Sunday, November 11, 2012

Haya sasa...

LILE tukio la madai ya wanandoa kusaliti ndoa zao kwa kwenda kuzini gesti na hatimaye kugandana, bado linaendelea kuumiza vichwa vya baadhi ya Wabongo kuhusu ukweli wake, Ijumaa Wikienda lina mpya.

Novemba 8, mwaka huu, saa 5 asubuhi, umati wa wakazi wa Jiji la Dar ulifurika kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Temeke kushuhudia tukio hilo.

Mapaparazi wetu walifika eneo la tukio ambapo dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Margret alithibitisha kuwaona wagoni hao wakishushwa kwenye gari aina ya Canter huku wamefunikwa shuka moja jeupe.

Aidha, gazeti hili lilimshuhudia bibi kizee aliyefika eneo hilo na kusema hilo ni tego ambalo analifahamu na kuwahi kulishuhudia mara kadhaa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Akilipa ushuhuda gazeti hili, bibi kizee huyo aliyekataa kutaja jina lake, alisema yeye alifika eneo la tukio lengo likiwa ni kuwanasua wawili hao lakini alisikitika akisema alinyimwa ushirikiano.

Bibi huyo aliyetokea Tanga, anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 75, alisisitiza kuwa, tukio hilo ni la kweli na kusema hata waliosema wameshuhudia walishindwa kulifuatilia vizuri kwa sababu suala lenyewe lilikuwa na mazingara ndani yake.

Alisema aliyeliona mwanzo lilimpotea katika hali ya kimazingara kutokana na macho yake kutokuwa na uwezo wa kuona zaidi ya alichoanza kukiona awali.

“Hapa Dar es Salaam, dhambi ya zinaa imezidi sana. Mungu ameamua kuonesha miujiza yake,” alisema bibi huyo akiwa na dawa zake mkononi.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Amani Malima alipohojiwa, alikanusha kutokea kwa tukio hilo.

Baada ya hapo, mapaparazi wetu walifika kwenye Gesti ya Mchei inakodaiwa ndiyo kulitokea tukio hilo na kuzungumza na mhudumu wa mapokezi, Masha Abdallah ambaye alikanusha tukio hilo kutokea.

Mmiliki wa gesti hiyo, Salmada Mchei naye alisema tukio hilo halijatokea na anashangaa uvumi huo umeanzishwa na nani.

0 comments:

Post a Comment