Tuesday, January 29, 2013

Hahaha Vunja Mbavu...

Mwanamume mmoja alimuomba Mungu amjalie ageuke kuwa mwanamke,kwa sababu alihisi mke wake anafaidi kubaki nyumbani wakati yeye anapiga kazi masaa kumi mfululizo.

Mungu hakuwa hiyana,asubuhi alipoamka,akajikuta tayari amekuwa mwanamke.
Haraka haraka akamtayarishia 'mumewe' chai,ili aende kazini,akaogesha watoto,akawapa chai na kuwatayarisha kuwapeleka shule.

Wakati anarudi,akapitia sokoni kununua mahitaji ya siku.Kufika nyumbani,akaanza kusafisha nyumba na kufua nguo.
Wakati anataka kutayarisha chakula,akagundua kuwa umeme umekatwa kwa sababu yadeni,ikabidi atoke mbio kwendakulipa bili ya stima.
Alipotoka kule,wakati wa kwenda kuwachukua watoto ulishafika,ikabidi apitie shule.
Kufika nyumbani,akaanza kutayarisha chakula huku watoto wanamlilia njaa.
Kwa ufupi,hadi kufika wakati wa kulala,bado hakuwa hajamaliza kazi zote,ikambidi aingie kitandanihivyo hivyo.

Kitadani nako hakukuwa na kupumzika.'Mume alitaka apewe kidogo,hakumkatalia.
Lakini baada ya kumaliza tu akamuomba Mungu: "Mungu wangu,nimefanya makosa,kwani kazi anazo fanya mke wangu ni kubwa kuliko nilivyokuwa nikifikiria.Naomba unirejeshe katika hali yangu ya zamani."

"Hakuna taabu kiumbe wangu",Mungu alimjibu na kuendelea,"Ombi lako nimelikubali, lakini itabidi usubiri miezi tisa kwani jana ulipofanya mapenzi na mume wako,ulishika ujauzito!!"

0 comments:

Post a Comment