Friday, June 27, 2014

hivi kwanini wanawake walio kwenye ndoa wanaogopa nyumba ndogo...

MWANAMKE YEYOTE ANAPOKUA AMESHAKUA MTU MZIMA UNAANZA KUWAZA KUOLEWA NA KUWA NA FAMILIA YAKO UNAANZA SASA KUPIMA KATI YA WALE WA TANO ULIOWAPANGA YUPI UNATAKA AKUOE

UTAKAPOAMUA SASA LABDA JOHN NDIO HUSBAND MATERIAL SASA BIBI WEWE NINAVYOKUAONA UNAVYOJISHUGHULISHA NA NDIO KAMA HIVI MWANAUME ANAKAA MWENYEWE KWAKE UTAENDA UTAJIPIKISHA, UTAFANYA USAFI, UTAJITUMA WEWE KAMA MKEWE....(KWA AKILI ZAKO UNADHANI HIZO TU NDIO SABABU ZA KUKUFANYA WEWE MKE)

LAKINI KWA UPANDE WA JOHN YEYE PIA ANAWANAWAKE WA TATU LABDA ANAWAPIMA AONE YUPI ANAFAA KUWA MKE NA KWAKUWA WEWE TENA NDIO MCHAPAKAZI ANAONA UNAFAA KWAKUA UNAJUA KUMUHUDUMIA VYEMA KAMA MUME

BASI PROCESS ZINAANZA BINTI UNAOLEWA..HUKU WEWE USHAWAACHA WALE WANNE WAKATI JOHN HAJAWAACHA WALE WAWILI ILA KAKUWEKA WEWE KUWA MKEWE...(NA HAPA NDIO TUNAPOKOSEA SISI WOTE WANAUME KWA WANAWAKE) LAKINI NITAGUSIA UPANDE WA WANAWAKE KWAKUWA NDIO TUMO HUMU

UNAPOMUONA FULANI NDIO ANAFAA KUWA MUMEO KUNA MAMBO MENGI TU UNATAKIWA UJUWE, UNAIJUA FAMILIA YAKE?? WAZAZI WAKE?? NA KAMA NDIO NA UMERIDHIA HUYU NDIO WA KUKUOA UMEMKABIDHI KWA MUNGU???

UMEMUOMBEA KWAMBA MUNGU AKUPE KIBALI HUYU AWE MUMEO, UMEVUNJA LAANA ZOTE ZINAZOAMBATANA NAYE, ZIWE ZA MWILI, ZA AFYA NA ZA KIAKILI?????

LAITI NINGELIJUA HILI TOKEA MWANZO NINGEFANYA ILA SIKUANAMTU WAKUNIAMBIA NA WALA SIKULIWAZA NILIINGIA TU KICHWAKICHWA ILA BAADA YA MUNGU KUNIBARIKI KUONGEA NA WANAWAKE BASI NIJUKUMU LANGU KUKUFUNDISHA NA WEWE AMBAYE HUJAINGIA BADO ILI UINGIE KAMILI....

UMEFANYA HAYO YOTE UMEFUNGA UMESALI UKAOMBA SIKU IKAFIKA NA BADO HUYOHUYO MUMEO AKAKUOA BASI MUNGU AMEKUPA HUYO..(KWANI HAMJASIKIA WALIOOMBA KUHUSU WAKE AU WAME ZAO SIKU KADHAA KABLA YA NDOA WAPENZI WAO WAKAFA, AU WAKAWAFUMANIA???) WAKAACHANA

UKISHAINGIA SASA KWENYE NDOA HAPA NDIPO WENGI TUNAPOJISAHAU, MWAKA WA KWANZA UTAPITA VIZURI BADO MPO WAWILI MAPENZI BADO YAPO, KUELEKEA MWAKA WA PILI NDIO NDOA INAANZA KUKOMAA SASA

MUME TENA WASHKAJI WANAANZA KUMTIA AKILI MPYA TOKEA UOE UMEFUGWA HATA HUTOKI UKAE VIJIWENI BASI NAYE KWA AIBU ANAANZA VYA VUJIWENI WEWE TENA UNAACHEA NYUMBANI MPAKA SAA SABA USIKU

WEWE TENA SHOGA KIDAWA HUKUFUNDWA WALA MUNGU WAKO HUMJUI UNAANZA KUPANIC KUMPIGIA SIMU YA MINENO NA MITUSI KIBAO (UKU WAPI HAO MAHAWARA ZAKO NDIO UNAWAONA WA MAANA KULIKO MKEO)UKIMKUTA MWENYE MITUSI KAMA MIYE UNAIMWAGAAAAAAA NA KUMKATIA MUMEO SIMU

KWA AKILI YAKO UNADHANI MWANAUME ATARUDI???ATAENDELEA KUNYWA HUKO NA WEWE HUKU NYUMBANI MIPRESHA INAZIDI KUKUPANDA KILA SAA UNAPIGA MARA MIMESSAGE..MWANAUME HAJIBU WALA HAPAKEI SIMU KWASBABU ANAJUA YATAKAYOJIRI

MWANAUME KARUDI SASA SAA NANE USIKU MTOTO WA KIKE HUJALALA UNAANZA TENA MINENO UKIMKUTA MWANAUME MWENYE MAPENZI ATAOMBA MSAMAHA NA KUTULIA ALALE SHOGA UKIMKUTA KICHAA HAPA NDIO MZIKI UTAUCHEZA ATAONDOKA ATATAFUTA MMOJA KATI YA WALE MAHAWARA AMBAO HAJAWAACHA NA KUMFWATA USIKU HUO AKAMTOE MAWAZO

SHOGA MUMEO TENA NDIO ANIKUTE HAWARA KAMA MIYE GUMEGUME LILILOSHINDIKANA NA MITUME NDOA SINA KAZI YANGU KULEA WAME ZA WATU..UTAOMBA POO MAANA AKIJA HIYO MIHABA,NITAMTULIZA HASIRA,NITAMPELEKA KUOGA,NITAMPA MAJI YA BARIDI AKATE POMBE NITAMPA KIUNO CHA HAJA NITAMBEMBELEZA ALALE....TUKIAMKA SAA TATU NITAMPIKIA CHAI KAMA HANYWI NITAMUOGESHA BIBI NDIO NIANZE KUMUULIZA YALIYOMSIBU JANA KWAKO

SHOGA MUMEO AKINIPA SABABU ETI KISA WIVU WAKO NITAKUKANDIA WEWE MUME AKUONE HUNA MAANA MWENYE MAANA MIYE TU (HAKUNA HAWARA ANAYEWEZA MSIFIA MKE WA MTU HATA SIKU MOJA) KWANI ALIVYOINGIA KWENYE NDOA HAKUJUA WEWE MLEVI AMA UNAMARAFIKI HEBU AKUWACHE MPENZI WANGU..MABUSU TENA HAPO SHOHA NAYATOA...MUME ATAAGA KUONDOKA ARUDI KWAKE

SHOGA MUME TENA AKISHARUDI KWAKO BADALA UFUNGE MDOMO WAKO NAJUA INAUMA ILA UUMIYE KIMOYO UNAANZA TENA KUROPOKA UMEONA KURUDI USIKU HAITOSHI KUKUULIZA UKAAMUA UENDE KABISA KWA HUYO HAWARA YAKO UKALALE WEWE MWANAUME WA AINA GANI HUTHAMINI KABISA MKEO WALA FAMILIA YAKO UNAJIJALI TU WEWE MARA UNAANZA KUMCHUNIA MUMEO SIKU TATU HUONGEI NAYE NI KUINGIA NA KUTOKA TU KULA NA KULALA

WAKATI WEWE MKE UMEMCHUNIA MUMEO HUKU MUME ANAPATA COMPANY KWA YULE HAWARA KWAKUA WANAWASILIANA MARA KWA MARA MAPENZI JUU YAO YANAZIDI KUKOMAA

UMEANZA SASA KUONA.MUME AKUFWATILII HANA HABARI NA YYE KAWA KAUZU UNAANZA SASA KUMPEKENYUA KWENYE SIMU AKIWA KALALA TAFUTA MISSED CALLS TAFUTA ZILIZOPIGWA NA KUPOKELEWA MSG ZOTE INBOX NA OUTBOX...ILIMRADI TU MARA UKAKUTA MSG MUMEO KASIFIWA ALIVYOMPA  MTU VIZURI JUZI NA JANA UNAANZA KUPATA PRESHA

