Tuesday, November 6, 2012

Unaijuwa ndoa wewe ama unaitaka tu..

Jamani wanawake kila mmoja sasa hivi anataka ndoa ni wachache sana wasioitaka ama kama labda unasomea usista ndio ndoa huitaki basi tu ilimradi na wewe watu wamekuja umekaa pale hightable tunasaza kwa kula na kunywa ndio furaha ya kila mwanamke na ndio baraka ya kila familia kila mzazi anataka na kumuombea mtoto wake siku na yeye aoe ama aolewe.

Shoga lakini umejipanga ya baada ya ndoa, shoga unakifua, shoga we mbabe maana bwana kuna ndoa nyengine kama wewe sio mbabe shoga itakushinda, maana utakumbana na vipepsi vya mawifi ushangae na maisha yako, huyo mama mkwe je utakuta mdomo kauvuta mpaka nyuma ya kisogo akikuona unakumbatiwa na sweety..inahusu

Jamani wanawake mnaotaka kuingia na mlio kwenye ndoa mtambuwe kama ndoa ni kama TV yako nyumbani shoga siku nyengine umeme ukiwa mdogo utaiwasha mpaka vidole viumie ng'o haiwaki, ila umeme ukiwa sawa ukiwasha tu kidogo bila kutumia nguvu inawaka, na sio kuwaka tu siku nyengine tv inaonyesha chenga na siku nyengine clear hayo unayajuwa shoga ama wewe unataka kutembea na magold tu mkononi kama mchimba madini ilimradi tu na wewe tukujuwe unandoa ukitikiswa kidogo tu unaondoka shoga vipo vyakukufanya uondoke lakini sio mwanamke mwenzio.

Maan siku hizi kesi nyingi oohh mwanaume malaya nimeamua kuondoka, wanawake hawamwishi shoga kuna njia nyengine za kujikinga na hayo matatizo lakini sio kuondoka ndio maana wanawake tunakutana kila mara kufundwa kuhusu ndoa na mahusiano kama kwako baridi kwa mwenzio kunafukuta joto.

Naujuwe kufundwa huku kwa haja sio maneno ya juu juu tu shoga unapewa kama lilivyo jeupee huku sisi hatufichagi mambo kama unajipenda na kumpenda mwenzio tukutane upewe maujuzi zaidi hiyo 7/12/2012.

Heshima ya mwanamke sio madegree tu heshima utunzaji bibi..

No comments:

Post a Comment