kama
tunavyojuwa kuna kipindi tukifikaga tunaanza kuwaza na kutamani kwamba
siku moja na sisi tuje kuolewa unaanza kupata picha sendoff na kitchen
party yangu nataka iwe hivi na vile, nguo iweje rangi na kadhalika
halafu
katika wale wanaume ulionao kama ni watano au wawili unaanza sasa
kuwapima nani anafaa kuwa mume au yule mmoja uliyenaye unaanza kumpatia
picha siku akikuoa itakuwaje na mambo kama hayo
ndivyo
ilivyokuwa kwa dada mmoja anaitwa Neema na yeye alitamani hivyohivyo
akawa anapenda sana kumuhadithia ndugu yake mmoja anaitwa Astazia kwamba
siku yangu ya ndoa nataka iwe hivi na vile
na
kweli MUNGU alimbariki Neema akapata mwanaume mmoja wa maana anakazi
yake nzuri sana alikuwa ni daktari anapesa yani alikuwa anajua sana
kumuhudumia Neema wakati mwengine za weekend Neema alipenda kutoka na
Astazia kwakuwa walikuwa wanaishi wote waende kuenjoy pamoja na huyu
mwanaume wake Neema.
mwanaume
yule alikuwa anawapa raha sana wakina Neema yani kila mtu alikuwa
anasema mwanaume si ndio huyu na kwakweli kwa mapenzi alimpenda sana
Neema. mpaka Neema hakuamini kama kweli kuna wanaume wa aina hiyo hapa
dar na kuwahadithia wenziye wa kazini na kufurahi nao..Neema yeye
alikuwa anafanya kazi katika kampuni fulani ya magazeti alikuwa
anaandika kuhusu mada za mapenzi na mapenzi kwa ujumla
basi
bwana mapenzi yakaendelea motomoto miezi ikapita ikafika kipindi yule
mwanaume wake Neema kwa jina anaitwa Michael alitaka kumuoa neema na
kuishi naye kama mkewe na kuanzisha familia akamueleza neema kwamba
tokea nimekuwa na wewe sijapata kuona mwanamke mwengine ambaye nataka
kuwa naye, umekuwa mwanga kwangu umeniletea faraja katika maisha yangu
kutokana nahayo kwakuwa nakupenda sana nataka neema uwe mke wangu
tuoane!!!!!
Neema
alifurahi akamkumbatia michael akambusu na kumwambia yupo tayari kuwa
mke wake basi jioni ilipofika michael kama kawaida yake akamrudisha
neema nyumbani neema alipofika tu nyumbani basi akaenda kumwambia ndugu
yake astazia kwamba michael anataka kuja kuwaona wazazi wangu anioe
basi michael na ndugu zake wakajipanga wakaenda kuwaona wazazi wa neema na kuanza process za ndoa
process
zikaanza neema akavalishwa pete ya uchumba, vikao vikaanza kama
tunavyojua vikao huchukua miezi mitatu ndio shughuli basi vikao
vikafanyika neema akapata watu wengi sana waliomchangia
kumbe
huku nyuma astazia alikuwa anawivu na roho kuumia kwanini ndugu yake
amepata mwanaume wa kumuoa na ndoa wakati yeye yupoyupo tu na wote
walikuwa umri mmoja
basi
kwakuwa alikuwa na number ya michael akaanza kumjaza maneno michael
kwamba neema ni malaya yani anawanaume wengi amewapanga wengine
wakumuhonga hela wengine sijui wakuhonga vitu pamoja na wewe yani
usipoangalia utakufa kwa ukimwi maana yule hulka yake ni umalaya hawezi
kuwa na mwanaume mmoja
michael akamwambia sawa nimekusikia lakini unaushahidi kama kweli neema ni malaya??
Astazia
akamwambia wala usipate tabu nitakupa ushahidi, basi anastazia
akamtafuta mkaka ambaye ni rafiki yake ila sio rafiki wa neema na wala
neema hamjui akachonga naye dili na kumwambia atamlipa basi yule
mwanaume anayeitwa peter akakubali
Jamani
hizi simu zetu za kisasa tunazipenda ila ndio chanzo cha matatizo basi
anastazia akamrushia peter picha za neema nyingi tu hata ambazo huwa
walikuwa wakipiga chumbani huku wamevaa kanga na nyengine neema amevaa
tu chupi na sidiria zote akamtumia peter halafu yeye akazifuta zake
kwenye simu yake
siku
hiyo akampigia michael kwamba wakutane ili ampe ushahidi huku michael
moyoni yeye alikuwa haamini kama kweli neema anaweza kufanya hivyo
lakini hakutaka kujiaminisha sana asije akaumia baadae
ILIKUWAJE BAADA YA MICHAEL KUFIKA SUBIRIA PART 2.....
No comments:
Post a Comment