZIPO MIKONONI MWAKO UJUE SASA, UWE MWANAMKE MUMEO AKISIMAMA ASEME HUYU MWANAMKE NI BARAKA KUTOKA KWA MUNGU, MKE WANGU NI MALKIA WANGU, MUMEO AKUPE SIFA ZOTE NA NYINGI ZAIDI UNAZOSTAHILI
****END****
Tuesday, July 1, 2014
SI huyu mwanamke uliyenipa....
11:12 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment