Friday, November 1, 2013

Leo nataka kuongelea swala hili la kuoana watu wasomi, wenyewe mmemaliza chuo mna ma vyeti vya hatai sijui madegree na mamasters mnavitumiaje kwenye ndoa...

mimi naamini tunasoma na kupata kazi ili tuweze kujikimu kimaisha na kujenga taifa letu, apa nitagusia sana wanawake kwasababu malalamiko mengi niliyoyapata ni kutoka kwa wanaume kuhusu wake zao

ana nilikutana na rafiki yangu mmoja ambaye ameoa na mkewe ni daktari, akaniambia Rose aisee ninahamu sana ya kupendwa...ebooo nikamuangalia kama sijamsikia vizuri ama nilihisi nimesikia vibaya akarudia tena kuniambia nina hamu ya kupendwa

na mimi nikamuuliza mkeo si anakupenda na marafiki zako sisi tunakupenda hata maadui zako pia wanakupenda sasa wewe unataka upendwe upendo gani???

akaniambia Rose yani nataka kupendwa kimahaba, niwe na mwanamke atakayenibembeleza, atakaye nikumbatia na kunipa raha za dunia, mwanamke ambaye atanisikiliza nikitaka kutoa la moyoni...

enhee...nikamwambia sasa hiyo si kazi ya mkeo maana mahaba marafiki na maadui hatuwezi kukupa na huko kukusikiliza ni wachache tutakusikiliza na kukupa ushauri ambao baadae ukusaidie usikusaidie sisi haitatudhuru ila mkeo tu ndio anaweza kukupa yote hayo na matokea yake yeye ndio atayajua na kuyafurahia ama kuyachukia

akaniambia Rose huu ni mwezi wa tano sasa sijui hata joto la mke wangu likoje, usiku nikitaka chakula cha kitanda nikimgusa tu utasikia nimechoka sana leo nilikuwa na wagonjwa wengi sana, siku nyengine ndio anaingia shift za usiku nabaki tu kitandani nalala na wanangu, weekend ikitokea yupo nyumbani hatuna cha kuongea yeye yupo busy na mambo yake ya nyumbani najikuta nimekaa tu nacheza na watoto na kuangalia Tv nikichoka naenda kupiga misele kwa marafiki zangu nakaa huko mpaka usiku ndio narudi yani haya ndio maisha yangu

nikamwambia labda kwakuwa mkeo wiki nzima anakuwa busy kwahiyo weekend hiyo jumapili anayokuwa nyumbani ndio siku ya kuhakikisha kitu nyumbani kinaenda sawa pamoja na watoto sema anachokosea yeye ni kwamba hatengi muda wa kuwa na wewe siunajuwa nyumba bila mwanamke vitu haviendi

akaniambia unamtetea?? mbona huwa namwambia aache hivyo vitu kwani mimi si mumewe aje tu awe na mimi chumbani ananijibu kila kitu kina muda wake na haji kweli

sasa Rose mimi nahisi kuchoka na ninahitaji kupendwa kwahiyo nataka nitafute mwanamke wa nje, sijawahi kufikiria kuingia katika mapenzi mazito nje ila sasa nahisi nahitaji kuwa na mpenzi nje na sio tu kuwa ni hawara bali nitumie naye muda mwingi kama mke wangu maana najihisi kama mwili unachoka yani kama nimeelemewa na mzigo ambao nahitaji kuutua nahitaji mwanamke

nikamwambia kwahiyo kweli umeamua hivyo??? na je huko unapodhani kwamba wewe utapata pumzimko usipopata je?? maana pia kuna wanawake nawao wamevurugwa huko na wapenzi wao je usipopata unachohitaji huko nje huoni utazidi kujichosha??

akaniambia Rose acha kumtetea mke wangu nahitaji mwanamke wa nje, nikamwambia basi naomba hata number ya mkeo niongee naye (mimi mkewe sinaga mazoea naye kwahiyo number yake sikuwa nayo) akaniambia sawa akanipa

akaniambia tena ukiweza mwambie kabisa sasa hivi natafuta mwanamke wa nje yeye naona kazi yake imemshinda..

basi nikamwambia mimi naondoka ila nikiwa njiani narudi nyumbani nitampigia mkeo nimpe vidonge vyake halafu wewe majibu utayapata ukifika nyumbani jioni leo sikaingia asubuhi kwahiyo jioni yupo basi utapata salamu zangu

basi miye tena huyo nikaingia kwenye kiberiti changu naelekea nyumbani sasa kwanza nikamshukuru MUNGU ninagari maana ningekuwa kwenye daladala huu mchambo mbona ningeshushwa kwenye daladala

ngriingriiiiiii simu ikaita akapokea mdada Hallo, nikamwambia habari yako akajimu salama sijui nikusaidiaje nikamwambia samahani wewe ndio ************* akanijibu ndio nikusaidiaje??

nikamwambia mimi naitwa Rosemary Mizizi ni rafiki mkubwa wa mumeo akajibu mume wangu??? nikamwambia ndio si anaitwa ******** mnaishi*******

akaanza kunijibu kwa dharau na hasira kwahiyo nikusaidiaje kama wewe rafiki wa mume wangu, number yake huijui mpaka unipigie mimi???? moyoni nikasema hapohapo ndio nilipopataka mimi uanza hizo dharau zako na miye nimejaaliwa maneno kama nimemeza cassette umefika kwenye idara yangu

nikamwambia weee koma kabisa kuniongelesha kwa dharau nipe heshima yangu kama mke mwenzio usiniongeleshe kama msichana wako wa kazi....akapozi kwanza kama dakika tatu akarudia kuniuliza umesemaje???

nikamwambia unapoongea na mke mwenzio kuwa na heshima maana wote tunachezea mb****** moja na nampikia na kumpakulia kwangu ama unadhani anavyochelewa kuja nyumbani siku hizi anakuwa wapi au jumapili unapokuwa busy na kazi zako unamuacha anaangalia tv kama kasomea uhandishi wa habari akitoka hapo anaendaga wapi anakuja kwangu..akaa kimya tena

akaniambia mbona sikuelewi unachoniambia, nikamwambia leo utanielewa maana nimekuwekea vocha special nikamwambie tafdhali acha kabisa kumchosha mpenzi wetu kama wewe huwezi kazi achia ngazi nikusaidie kwasababu nimechoka kusikia jina lako kila tukimaliza kut********a yani leo mpenzi umenipa raha muache tu huyo ******** azidi kuhangaika na kazi yake nipe raha Rose wangu hayo ndio maneno ya mumeo kila tukimaliza kula tunda la usiku sasa nimechoka kuyasikia

huu ni mwezi wa tano tokea nianze mahusiano na mume wako tulipokutana alikuwa na mawazo na ny******e nakumbuka siku ya kwanza nilitaka kutapika alivyok*****a condom ilikaribia kujaa...halafu wewe daktarai hiyo ndio afya unayofundisha huko wagonjwa wako ama wewe ni hodari wa kutibu wagonjwa wako lakini kumtibu mumeo huna uhodari huo...nikamsonya

basi nilivyomsonya akapandisha hasira na kuanza kunitukana hivi wewe umesoma wewe maneno gani hayo unaongea unajuwa mimi naweza kuwa mtu mzima sana kwako huna adabu wewe mtoto

nikamwambia mama tafadhali aliyekuambia mume anat********a cheti cha shule nani kwani wewe hata siku moja ulishamgea mpenzi wetu cheti akaki*******a au alishakuomba hicho cheti aki********e bibi wee mimi sijasoma ila somo nililokuwa nalo mimi ni kufundisha wanawake kuwa imara kwenye ndoa zao na ukishindwa baada ya kukufundiha kwa kuongea na kuandika nitakufundisha kwa vitendo kama ninavyokufundisha wewe sasa hivi kwa mumeo maana somo yako sijui alikuwa nani wakati unaolewa alisahau hilo

kisa unakaa kwenye nyumba ya ghorofa ndio upo busy kila jumapili kuisafisha hahahahahahaha akaniambia kama unataka na wewe gorofa mwambie huyo mpenzi wako akupe

nikamwambia akinipa mimi ghofofa ujuwe wewe ndio habari yako imekishwa kwasababu nikifikia kumpa ya kumkomoa kisa nataka vitu kutoka kwake wewe utaachwa, ghorofa atanipa na watoto wako nitalea

akaniambia unaubavu huo..nikamwambia ubavu niliokuwa nao wa mpaka kupewa number yako na mumeo ndio huohuo nitakuwa nao atakaponiletea wanao kulea

