kuna familia moja ya baba, mkewe na watoto wao wawili, mtoto mmoja anafanya kazi hospitalini na huyu mwengine ndio yupo form three
huyu baba yeye katika maisha yake alishasema kwamba kipindi atakapooa atataka na kumuomba MUNGU ampe watoto wawili tu kama wote ni wakike sawa, kama wote ni wa kiume sawa ama hatakama ni mchanganyiko pia sawa
basi bwana kweli MUNGU akawapa watoto wawili huyu wa kwanza wa kiume na wapili wakike
kama tunavyojua maisha ya ndoa kuna kupanda na kushuka, mapenzi kuisha na kurudi vurugu za hapa na pale lakini mwisho inaposhindikana basi wanandoa hutengana ama kuachana kabisa
basi ndoa hii pia ilikuwa na vihoja sana yani mwanamke haishi vituko kwa mumewe, japo mumewe alivumilia sana lakini naamini ndani ya moyo wake alishasema kwamba siku itakuwa basi
akavumilia mpaka huyu mtoto wake alipofika la saba huyu baba na nahisi kwatika wanaume wote ni mara yangu ya kwanza kusikia akaamua kwenda hospital na kuweka njia ya uzazi wa mpango akaamua kufunga kizazi
alifanya hivyo baada ya kuona ameshamaliza kupata watoto aliowahitaji ni kumuomba tu MUNGU awape maisha marefu na afya njema basi akaenda kufunga kizazi bila kumtaarifu mkewe
basi bwana maisha yakaendelea mume akivumilia vituko vya mkewe, uhuni ndio ulikuwa umekomaa sana kwa mkewe na mengine madogomadogo kama anavyosema mumewe
ikafika kipindi mkewe akaingia kwenye mahusiano na kijana mmoja mdogo sana kwa mumewe, yule mama alichanganyikiwa sana na yule kijana kwani aliweza kumridhisha sana kitandani na kumpa mapenzi tele
kijana huyu alikuwa anajiweza anafanya kazi zake nzuri tu na japo yule mama alikuwa na hela zaidi yake mtoto wa watu alijitutumua na kumuhudumia mama japo kwa kidogo alichokuwa nacho
mapenzi kati yao yakawa motomoto mama anachelewa kurudi nyumbani anarudi usiku sana wakati baba na watoto wameshalala, baba hapewi tena haki yake ya ndoa kama zamani na akipewa basi kwa mwezi ni mara mbili tu nyengine zote anapewa kijana
basi bwana huku na kule mama akaanza kujisikia vibaya mara kizunguzungu, mara anahamu ya chakula fulani mara asubuhi anatapika akajua anamalaria kwenda hospital akapima malaria na mkojo akakutwa na kimimba
sasa akaanza kuchanganyikiwa hii mimba ya nani ya mume wangu ama ya hawara..
basi siku hiyo mwenyewe karudi nyumbani kamuandalia mumewe chakula kizuri mapenzi motomoto mpaka mumewe na watoto wakaanza kushangaa walipomaliza kula wakaenda chumbani kwa mahaba mama akaanza kumtomasa baba na kumwambia kwamba anamimba, wanategemea kuzaa mtoto wa tatu
baba ndio kushtuka unamimba??? hapana hiyo mimba sio yangu sasa yale yote mume aliyokuwa ameyaweka moyoni ndio yakamtoka gombana na mkewe mama analia hii mimba yako mume anakataa ndio mume kuamua kumuonyesha mkewe sasa ile alama ya operation aliyoamua kufanya kufunga uzazi
mama tena kumshuka lakini bado akawa mbishi hapana haiwezekani labda ulifanyiwa operation kwa magonjwa mengine kwanini ukaenda kufunga kizazi bila mimi inamaana gani unafanya jambo kama hilo kubwa bila mkeo
yule baba akamwambia kama huamini kesho twende nikupeleke ukashuhudiwe na daktari basi kweli wakaenda mpaka hospital fulani maarufu nchini hapa akachukuliwa file lake daktari ndio kumuhakikishia yule mama kweli mumewe alifanya hivyo
basi ndio mume kumuhoji yule mama hiyo mimba ya nani yani uhuni wote unaoufanya unashindwa kutumia kinga mpaka unaleta mtoto asiye wa ndoa kwenye familia kwakweli sintoweza kukusamehe bora tuachane
yule mama kwa aibu akamuomba sana mumewe msamaha lakini mumewe alimsisitizia hawezi kulea mtoto aliyekuwa sio wake kwahiyo aondoke
basi yule mama akaondoka, akamuacha mumewe na watoto wale wake wawili kwakuwa watoto wote walisema wanataka kubaki na baba yao
*****END*****
Thursday, March 20, 2014
hekaheka za ndoa, MUNGU tu mwenyewe anajua.....
12:24 AM
2 comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
huyo anafanya mzaha watu hata boyfriend hatuwapati alafu yeye anachezea ndoa alafu mmewe akiopata wa nje ataanza tafuta mganga si ndo uchawi wenyewe huo da rose natamani nimpate huyo mwanaume nimkomeshe huyo mwanamke wallahi
ReplyDeleteNdo mm hapa sipo mbali. Talk to me mama.
Delete