Monday, June 2, 2014

sikia hii...

kuna dada mmoja ameolewa ndoa yake sasa inamiaka minne, ameishi mwanzo vizuri tu kama ndoa zote zinavyokuaga

huyu dada anafanya kazi nzuri tu mjini na analipwa vizuri kwa bahati mbaya ama nzuri yeye ndiye mwenye mshahara mkubwa kwenye nyumba lakini japo ya hivyo ni mwanamke tu wa kawaida hapendi makuu, anamuheshimu sana mumewe yani hata ukienda nyumbani kwao huwezi ona tofauti wala kujua kama mama ndio ananguvu ya hela kuliko baba

siku zikaenda mwaka wa pili ya ndoa yao yule baba akapata matatizo ofisini kwao na kufukuzwa kazi kwahiyo akawa hana kazi, amebaki mama tu ndio anayehudumia nyumbani kwa kila kitu

kwa mwaka mzima yule baba alikua anakaa nyumbani tu akiamka afanye usafi wa ndani na hukakikisha nyumba ipo sawa kama kuna nguo atafua yani kazi zote ambazo mama huwa anafanya akiwa nyumbani, huku mkewe akihakikisha ameacha hela ya baba kula mchana na jioni akirudi kazini lazima apike chakula kama mke au siku nyengine anaweza kuta mumewe ameshapika tayari

mapenzi yalikua motomoto na hawakuwa na mtoto, kipindi chote hicho mama alikua anatafuta mimba haikuingia na alipopata moja kwa bahati mbaya alidondoka siku moja mimba ikiwa changa ikatoka kwahiyo miaka mitatu ya ndoa hawakua na mtoto, baba hana kazi wapo wao tu

mwaka wa nne wa ndoa yao baraka zikaingia ndani kwao yule baba akapata kazi na yule mama kwa uwezo wa MUNGU akapata mimba, basi wakaendelea vizuri sana mpaka mimba ya yule dada ilipotimiza miezi mitano na mumewe kutimiza miezi mitano kazini ndio mabalaa ya kaanza

huyu dada mimba ilipokuwa miezi mitano kwakuwa ilikua haionyeshi sana na hachoki wala kuzorota kiafya kazini akapata safari ya kwenda ulaya wiki mbili akaagana vyema na mumewe na kuondoka alipokua safari waliwasiliana vizuri na mumewe kwa email na simu mara kwa mara siku zikaenda

kila mara wakiwasiliana mume alitaka kujua mkewe anarudi lini lakini mkewe kwa mapenzi hakutaka mumewe ajue ili amasuprise kwahiyo akawa anamwambia bado hatujaambiwa kikao kinaisha lini ila soon nitakuja mume wangu..wanamalizia na mabusu simu zinakatwa

kumbe bwana yule baba huku nyumbani kawa kiwembe kwanza harudi nyumbani, mara atongoze wanawake wa mtaani kuna ambao wanamkubalia na ambao wanamkatalia kwa heshima ya mkewe

basi siku ya siku mkutano ukaisha mama akaenda madukani kesho yake akafanya shopping ya vitu vya mumewe na hivi ndio kazi mpya basi kamnunulia mashati na tai kibao mumewe akapendeze kazini, akanunua na vitu vyengine vya nyumbani kwao huyo akapanda ndege na kurudi nyumbani darslam

 basi bwana kwakuwa ni suprise alipofika airport hakumpigia mumewe aje kumchukua na hivi alifika na ndege ya jioni akaamua tu kuchukua tax na kwenda nyumbani alipofika nyumbani kwake nje akakuta geti limefungwa akajua mumewe labda atakuwa hajarudi na kwakua kila mtu anafunguo zake basi akafungua mlango wa nje na baadae kuweza kufungua mlango wa ndani na kuingiza vitu vyake

nyumba ilikua kimya saana akazidi amini mumewe alikua hayupo akaamua kabla hajafanya chochote aende chumbani akaoge kwanza akimaliza ndio aanze kumtafuta mumewe, basi akaelekea chumbani kufika kufungua mlango!!!!! lahaula suprise yote ikageuka shubiri baada ya kutoamini macho yake kumkuta mumewe yupo kitandani anakula uroda na msichana wa jirani!!!!

huyu dada na mimba yake anakwambia nilitaka kuzimia akahisi kudondoka akajikuta amekaa chini kwenye sakafu akiwa bado na mshangao akaanza kulia kwa uchungu kama amefiwa basi yule mwanamke wa jirani ndio kuchukua nguo zake na kukimbia

mume sasa kabaki analia hajui afanyaje, mkewe alichofanya ni kuoga tu na kutoka kwenda jikoni akaanza kupika nadhani alikua na njaa akala akalala chumba cha pili bado akiona alichokiona kama ndoto anashindwa kuamini na hajui afanyaje sasa

anasema kabla ya kulala nilimuomba MUNGU anipe amani ya moyo maana naweza kufanya jambo nikalijutia baadae, anasema alitaka kuwapigia simu wazazi wa mwanaume awaambie ila alikua mzito alitaka amatafute mama yake amlilie akaogopa mama ataumia sana alijikuta analia usiku kucha bila kulala na asubuhi yake ndio akanipigia kunipa hii story nimshauri

 ****END****

0 comments:

Post a Comment