Monday, November 26, 2012

TUMETOKELEZEA..

Ohhh kila siku mlikuwa mnanisema kwanini sioi haya sasa ongeeni lengine my wife wangu ndio huyu hapa


Cheki toto toto mwanamke kujiamini bwana sio ukiambiwa ongea mbele za watu unaanza kutetemeka kama una degedege wanaume siku hizi wanataka kuoa mwanamke anayejiamini idara zote anaingia kwa nguvu ya tano.

Kijana unaona mtoto alivyonaafya yake huyo, unaona alivyo jaa sasa kamrushe roho umrudishe kwao kilo na nusu.

Wanaume wengi jamani utakuta wanaoa wake wazuri, wanamiili mizuri watoto wameshiba basi kero za kwenye ndoa muda mchache tu mara mtoto wa watu anaanza kutereka huh kama kwao hali unadhani hapo kwako kafwata chakula kafwata mapenzi hebu mjitahidi wanaume na ndoa zenu wapeni raha wake zenu yani azidi kuwa mzuri zaidi ya ulivyomtoa kwao,hiyo ndio heshima ya mume.



Hiki ndio chakula chetu cha kwanza pamoja kama mke na mume tukikate tule na tusiusahau utamu wake kwani kila tutakachokula pamoja kwanzia siku ya leo mume wangu kitakuwa kitamu kama keki hii, mwili wako utabadilika na kila mtu atajuwa na kuona faida za wewe kunioa.

Na sikuzote nakuahidi mke wangu nitafanya kazi usiku na mchana nikulishe vyakula vitamu na vinunono kama hii keki ninayokupa sasa.

Kula mke wangu, kula ufaidi matunda ya kuwa mke wangu hata baada ya miaka kumi hubaki na mwili wako huu niliokuoa nao.


Siku hizi rangi mpaka raha yani ushindwe mwenyewe umeona Purple and Yellow hiyo..mmhh mngekuwa embe ningewala na maganda kwa jinsi mlivyonoga.

Hehe heiya umeona wanja wa jicho la mke mwenza..mwanamke pambo bwana chezea lijicheni hilo


Mmmhh hapana jamani wanawake kabla mumeo/mpenzi wako hajatoka ndani kwenda kwenye mihangaiko ama sherehe hivi unamkaguwa? unajuwa kama nguo aliyovaa haimbani, imechanika ama kupauka ama kisa mmenuniana na kulala mzungu wa nne unamuacha tu na kumpotezea shoga mnaaibika wote nini sasa kuwa na msaidizi ndani au kisa dada anafua nguo ndio akusaidie mpaka kumvisha mumeo..salaleee


Mwanamke kiuno haswa ukiwa unacho cha kushikiwa na kukizungusha


Tunashukuru wote kwa kuja na MUNGU awabariki, Tchao

No comments:

Post a Comment