Ulitaka kunitia kiroho dunda lakini wapi, mola amenipa mbora zaidi anayenipenda kwa taarifa yako miye mtu na bahati yangu..hehe heiya liwaendee wote wanaopenda kushobokea mabwana wa watu kisa wivu wako kwenda kumjaza mtoto wa watu maneno amuache yule akuchukuwe weye..haya sasa umeshaachiwa hangaika naye...hehe heiya LAKO HILO
Ulidhani utanikomoa lakini wapi umeshaula na chuya, hehe heiya sijaipata hidhara kwangu ulipomchukuwa kwavile sina papara na mimi nikakuachia, mola kanipa mwengine kaniletea miye mjawa wa stara kama hujanielewa..haloooooooo chezea miyeeeeee
Nimempata mbora mwenye hadhi na muruaaaa sasa nazidi kung'ara donge litakuingia..wapi mama maria na kati ya kinondoni chezea weyeeeeeeee haha halooo analo hilo lishamganda alikung'ute sasa
Kupata majaaliwa nakupasha kabisa huyo uliyomchukuwa mbona anakunyanyasa, kama bado hujajuwa hujajuwa fungu lako la kukosa ukae kuelewa huzibi yangu fursa..hehe heiya wapi muarabu wa dubai ndani ya mburahati chezea siyeeee mola kanijalia kwa mapenzi natakata.
Kwahilo hujanikomoa mambo yangu yananinyookea nimepata mwengine natanua..hehe heiya
Hapo sasa wenye nyonga zaoooooooooooooooooooooooooooooooo wapi dada rehema na kati ya magomeni mikumi chezea siyeeeeeeee
Kwenye meli hii captain miye halianguki ng'o waliopanda jeee hehe heiyaaaaaaa mburahati tumo, magomeni tumo, kinondoni ndio usieme mwananyamala wapiiiiiiiiiii
Na hizo fitina zako mimi ndio riziki yangu tena kanipa ujiko mimi kwa mpenzi wangu anazidi kunipenda mtu na bahati yangu na mimi nimemganda raha zake ndizo zangu..hehe heiya
hapo sasaaaaaaaaaaaaaa mpaka chini...hahaha juuuu....utamrusha nani roho unaniweza miye chezea haohao wakwenu wa huku watakutia doa..
Chezea miye mtoto wa mabibo kulia magomeni, kushoto mburahati,mbele manzese kwa nyuma kishoto kigogo, hahahaa utajuta kunifahamu.
No comments:
Post a Comment