Tuesday, December 10, 2013

Kila mwanamke ana jumamosi na ijumaa yake, hata wakikubania vipi ipo siku wataachia...PART 4

sam akamuomba neema kutomuuliza kitu astazia mpaka watakapokuwa wote kesho yake mchana maana ilikuwa jumamosi akamwambia wataenda slipway kwahiyo aje na astazia hapo wamuulize kwa pamoja

neema akakubali basi wakala wakanywa sam akamrudisha neema nyumbani siku hiyo akamuachia neema laki saba na kumwambia aakikishe kesho anakuja na astazia slipway hatakuja kuwafwata kama kawaida yao na hela nyengine atatumia za matumizi

neema usiku hakuweza kulala yani alikuwa anawashwa tu kumuamsha astazia aliyelala pembeni yake na kuanza kumpaka lakini alikuwa anakumbuka tu maagizo ya sam

 basi kesho yake shoga tena kashaambiwa mtoko kajikoki anajua kwamba wakifika kule neema anatupwa huko kwenye dustbin kwasababu ya umalaya wake mwenyewe moyoni anafurahia huku neema moyoni anamchora tu ndugu yake na alikuwa anahasira naye anatamani kumpiga kwa kumsemea maneno ya uongo

wakafika slipway wakakutana na sam wakaagiza chakula huku wakiwa wanakula sam akamuuliza astazia kuhusu yale aliyomwambia kuhusu neema je ni kweli anawanaume zaidi yangu kama ulivyoniambia maana mimi sitaki mwanamke anayehangaika huku na kule asije niletea magonjwa huyu hapa neema naomba unihakikishie

astazia akaanza kuuma midomo na kumjibu sam ndio huyu neema ni mtu mbaya sana yani ni malaya anawanaume kibao ni ndugu yangu namjua nakaa naye na kulala naye kitanda kimoja yani hafai ndio maana nikakwambia hivyo sam ili umuache asije akakuua kwa magonjwa

neema alichanganyikiwa na kutaka kuzimia akamwambia astazia unasemajie wanaume gani hao unaoongelea mbona sikuelewi lini nimeshakuonyesha mwanaume zaidi ya sam huku machozi yakimtoka akilia kwa uchungu alimuuliza astazia

ndio unawanaume sijui yule peter na john leo unataka kujifanya msafi hapa mbele ya sam ili umchune tu kaka wa watu au kisa mara ya kwanza alikupa milioni moja jana kakupa laki saba ndio unazipapatikia unawaacha wa kina john na peter usijifanye unalia hapa uonekane mwena mwanamke mbaya sana wewe usije kumuua kaka wa watu

sam huyu ni muongo muone tu hapo anajifanya analia lakini ni muongo sana tena naweza kumpigia bwana yake mmoja hapa akaja ukamuona, hapo sasa sam alikuwa ameshachanganyikiwa hajui amuamini nani tena akamwambia astazia muite huyo mwanaume tumuone hapa

basi astazia akampigia yuleee peter njoo hapa slipway chukua tax tutakuja kulipa mara baada ya lisaa limoja peter huyo karibu naomba ujitambulishe ilikuwa sauti ya astazia

peter alivyofika pale na kumuona neema amekaa na sam akajifanya anamfokea sana neema huyu ni nani huna adabu yani unamwanaume zaidi yangu pumbavu kabisa ndio maana siku hizi simu yangu hupokei na hata huji kuniona nikija kwenu kila siku namkuta astazia ananiambia haupo umetoka kumbe huyu ndio bwana yako utanikoma leo malaya wewe

peter akapandisha sasa kutaka kumpiga neema sam akaingilia kati na kumwambia muache mwanamke wangu ole wako umpige leo utaozea segerea

peter akamwambia tena wewe malaya mwenzake nyamaza kabisa unachukuwa tu wanawake wa watu halafu unajifanya unasauti tena usinivuruge wewe ndio utaozea segerea usipoangalia huo mdomo wako

huku neema yeye analia tu haelewi kinachoendelea pale analia kwa nguvu sasa watu wakaanza kujaa pale kuamulia ugomvi neema analia astazia yupo upande wa peter anamtukana neema na sam basi vurugu tupu

 neema akawa analia na sam tu mpenzi wangu hao waongo achana nao huyo peter mimi simjui wala sijawahi kumuona waache tuondoke mpenzi wangu sam akamuangalia neema na kumwambia anyamaze hayo yote atajua baadae kama ni wake ama sio wake

peter akarusha ngumi kumpiga sam sama naye akaanza kupigana na peter pigana sana huku neema analia huku astazia anacheka, baadae sama akatoa bastola kutoka kibindoni mwake na kumuonyeshe peter sasa leo nakuua najiua na mimi tukose wote

