Monday, October 1, 2012

Angalizo...

 Jamani sisi kama wazazi hivi tunakuwaga na muda kweli wa kuaangalia watoto wetu hata mara moja kwa wiki ipasavyo? ukiangalia na hivi tunavyobanwa na majukumu kazini na sehemu za kutafutia tonge..

Nyumba nyingi sana siku hizi zinawasichana wa kazi, lakini sio wasichana wote wapo makini kwa watoto ni asilimia chache tu, je wewe kama mama umeshawahi ukiwa nyumbani hata kama ni siku moja tu ya wiki kumchunguza mtoto wako awe wa kike ama wakiume, umeshawahi kumuangalia maumbile yake kama ni mzima au vipi kwa nini ninasema haya;

Jana uswahilini kwetu kumetokea jambo ambalo limenisikitisha na kuniuma sana, kijana mmoja ambaye yupo form one amekamatwa kwamba anatabia za kulawiti watoto, sasa hivi alimfanyizia mtoto wa miaka minne!!!!!!!!! baada ya mama yake jana jumapili kuwa nyumbani na kukaa karibu na mtoto wake wa kike nakugundua anatoa harufu mbaya huko kwa bibi.

Baada ya kuona hivyo akaamua kumuita mwanaye chumbani na kumvua nguo na kumwambia alale kwenye kitanda baada ya kumchunguza akagundua anatokwa na uchafu mwingi huko chini na pamechezewa ndio mama kushtuka na kumuuliza mtoto kwa upole ili mtoto asiogope na kushindwa kumjibu, basi yule mtoto akamtaja kwamba yule ananifanyiaga hivi!!!!

Basi ndio yule mama kupagawa kwenda kwa yule mtoto kwakuwa ni jirani kumbana kweli na kwa vitisho ndio yule mtoto kukubali na kuanza kulia akiomba msamaha, yule mama wa mtoto wa kike hakutaka kuelewa hayo akambeba pamoja na mama yake mpaka polisi ambako alikaa huko mpaka jioni ndio ndugu zake yule mtoto wa kiume kwenda kuomba radhi na kumbembeleza sana yule mama amsamehe na kumtoa kijana wao.

Baada ya muda mrefu sana wa kuvutana huku na huko baadaye yule mama akakubali kumsamehe mbele ya mjumbe wa nyumba kumi na kumwambia kwamba ahame mtaa na kila mzazi mtaani hapo akakubaliana na hilo swala kwamba yule mama na mwanaye wahame.

Inauma sana sasa hapa afadhali mtoto alikuwa anajuwa kuzungumza je kwa watoto ambao hawawezi kuzungumza vizuri, sio wa kike tu siku hizi hata wanaume hufanyiwa hivyo..jamani tuwe makini tusikimbize sana tonge tukasahau majukumu yetu kwa watoto wetu.

0 comments:

Post a Comment