Tuesday, November 20, 2012

Tumetokelezea..

Wapendwa ndoa ni baraka na nimpango aliotupangia MUNGU na tunajuwa ya kwamba inashida zake lakini raha zake ndio nyingi, tumekuwa tukipata posts nyingi za kuhusu ndoa nyengine mpaka unashindwa utaipost vipi hapa maana ni nzito inabaki tu kuijibu juu kwa juu maana mengine yanaweza kukatisha watu wasiingie kwenye ndoa kabisa, ndoa ni raha jamani na unathaminiwa zaidi ukiwa mume au mke wa fulani mengine ni nyongeza..Usiwe nyauba wa kuliwa na kuachwa tu na wame za watu kisha wawakimbilie wake zao mwanamke ndoa, mwanamke kujiamini kumiliki wako sio wa watu. hehe heiya lako hilo kama limekuchoma na kukukereketa na litakubugdhi mpaka ulitapike.

Sasa basi kwa wale ambao hawajaingia na wapo njiani kuingia kwenye ndoa ninaanzisha hii TUMETOKELEZEA hapa tutakuwa tunaonyesha harusi mbalimbali kuwapa ideas nguo gani ushone na nini ufanye kwenye shughuli yako kwani harusi ya kwanza ndio yenye maana na yenye kukaa katika kumbukumbu hata ukiachika na kuolewa tena itakuwa ni marudio tu.

Unaweza ukapata mshono, ukumbi mzuri na mengine mengi ya kuhusu harusi haswa kwa wewe ambaye unataka kuingia na uliye na ndugu anayeingia.

No comments:

Post a Comment