akaniambia mtu mwenyewe wewe unaonekana mswahili sana hapo ni kwenye simu tu sijui ukionekana ukoje huna hadhi ya kuwa na mume wangu, nikamwambia kweli mimi mswahili nakaa mabibo uswahilini hatari na mumeo huyo kafunga safari kutoka mbezi uzunguni kanifwata mabibo ndipo anapopumzikia kila akitoka kazini

akaniambia mpumbavu kweli wewe nikamwambia mpumbavu wewe uliyesoma unatibu watu ukashindwa kumtibu mumeo..kwako unaniona mpumbavu mumeo ananiona malkia ndio kimbilio lake...nikamsonya akakata simu

nikampigia simu mumewe nikamuhadithia kila kitu na kumshauri awahi kurudi nyumbani hiyo jana halafu amsikilizie mkewe ila hata kama nini asigombane naye na wala asiondoke kama kawaida yake hata kama mkewe ataongea nini au kutukana nini amsikilize tu na kukaa kimya

halafu leo asubuhi anipigie ili anipe yote yaliyojiri

asubuhi na mapema kabla hata sijaondoka nyumbani wala mume wangu hajaondoka simu ya jamaa hiyo nikasema moyoni kudadadeki leo kwa huyu najenga kwangu leo patawaka moto sasa najua nikipokea hii simu story itakuwa ndefu na huyu baba ndio kwanza anavaa hapa na nikiiacha ataniuliza kwanini sipokei hiyo simu...mamae

nikaipokea nikapiga halo, halo mmmhhh mbona unapiga halafu unakaa kimya mtu nipo busy namuandaa mume wangu aende kazini wewe unasumbua halafu huongei hebu angalia number yako vizuri labda umekosea...najiongelesha tu yaani

nikaikata huyo nikaendelea na shughuli zangu mume wangu na watoto wakaondoka nikajiandaa nikafika kwenye gari ndio nikampigia na kumuhadithia kila kitu kwanini nilifanya vile akanielewa lakini tokea mwanzo ndio maana alikaa kimya

akaanza kunipa michapo sasa, dada jana alivyorudi karudi na mihasira hatari kuniona tu kwakuwa nilikuwa na watoto sebleni akaniita chumbani na kuanza kunisema kuhusu wewe eti nina hawara kasema hivi na vile akamuhadithia kila kitu

akamwambia mkewe kweli anamwanamke na ndio huyo aliyeongea naye na akampa sababu ya kuamua kuwa na mwanamke nje akamwambia mkewe anampenda lakini kama atashindwa kutimiza wajibu wake kama mke basi atamuacha na kuwa na rose

anasema yani alivyosikia hivyo alilia sana na kumwambia mwanamke gani huyo kwanza anaonekana ni mdogo na ni mswahili sana yani unanitia aibu wewe mwanaume akalia sana

mumewe akamwambia rose ananiheshimu, ananisikiliza, ananitimizia ya kitanda hivyo vyote mke wangu wewe hunipi upo busy na kazi na ukiwa nyumbani jumapili upo busy na nyumba na mara nyengine mashoga zako yani huna muda na mimi

mkewe akalia sana na kumuomba mumewe msamaha kwamba hakujua anamkwaza yeye alijua ni kawaida tu, mumewe akamwambia ni kawaida kukaa miezi mitano bila kunipa unyumba???

mumewe anasema rose yani alilia sijawahi kumuona ameumia hivyo nikaanza kumbembeleza nikambembeleza tukabembelezana na baada ya miezi mitano jana mke wangu alinipa unyumba tena kwa mapenzi tele na mahaba mengi sana

ulipomaliza tukawa tumelala akawa ananiomba msamaha na kuniahidi atajirekebisha nikamwambia sawa nitashukuru

moyoni nikasema mamae unachezea shilingi chooni watu wapo tayari muda woye kuingiza mkono chooni kuitoa...ukisema wa nini wenzio wanawaza watampata lini...mfyuuu



2 comments:

  1. Hahahaaa safi sn aisee. Mwanamke analeta pozi la kisomi kwny ndoa

    ReplyDelete
  2. Du we mwana we we mkare. Lakini hiyo pia imekuwa tiba, manake wanawake tunajisahau sana hasa tukiolewa

    ReplyDelete