Tuesday, October 23, 2012

SOMO..

Wanawake haswa wewe uliye kwenye ndoa nataka uelewe jambo moja katika usafi wa mwili wa mumeo na labda umuelekeze na yeye maana kuna wanaume jamani wakivua nguo zao za ndani wanatoa harufu yani wananuka, wao wanaume kuoga ni mara moja tu na huwahi kusaka hela kwahiyo siku hiyo moja kama ni jumapili au jumamosi yupo nyumbani ni wajibu wako wewe mama kumueleza, kumuelekeza au hata kumchukuwa mumeo kwenda naye kuoga ili uweze kumsugua vyema.

Katika mwili wa mwanume kuna vile vigololi viwili chini ya uume (napunguza ukali wa maneno nazani mtanielewa maana hii ni blog ya jamii na jamii lazima iheshimike) na vigololi vile kwakuwa vinakuwa ndani ya chupi na suruali vikipata joto vinatoa jasho na mafuta meupe ambayo mpaka uyachunguze ndio unaweza kuyaona sasa yale ndio yanayofanya mwanamme anuke kama hajioshi vizuri na ndio maana mwanaume akitoa nguo yake ya ndani yani unaweza sikia harufu kali sana ndio hivyohivyo kama sisi wanawake usipojisafisha vizuri kuna majimaji ndani yetu, ute na mikojo inayosalia ambayo intakufanya unuke vibaya sana kama shombo.

Kama ulikuwa unajiuliza ni kwanini huyu dada ama huyu kaka hunuka basi hio ndio sababu na dawa yake ni usafi tu.


1 comment:

  1. Jamani jamani mi nalia na hao wanawake waloolewa na kila kuchwa kutaka kuitwa mrs, ila huyo mr wake anatema balaa, asubuhi tu umekutana nae mwanaume domo lanuka, kikwapa chanuka, ana harufu kama mamilioni, eti na yy ana mke, jamaniii huruma.
    Hivi sie wanawake wa siku hizi tuna nn?? Babuu waambiwe wawakogeshe waume zao na wawasugue kila kona, si mume wako, na mpaka kwa mungu umehalalisha sasa kumpekua kila idara wanaona noma za nn. Vuziii vuzii linyolewe babuuu, kaah baba kaachwa na vuzi mpaka linamkata huyo mkewe mwenyewe nn lkn??
    Vuzii na joto la dar hili wee, baba hata rollon wacha perfume hana, eeeh mama wee hilo vundoo hujawahi ona.wasutwe siku hiyo, sio kuambiwa

    Tum

    ReplyDelete