Wednesday, November 21, 2012

Tumetokelezea...


Wacha nijishebedue mke mwenzangu anijuwe..hehe heiya chezea kuolewa hebu nipishe miye niende zangu


                               Inuka wakuone mpenzi wange wee, uliyejaa moyoni mwangu wee

    Hehe heiya chezea machejo vaa wakuone mume wangu, wenye roho za korosho ziwakerekete

Na wafe nazo kweli miye ndio nimeshakuchaguwa wewe uwe wangu kifo tu kitutenganishe

Nichum basi..Mwaahh na tena Mwaah tena Mwaah bwana tena Mwaaaaaaaaaahhhh



Mume wangu mbona mkono wako ujoto..nikiwa nawe damu inanichemka mke wangu kwa mahaba tele



Basi na mimi nakuahidi nitazidi kuwa mtamu siku zote za ndoa yetu na kwa keki hii nakudhihirishia utamu wangu hatukaa uishe kamwe



Katika wanawake wooote nimekuona wewe ndio unafaa kuwa mke wangu na mama wa watoto wangu nimechoka mke wangu tuage wazee watupe baraka tuondoke tukapumzike



Nawabariki wanangu, mke ukamtunze vyema mumeo katu usimnyime unyumba ukamkatikie viuno na kumpa yote uliyokuwa unaenda kufundwa kwa makungwi mara kwa mara kama mama yako alivyokuwa akiniambia ninaporudi nyumbani sikukuti mumeo akabadilike kimwili na kiafya aonekane tofauti ya kabla hajaoa na alivyooa akawarushe roho kila mwanamke akimuona amtamani hapo ndipo tutakapojuwa umefundwa na kukomaa kulea mtoto wa mwanamke mwenzio nendeni sasa mkapumzike.



Tunawashukuru wote kwa kuja kwaherini na MUNGU awabariki.

No comments:

Post a Comment