neema akawa analia sam usife mpenzi wangu nitakufa mimi ukifa wewe sam wewe ndio kila kitu changu umenipa matumaini ya kupenda tena baada ya kuachwa vibaya ukifa nitaishije mimi bila wewe

sam kusikia maneno yale ya neema uruma na mapenzi yakamuingia akajikuta anashikilia ile bastola kutaka kumlenga peter lakini akaipiga hewani

peter akalia nooooooooooo kwa uoga akidhani amepigwa yeye alivyojiangalia na kujua hakupigwa yeye akapiga magoti na kumuomba sam msamaha sam akashindwa kuelewa kinachoendelea kumbe peter alijua ile bastola labda haina kitu kumbe akagundua akiendelea na huo mchezo anaweza kufa ukweli kwa kosa asilolifanya

akapiga magoti na kuanza kumuhadithia sam na neema kila kitu tokea kwa michael mpaka hapo neema aliposikia hayo akazimia

sam kumbeba neema na kumpeleka hospital kuangaliwa akakuta ana presha pia kwahiyo anahitaki kupumzika neema akalazwa agakhan siku hiyo sam akamchukulia chumba cha private ili awe naye muda wote na hapo ilikuwa ni usiku saa mbili sasa ndio kapelekwa hospital

basi sam akalala na neema hapo hospital neema huku bado analia na kushindwa kuamini kama ndugu yake anaweza kumfanyia hivyo

kamkosanisha ndoa kwasababu ya wivu wake akawa tu analia sam anambembeleza akamwambia sam mimi nilikwambia sijafanya hivyo mpenzi hukuniamini

 sam akamuomba sana msamaha neema basi neema alilazwa pale siku mbili sam akalipia matibabu yake na kumrudisha nyumbani

neema akawa anamwambia sam sitaki hata kurudi nyumbani sijui nitaishi vipi nyumba moja na astazia kwa yote aliyonifanyia alipofika nyumbani ndio akawaeleza wazazi wake kilichomfanya alazwe maana hakutaka kuwaeleza walivyokuwa wanakuja kumuona hospital

walishangaa mama mtu akatokwa na machozi baba mtu aliumia sana basi wakasema labda ilipangwa na MUNGU unaona sasa amekupa sam anakupenda sana na hakutaka kusikiliza mameno ya ndugu yako

akaitwa astazia kweli akakiri huku akilia aliwaomba msamaha na kusema ni wivu ndio uliomponza alilia sana na kuomba masamaha neema kwa roho yake ya huruma alimsamehe ndugu yake na wazazi pia wakamsamehe astazia aliahidi kamwe kutomchukia tena hivyo ndugu yake basi sam akaaga na kuondoka

maisha yakarudi kama yalivyotakiwa kuwa mambo yakaendelea kazini akaenda neema siku hiyo alipokuwa anatoka kazini kama kawaida akategemea sam anakuja kumchukua mara akaja mwanaume tofauri kumchukua kazini na gari aina ya rav 4 nyeupe akamwambia ametumwa na sam kwamba yeye amebanwa kidogo atakuja nyumbani kumuona baadaye

japo alikuwa na wasiwasi kumuamini huyu mtu mara yule kaka akampigia simu sam na neema akaongea naye akapanda kwenye gari na kupelekwa nyumbani wakati anashuka yule kaka akashuka na kufunga gari akamkabidhi funguo neema neema akashangaa kwanini amefanya hivyo yule kaka akamwambia hilo ni gari lako sam amekununulia kutoka kwenye showroom yetu amenituma nikuchukuwe kwakuwa hujui kuendesha

neema alipatwa na butwaa hakuamini alifurahi lakini hakuamini akaingia ndani na kumrusha roho shosti astazia akawa amefurahi na kumpa hongera neema wazazi wake walipokuja jioni kukuta gari ile wakauliza neema akawaambia wakafurahi pamoja naye

usiku wa saa mbili sam alikuja kama kawaida yake kwakuwa sasa walishamjua akawa anaingia ndani akawasalimia wazee akala akaongea na neema baadae akaondoka neema alimshukuru sana kwa zawadi hiyo sam akafurahi naye basi akaondoka

ikapita mwezi sam akamwambia neema kwamba anataka kumuoa wakafanya process japo wengi waliogopa isije ikawa kama mwanzo lakini mwenyewe alisema anamtegemea MUNGU haitakaa kujirudia kama mwanzo

ikafika siku za shughuli neema akafanyiwa kitchen party ya pili akaongezewa vitu tu vichache kwani alikuwa navyo vile vingine akafanyiwa sendoff sam alipendeza sana pamoja na familia yake

na sam akafanya bonge la harusi pale serena hotel

NEEMA akaolewa na SAM


0 comments:

Post a Comment