Tuesday, November 26, 2013

Kila mwanamke ana jumamosi na ijumaa yake, hata wakikubania vipi ipo siku wataachia...PART 2

 kipindi chote cha haya yote hakuna mtu yoyote aliyemwambia kitu neema wala kumuonyesha mabadiliko kihisia ambayo yangemfanya neema kuhisi tofauti

basi bwana michael akakutana na kina astazia akaonyeshwa na mwanaume mwenyewe na zile picha na maneno kibao kutoka kwa peter na astazia mpaka akachanganyikiwa

michael wala hakumbadilika neema alikuwa anakufa kiume lakini ndani ya moyo wake alishamuacha neema ila alikuwa anashindwa kumtamkia kwamba hamtaki tena yani alikuwa hajielewi afanyaje

basi huku jamani process za ndoa zinaendelea kumbukeni vikao vikaendelea kukalika kila mtu anajua lake la moyoni kasoro neema lakini wamekaa kimya

basi bwana ikafika siku ya kitchen party ya neema jamani neema hajui kitu mwenyewe akafanyiwa bonge la kitchen party mazagazaga kibao wafanyakazi wenzake wa gazeti wakaja wakampiga picha mpaka ikatolewa kwenye kipengele chake anachoandikaga kwamba anaolewa na hiyo ndio kitchen party yake

alipata vyombo na zawadi nyingi sana za kwenda kuanzia maisha yani watu walikula wakanywa na wakaondoka na zawadi tele

basi bwana ikafika siku ya sendoff neema akafanyiwa bonge la sendoff ukumbi ulipambwa jamani neema alipendeza sana shughuli ikaendelea kama kawaida ikafika pale kamchukuwe mumeo mkale chakula ndio kasheshe ilipoanzia

neema tafuta tafuta na wewe mwanaume hayupo ila ndugu na marafiki wa mwanaume anawaona ila mwanaume hayupo wala bestman hamna tafuta akajua labda huu ni mchezo anafanyiwa lakini mumewe yupo akatafuta mpaka akachoka mwanaume hakuwepo

ndio minung'uno ya watu ikaanza nini jamani mbona mwanaume hayupo ndio neema kuamua kumpigia simu michael na michael kumtema neema kwenye sendoff yake akamwambia hamtaki tena mwanamke mwenyewe kumbe malaya hivi na vile na vile maneno kibao akamwambia tena akome kumtafuta akakata simu na neema kuzimia pale ukumbini

basi ndio huko na kule neema kuamka kuanza kulia no no no haiwezekani jamani watu sasa ndio nini neema kuwaambia michael alichomwambia watu ndio sherehe ikageuka kuwa kilio wazazi wake neema walilia sana kwa ile aibu watu walimuonea huruma neema alivyokuwa analia na wao kuanza kulia

mc akatangaza kwamba inabidi tu watu wale wampe waeze zawadi zao pale mbele halafu waondoke neema hakutaka hata kula akaomba tu aondoke basi pamoja na mama yake wakaondoka mama yake akaenda kumbembeleza mwanaye maana angeweza hata kujiua maana kila saa alikuwa analia nataka kufa mama nataka kufa mama

watu wakala wakatoa zawadi wakaondoka astazia ndio akakusanya zile zawadi zote walizotoa watu ndio kuzipelekea nyumbani kuchanganya na zile zawadi za kitchen party

nyumbani bado neema alikuwa analia sana yani alikuwa kama amechanganyikiwa astazia naye anajifanya kulia na kumbembeleza neema bembeleza sana mpaka neema akalala usingizi

alipoamka asubuhi akawa anampigia michael simu lakini michael alikuwa hapatikani tena hewani number alikuwa ameshabadilisha

basi bwana kama kawaida akalia wee na astazia ndio akawa anambembeleza

neema akakonda sana maana alikuwa hali chakula kabisa yani alikuwa kama amechanganyikiwa akiwapigia ndugu wa michael wenyewe hakuna hata jibu la kueleweka wanalimpa neema basi neema akachoka akaamua tu kujikalia mwenyewe ila mpaka kazini aliomba likizo ya miezi miwili maana alihitaji kwanza kupona hiyo hali inayomfanya aumwe

basi bwana neema akawa nyumbani na yeye yeye na chumbani hata kutoka nje hataki maana angewaangaliaje majirani yani alikuwa tu anaona aibu kilichomchanganya zaidi ni ndugu wanapokuja kila siku nyumbani kumpa pole na kumuuliza kama kuna kitu alimfanyia michael kilichomfanya amuache

basi ikapita miezi saba tokea hilo janga, neema akiwa kazini siku hiyo ametoka jioni anaelekea nyumbani ikasimama gari aina ya vogue pembeni yake na kumsalilimia neema

HAHAHAHAH STOOOPP NAJUWA UNAHAMU YA KUTAKA KUJUA NI NANI ALIKUWA NDANI YA HIYO GARI AKIMUONGELESHA NEEMA, ALIMUAMBIA NINI NA KWANINI...USIACHE KUFWATILIA PART 3

No comments:

Post a Comment