MARA UMALIANZISHA TENA KWA MWANAUME MNAGOMBANAA WEEE MITUSI MWISHOE KWA HASIRA ANAISHIA KUKUPIGA UNAPIGWA SANA WEWE TENA UNABEBA VILIVYOVYAKO NA KUONDOKA

UNAMUACHA MUME ANAJIVINJARI NA HAWARA TENA UKIMKUTA MUME MSHENZI ATAMLETA MPAKA KWENYE KITANDA CHAKO NA STORY YAKO NA MUMEO IMEISHIA HAPO MPAKA MTAKAPOAMUA KUYAONGEA NA WAKUBWA NA LABDA KURUDIANA

HIYO NI PART 1 YA MCHEZO WA NYUMBA KUBWA NA NDOGO TWENDE UPANDE WA PILI SASA

MUMEO KAANZA KUBADILIKA NA BAADA YA KUCHUNGUZA UKAJUA ANAMWANAMKE NJE..

KWANZA MUELEWE KUNA WANAUME WA AINA MBILI MWABAUME AMBAYE HULKA YAKE NI UMALAYA YANI MWANAUME HUYU HAWEZI KUWA NA MWANAMKE MMOJA YANI HUYU MWANAUME SIO KWAMBA HAMPENDI MKEWE ILA SKETI IKIMPITIA TU MBELE LAZIMA AIVUE ALE.

KUNA MWANAUME MWENGINE ANAKUA NA MWANAMKE KWA TAMAA DEMU KAJICHEKESHA KALIWA

MCHUNGUZE KWANZA MUMEO NI MWANAUME WA AINA IPI KATI YA HIZO JUU...NA UKISHAJUA

KWANZA KABISA HAKUNA MWANAMKE YEYOTE MWENYE UWEZO WA KUMBADILISHA MWANAUME, NI MUNGU PEKE YAKE HIYO NDIO SILAHA YAKO YA KWANZA KUSALI TU NAKUMUOMBEA MUMEO

SILAHA YA PILI NDOA YAKO IWE SAWA UKISHAGUNDUA NI MAWASILIANO KIZUNGU WANASEMA COMMUNICATION NA HAPA NDIO WANAWAKE WENGI TUNAKOSEA HATUZUNGUMZI NA WAME ZETU KWA UELEWA NA UTARATIBU BALI UKIGUNDUA TUNAZUNGUMZA KWA MATUSI AMBAYO YANABOMOA NA SIO KUJENGA

 KWAKUA WAKATI HUO UTAKUA NA HASIRA SANA LAKINI KWAKUA WEWE NI MWANAMKE MUNGU AMEKUPA HEKIMA NA UVUMILIVU WA HALI YA JUU UTALIMEZA KWA TABU UTASALI SANA WAKATI UNASALI KIMOYO UNAWEZA UKALIA SANA ILI UPOZE MAUMIVI,UTAJIKAZA ULALE MPAKA ASUBUHI

 SIKU YA PILI HASIRA HUWA ZIMEPUNGUA NDIO UTAONGEA NA MUMEO NA KUTOA DUKUDUKU LAKO LOTE HATA UKILIA LIA MWANAUME ATAKUSIKILIZA TU

 SASA WENGINE CHA KWANZA NIKUCHUKUA NUMBER YA HAWARA NA KUMUENDEA HEWANI CHAMBAAAAA CHAMBAAA NA WEWE TUKANA TUKANA NA WEWE UKIMKUTA HAWARA NAYE KAJAA ATAKUCHAMBAA WEWE UJUTE NA UZIDI KUUMIA NA KUONGEZEA ATAMWAMBIA MUMEO NA.MUMEO AKIRUDI ATAWEZA KUKUNADILIKIA UNAMDHALILISHA

 NA HAWARA AKUSHAJUA UNATAFUTA VITA NAYE ANAUWEZO WA KUKURUSHA ROHO WEWE KAMA UNAMOYO MWEPESI NDOA UKAIACHA AMA KILA SIKU UKAWA UNAGOMBANA NA MUMEO...YEYE HAJIONEI HASARA KUWAHARIBIA AMANI NA MUMEO AKIKUTANA NAYE HANA UWEZO WA KUMWAMBIA USIMPIGIE MKE WANGU WALA KUTUTAFUTA (NI WANAUME WACHACHE SANA WANAOWEZA KUFANYA HIVI) KWAHIYO AT THE END NI WEWE TU UNAUMIA

