MTOTO yatima Juliana Mwinuka, mkazi wa Kijiji cha Mavanga, wilayani Ludewa, mkoani Njombe aliyeungua usoni baada ya kuangukia kwenye moto kutokana na maradhi yake ya kifafa, amehamishiwa katika Hospitali ya CCBRT akitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Habari za mtoto huyo zilichapishwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika gazeti ndugu na hili la Amani.
Mwandishi wa gazeti hili Francis Godwin aliyemuibua mtoto huyo kijijini Mavanga, akiwa hana msaada wowote kutokana na ufukara wa mtu anayeishinaye alipozungumza jana na gazeti hili ameeleza sababu za kuhamishiwa katika hospitali hiyo.
“Amehamishiwa CCBRT kwa kuwa kuna taarifa kuwa kuna madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali duniani watafika hapo kwa ajili ya kuwafanyia matibabu wagonjwa tukaona ni vyema akapata bahati hiyo,” alisema Godwin.
Alipoulizwa hali yake kwa sasa ikoje, Godwin alisema: “Hali yake imeendelea kuleta matumaini baada ya kuanza kukaa mwenyewe huku akiweza kuinua mikono jambo ambalo linazidi kututia moyo.”
Alisema anawashukuru wale wote walioguswa na kutoa msaada kutokana na tatizo la mtoto huyo aliyeungua kwa kuangukia moto kutokana na kusumbuliwa na kifafa.
Wote walioguswa na habari ya mtoto huyu na kuwa na moyo wa kumsaidia wawasiliane na mratibu wa matibabu yake ambaye ni mwandishi wetu kwa namba hizi M-pesa 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199.
Source: Global Publishers
0 comments:
Post a Comment