Tuesday, November 13, 2012

Vituko Uswahilini..

Uswahilini jamani hapaishi vituko vya kila aina safari hii japo ya kusikitisha lakini inatakiwa itufunze je wewe kama mume unampenda vipi na kumthamini vipi mkeo akiwa hai na mpaka kufa na mke pia hivyohivyo jiulize unamthamini vipi mumeo akiwa hai na hata akifa.

Kuna baba mmoja alioa na wakazaa mtoto mmoja na mkewe, waliishi maisha ya kupendana kama tulivyokuwa tunawaona nje ila ya ndani inajuwa kuta na wao wenyewe, yule mama akaumwa sana wiki iliyopita akalazwa hospital moja maarufu tu hapa mjini.

Wakiwa hospital siku hiyo yule mama akaomba mtoto wake alale naye pale kitandani kwani alimkumbuka sana kwakuwa mwaaye ni mdogo ana miaka minne alishazoea kulala na mama yake, basi mtoto akalala na mama yake kitandani hospital mpaka akapotelea usingizini, baadaye yule mama akiwa amelala akafariki dunia baada ya muda mumewe kuona hawa watu mbona hawaamki ndio kwenda kuwaangalia na kumkuta mtoto kalala ila mama hana dalili za kuonyesha uzima akajuwa tayari mkewe amefariki alichokifaya ni nayeye akapanda kitandani nyuma ya mkewe akamkumbatia na akalala.

Yani bwana haya mambo kila mtu anashangaa na hatuelewi kwanini hakuna mgeni mwengine aliyeingia kumtizama mgonjwa wala muuguzi hakuingia wakalala muda mrefu mpaka muuguzi alipoingia akawaamsha yule baba alipoamka akamwambia muuguzi kwamba mkewe alishafariki ndio yule muuguzi kuchanganyikiwa kwanini hukutoa taarifa na umelala naye hapo??? basi wakamchukuwa kumpeleka kumuhifadhi ndio muda sio mwingi ndugu nao wakaja ndio yule baba kuwaeleza mkewe alishafariki ndio vilio vikaanza na taratibu za mazishi kuendelea.

Wakarudi nyumbani kwenye msiba yani hamuwezi amini yule babga hakuwa hata kama mfiwa hakutulia kuomboleza yeye alitaka afanye shughuli zote mwenyewe, hakutaka kupewa pole ya msiba wala kuhurumiwa, na cha kushangaza ni kwamba alitaka maiti ikachukuliwe hospital ilazwe ndani mpaka wakati wa kwenda kumzika!!! tena alikuwa mkali kweli na kusema kama hakuna atakayekwenda kuichukuwa angeenda mwenyewe.

Watu ndio wakamkatalia na ugomvi kubuwa ukazuka mpaka kushikiana mapanga mume mtu na ndugu wa mkewe, akasema sisi wenyewe tulishapanga kila mtu akifa itakuwaje kama nitatangulia mimi nilishamwambia afanyaje na akitangulia yeye alishaniambia nifanyaje na hivi ndivyo alivyotaka kwanini nyie mnizuie, basi ikawa ugovi tafrani mpaka dakika za mwisho wakakubaliana kwamba kuamkia siku atakayozikwa siku hiyo ndio maiti ikachukuliwe ilazwe ndani halafu kesho yake ndio ikazikwe.

Na kweli maiti ikachukuliwa hospital mumewe akaenda kumnunulia jeneza zuri kila mtu alilishangaa, akaletwa kutoka hospital nakuwekwa sebleni pale ambapo watu walikuwa wamelala japo mumewe alitaka akalale chumbani na mkewe lakini walimkatalia, basi asubuhi ya kuzika ilipofika yule mume akaamka akaja na vitenge vya wax vipya akalifungua jeneza la mkewe mwenyewe lote akamvalisha mkewe zile wax hakutaka kusaidiwa akamfunika vizuri mpaka miguuni akalifunga msiba ukanedelea.

Muda wa kuzikwa ulipofika wakaenda makabaruni yule baba hakutaka kukaa kuona mkewe anazikwa akaingia kaburini na waliozika akamzika mkewe na kulijengea lile kaburi baadaye ndio akaondoka na kusema hataki mtoto wake achukuliwe na ndugu yoyote hivyo ndivyo walivyokubaliana na mkewe kwamba mtoto ataenda boarding na ndio hivyo itakavyokuwa na kuwaambia kwa vile mmeshazika sasa kila mtu anede kwake aniache na mwanangu.

Ni ngumu kuamini lakini ni kweli, na inataka moyo sana je wewe na mwenzako huwa mnaongea ukifa akufanyiaje, umejiandaa kama siku moja utakufa ama unaipotezea tu hiyo siku.

Mimi nimejiandaa kufa siku yoyote MUNGU atakaponichukuwa na mara kwa mara huwa na mwambia mume wangu nikifa afanye hivi na hiki asifanye, ila cha muhimu ni kwamba kaburi langu ahakikishe walijengee na tiles ili nisije nikazikiwa na mtu mwengine juu na watoto wangu wapate kuja kukaa na kuongea na mimi wakinikumbuka. Ila kwa sasa bado niponipo sana sijamaliza kazi MUNGU aliyonipa kuifanya hapa duniani.

Wewe je unaitambua kazi yako MUNGU aliyokuwekea hapa duniani na unaifanya atakavyo hata akirudi leo akikuuliza utampa jibu zuri.....tafakari na ukumbuke wote tupo njiani

0 comments:

Post a Comment