WAKE WENGINE WANAWAFWATA MAHAWARA NA KUWATUKANA KUGOMBAMA MPAKA KUPIGANA KISA NINI??? UNAMAUMIVU SANA KULIKO HUYO MUMEO ALIYEAMUA KUKUFANYIA HIVYO KWANINI USIJIPENDE ZAIDI KWANINI UPOTEZE MUDA WAKO KUMFURAHISHA MWANAMKE MWENZIO

 HALAFU WAKATI WEWE UPO BUSY KUMCHAMBA HAWARA NA KUMPIGA NA KUMTUKAMA JIONI MUMEO YUPO BUSY KUMTAFUTA NA KUMPA POLE HUKU AKIKUITA MJINGA SANA YULE.MWANAMKE ANAKURUPUKA TU

KAMA MKE UJITAHIDI KWA MWAKA ANGALAU MARA MBILI MUWE MNAPIMA AFYA ZENU HII INAMSAIDIA PIA MUMEO KUA MAKINI ZAIDI ANAPOAMUA KUCHEPUKA

KAMA MKE JITAHIDI KUONGEA NA MUMEO SABABU ZINAZOMFANYA KUTOKA NJE YA NDOA NA KAMA NI ZA KUBADILIKA MSAIDIANE MBADILISHANE TARATIBU ATABADILIKA HATA KWA IDADI TU KAMA KWA MWAKA ALIKUA ANABADILISHA MARA NNE ATAPUNGUZA KIDOGOKIDOGO

UKIONA UMEFANYA YOTE NA BADO MUME HAELEWEKI AU ANAZIDISHA TABIA ZAKE ZA AJABU NA HAUNA RAHA KWENYE NDOA YAKO WATAARIFU WAZEE KAA PEMBENI USIJE UKAJILAZIMISHA ILI UONEKANE UNA NDOA KUMBE UNAKUFA NDANI

NDOA NI HESHIMA NA SAKRAMENTI WENGI WANAITAMANI LAKINI HAWAIPATI NDOA NI ZAIDI YA KUTOMBANA NDOA NI ZAIDI YA HAWARA NA MAUMIVU YOTE MUMEO AMESHAKUFANYIA NDOA NI AGANO KATI YENU NA MUUMBA NI VYEMA KULIONGOZA VYEMA KATIKA IMANI YAKO NDIPO UTAONA BARAKA ZAKO

NDOA NI HESHIMA NA SAKRAMENTI WENGI WANAITAMANI LAKINI HAWAIPATI NDOA NI ZAIDI YA KUTOMBANA NDOA NI ZAIDI YA HAWARA NA MAUMIVU YOTE MUMEO AMESHAKUFANYIA NDOA NI AGANO KATI YENU NA MUUMBA NI VYEMA KULIONGOZA VYEMA KATIKA IMANI YAKO NDIPO UTAONA BARAKA ZAKO

NA NI VYEMA TUKAJUA KUWAHESHIMU WALIO KWENYE NDOA NA WALIOACHA NDOA ZAO PIA KWANI MPAKA KUAMUA KUACHABA BASI WAMEPITIA MENGI SANA MAZITO NA YENYEKUUMIZA WAKAONA NI HERI KUTENGANA TUACHE KUWAANGALIA KWADHARAU AMA KUWAONA HAWAJUI KUTUNZA MUME WENGINE WALITUNZA NA KUVUMILIA LAKINI NDOA HAIKUWEMO..

HAKUNA MKAMILIFU DUNIANI WEWE UNAMAPUNGUFU YAKO NA MUMEO ANAYOYAKWAKE BASI MJIFUNZE KUBEBEANA MISALABA MKITUNZIANA SIRI ZENU NZITO NA NYEPESI NA KUTIANA MOYO KILA WAKATI BILA KUSAHAU KUFARIJIANA WAKATI WOTE

NENDA UKAWE MKE USIWE MWANAMKE BADILISHA MWENENDO WAKO WA KUIONGOZA NDOA YAKO NA MUNGU WETU WA MBINGUNI ATABADILISHA KILA KILIO CHA NDOA KUWA FURAHA....KATIKA JINA LA YESU...AMEN

0 comments:

Post a Comment