Thursday, January 2, 2014

Kuoa na kuolewa ni bahati au ni Baraka... PART 1

Watu wengi wanasema kuolewa ni bahati lakini mimi nakataa mpaka kufa..kuolewa ni baraka ambayo mwanamke amepewa na MUNGU..

Sikumbuki ni kitabu gani ila kuna sehemu kwenye BIBLIA siku nilisoma kwamba kuna watakaoa, watakaoolewa na pia kuna ambao watakufa bila kuoa wala kuolewa

na pia inasema heri tumbo lisilozaa maana siku ya mwisho katika hukumu kutakuwa hakuna baba, wala mtoto wote tutahukumiwa na kupewa tulichopanda sawa kwa sawa

tatizo wanawake wengi hawaolewi kwasababu ya kuchagua sana na kuendekeza umimi

yani wanawake wengi sana wamejiwekea akilini wanataka mwanaume smart, mwenye kazi ya kueleweka, mwenye gari na vitu kama hivyo

na pia wanaume wengi siku hizi nimesikia wanataka mwanamke aliyesoma, mwenye kazi yake na wengine wanataka mwanamke wa familia bora, yani ambao kwao mambo safi na wao wakitafuta mteremko

laki je..huyo mwanaume wa aina hiyo na huyo mwanamke wa aina hiyo kama hayupo, hujawahi kumpata na sio wanaokutongoza ama unaowatongoza inakuwaje...unakaaaaa weee siku zinaenda umri unaenda unasema huna bahati

kuna dada mmoja rafiki yangu sana, baba yake na baba yangu ni marafiki sana kwao wanahela sana, wanamiliki nyumba nyingi sana, magari mengi ya kifahari na kampuni moja ya mambo ya construction inayofanya vizuri sana nchini

huyu dada alikuwa anawanaume wa kila aina mwanzo kabla hajaolewa na wanaume wenye kazi zao na pesa zao nzuri tu

kabla ya kuolewa hata mimi na marafiki zangu tulikuwa na aina ya wanaume ambao tunakuwa nao na kweli wanahela na kwao hela zipo haswa..ndio hivyohivyo rafiki yangu huyu alivyokuwa

 rafiki yangu alikuwa anagari aina ya rav 4 siku moja akiwa njiani anaelekea kazini kutoka kwao kijitonyama akapata ajali akagongwa na daladala, taa yake ya nyuma ikawa imevunjika na gari kubonyea upande wa nyuma kushoto

akaja dereva na kondakta ili waongee na kuyamaliza iliwachukua muda lakini wakafika muafaka, konda akachukua number ya rafiki yangu ili awasiliane juu ya matengenezo ya gari baada ya kuongea na boss wao

baada ya hapo konda akawa anampigia simu kila mara kuhusu gari yani huyu konda ashukuruwe mama yake anaongea kwa upole na adabu akafanya juu chini mpaka gari ya shoga yangu ikatengenezwa

baada ya kutengenezwa pia bado alikuwa siku baada ya siku anampigia rafiki yangu na kumuuliza kama gari inamatatizo yoyote na salamu pia

basi bwana uongeaji upole na kujali kwa konda kukaanza kumshtua rafiki yangu kwa jinsi ambayo aliogopa sana...alihisi sio kawaida

konda hatumi msg yeye akitaka kumjulia dada hali anampigia tu

siku moja konda akamuomba rafiki yangu waonane, akamwambia ni kupiga tu story na kufahaminiana kwakuwa wameshakuwa wakiwasiliana mara kwa mara rafiki yangu alimchukulia konda kama rafiki tu wakawaida akaona sio mbaya kwenda kuonana naye basi wakapanga weekend moja wakakutana

basi bwana siku ikafika shoga yangu akaniambia nikaenda konda aliniambia tukutane brekpoint ya pale kijitonyama, basi kwakuwa ni karibu na nyumbani aliamua kutembea tu na kufika hapo, akamkuta konda amefika maana anasema hata hakumuona kwa jinsi alivyopendeza siku hiyo alihisi kama sio yeye mpaka konda alipomfwata alipokuwa amesimama akikodoa macho na kumtafuta mwanaume wa kawaida sana au labda bado yupo kwenye nguo zake za ukonda

anasema Rose sikuamini shoga yangu nimefika, tumekula tumekunywa sijalipa hata shilingi yote amelipa konda..yani mpaka nikajionea aibu maana nilibeba hela nikijua konda hana uwezo wa kunilisha pale incase akishindwa nilipe mwenyewe..akanizodoa

basi tukawa tunaongea konda akaniuliza mengi kuhusu mimi na wala sikumficha nikamwambia yote kama yalivyo kuhusu maisha yangu, mahusiano yangu, na familia yangu kwa ujumla

hakuonyeshwa kushtuka na labda kama alishtuka ni moyoni mwake, na yeye akanielezea kuhusu maisha yake kwamba ametoka kwenye familia masikini na yeye ni wa kwanza kwao kati ya watoto wa tatu mama yake anauza maandazi na chapati wakati baba yake ni mlinzi wa kampuni binafsi, yeye ndio tegemeo kwao kubwa kulisha familia na kuhakikisha wadogo zake wameenda shule, mdogo wake mmoja yupo form four na mwengine form two

nilimpa pongezi kwa kuweza kuwasomesha wadogo zake mpaka hapo walipofikia na kumpa moyo kwamba MUNGU atamsaidia na ahakikishe anafanya tu kazi zake vizuri basi ataendelea

tukawa tunapiga story nyengine tu baadaye jioni ikafika tukaamua kuondoka alitembea nami akanisindikiza mpaka nyumbani kwetu na kuishia nje ya nyumba..kwa utani akanisifia gorofa yenu nzrui inaweza kutoa nyumba ishirini ya ile tunayoishi sisi, tukacheka tukaagana akaondoka na mimi kuingia ndani

KUTAKA KUJUA KILICHOTOKEA BAADA YA KUONANA....SUBIRI PART 2

0 comments:

Post a Comment