Asilimia kubwa ya wenye ndoa zenye umri wa miaka mitatu na kuendelea kwa utafiti nilioufanya karibia kila ndoa kuna wanandoa kipindi fulani walishalala mzungu wanne, ndio kwa nini nitakupa sababu zinazofanya wanandoa na kulala mzungu wanne kwa wanaoishi pamoja bila ndoa hao siwezi kuwasemelea kwasababu kila mmoja bado anaficha makucha yake kwa mwenziye kwahiyo mara nyingi matatizo yao huwa sio makubwa kama ya wale walio kwenye ndoa.
Kwanza utakuta mwanaume anarudi saa saba, saa tisa au hata asubuhi kweli wewe mwanaume unategemea utamrudia mkeo saa tisa za usiku halafu akupe mapenzi motomoto na wanaume wengi wanasema kitchen party kwani hamfundishwi mumeo akichelewa kurudi umpokee na umkaribishe, kiukweli kabisa kiubinadamu wewe mwanaume mkeo akikurudia saa tisa usiku utampokea na kumpa penzi motomoto au kwasababu yeye ni mwanamke ndio anatakiwa awe mtumwa??? asiumie moyo asionyeshe kwamba anataka kuheshimiwa na kuthaminiwa??? hapana lazima utamkuta amekasirika tena mwengine hata mlango akufungulii urudi hukohuko ulipotoka lakini yule mstaarabu atakufungulia japo atakupa hata chakula ule lakini usitegemee ukitaka mzunguko utapewa kwa mapenzi na akikupa anatimiza wajibu wake kama mke lakini anamaumivu na uchungu sana, ndio maana wengine wajikuta tu hawataki hata kulala na wewe karibu bora ageukie upande mwengine.
Pili, wanaume wakishaoa huwa wanajisahau sana, yani wanaona kama umeshampata basi ni wako utamuonyesha mapenzi unapojisikia wewe cha muhimu ukirudi nyumbani kila kitu kipo sawa na ukitaka mzunguko upewe, hapana hizo enzi kama zilikuwepo zilikuwa za zamani wanawake siku hizi wamejanjaruka wanataka kupendwa, na sio kupendwa bali umuonyeshe unampenda, umpe muda wako, muongee utakuta wanandoa wengine hata muda wa kukaa na kuongea mambo ya kuhusu familia yao hawana haitakiwi hivyo maana mkiongea ndipo unapozidi kumjuwa mwenzio na kuona msimamo wake kwa familia yake, sasa hiyo attention mke anapoikosa ndipo anakuwa na maumivu moyoni anakuona unamchukulia poapoa na ikiendelea kwa muda mwanamke anajikuta anapoteza mapenzi na mumewe kabisa naye anajikuta hataki kabisa hata kuguswa na mwanaume unamkuta anageukia upande mwengine wakitanda.
Tatu, mwanaume usiombe matatizo yakatokea ndani ya ndoa yenu na mkashindwa kuyatatua sisi wanawake tunapenda kutunzwa kama yai matatizo mnaposhindwa kuyatatua katika ndoa wanawake wengi hutafuta sehemu ya kumalizia matatizo japo sio kwa mzunguko ni kwa maneno atatafuta mtu wa kuongea naye kuhusu matatizo yake ya ndoa na usiombe akampata mwanaume wa kuzungumza naye na huyo mwanaume akawa muelewa na kumsikiliza vyema na kumbembeleza mkeo sisi wanawake hatuna hisia za kuchezea eti huku unamzungusha mchana fatuma jioni unaenda kumpenda mkeo hapana mwanamke akiamua kuzungusha kwa john ataanza na kumpenda john na wewe baba nanihii mapenzi kwako ndio mpaka next time, akikolea na penzi la nje amini na kwambia ataishi na wewe kwasababu ya watoto tu tena wengine ndio mpaka vyumba wanahama akikuheshimu asipohama chumba atalala mzungu wanne.
Nisiwachoshe hiyo ni mifano tu michache ya kusababisha wanandoa kulala mzungu wa nne cha muhimu ninachotaka kuwaambia labda kama uliamuwa kuolewa au kuoa utoe nuksi sawa lakini kila ndoa ni mpango na baraka ya MUNGU hakuna anayeolewa kwa bahati kila mwanamke ametoka kwenye ubavu wa mwanaume kwahiyo ujuwe kama wewe ni mwanamke unamwanaume wako yupo sehemu na kama wewe ni mwanaume unambavu yako inatembea sehemu cha muhimu nikumuomba sana MUNGU amlete kwako na akuwezeshe kuishi naye kwenye shida na raha.
No comments:
Post a Comment