JAMANI niokoeni, ninakufa ni kauli ya huzuni iliyotolewa na mtoto Swakimu Erius ,14, mkazi wa Mtwara aliyekata tamaa ya kuishi kufuatia kusumbuliwa na uvimbe usoni.
Akizungumza kwa shida na mwandishi wetu juzi katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa, Swakimu alikuwa na haya ya kusema:
“Ugonjwa huu ambao sijui chanzo chake umekuwa ukinitesa sana na kunifanya nishindwe kuendelea na masomo katika Sekondari ya Libobe, Mtwara.
“Uvimbe unaonitesa ulianza kama kipele lakini kadiri siku zilivyokuwa zikisonga mbele uliongezeka ndipo nilikwenda Hospitali ya Mkoa wa Mtwara ambapo walinitibu kisha waliniambia nije hapa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
“Kinachonihuzunisha sina msaada wowote kwani ndugu yangu aliyenipokea hana uwezo na ninatakiwa kutoa gharama za matibu shilingi 90,000 na damu,” alisema mtoto huyo.
“Nawaomba Watanzania wanisaidie kiasi hicho cha fedha na damu ili nifanyiwe upasuaji ambao nimeleezwa na madaktari kwamba utaisha na kuwa na afya njema,” alisema Swakimu.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili, Mary Ochieng aliomba kijana huyo asaidiwe kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia.
Yeyote aliyeguswa na maradhi ya kijana huyu aende wodi namba 23 Sewa Haji, Muhimbili .
MUNGU anapokupa afya njema wewe pamoja na familia yako unakumbuka kumshukuru au hata kusaidia wanaohitaji msaada wako???? tumtafakari na kumuogopa sana MUNGU
0 comments:
Post a Comment