Tuesday, October 23, 2012

SOMO...

wanawake wengi sana tunapenda kutumia udi mimi nikiwa mmoja wapo na katika kutumia udi kuna vichotezo vya aina mbili vya bati na vya udongo tunashauriwa sana kama unamtindo wa kujifukiza udi kila siku utumie cha udongo na sio kila siku unajifukiza kwa bibi moja kwa moja.

Unapotaka kukutana na mumeo ndio ukajifukize kwa bibi tena kutumia chotezo cha udongo maana ukiwa unajifukiza mara kwa mara kwa bibi na chotezo cha chuma wanasema kinavyozidi kuungua na kuingia ndani mwako kina uwezo wa kusababisha saratani kile chuma kinavyochoma mara kwa mara ndio maana wanashauri kama unapenda sana udi jifukize na vya udongo.

Napia kama unataka kujifukiza udi na sio kwa kwenda kufanya mapenzi basi vaa nguo zako na ya ndani ikiwemo chukuwa choteco weka udi wako jifukize ukiwa umevaa nguo pamoja na ya ndani, na kumalizia usiache kufukiza nyumba yako haswa chumbani kwako maana pale ndipo unapomalizia uchovu wako wa siku nzima.

No comments:

Post a Comment