Jamani leo kuna jambo nimesikia sikuliamini nikaona hata hapana lazima niulize na miye kwa wale wanaoweza kujuwa kama ni kweli.
Mimi hependelea sana kula papai, sasa leo kuna sehemu nilikuwa na rafiki yangu mmoja wakati tunakula nikamalizia na kula papai kwani nililiona lilikuwa linanivutia sana basi mwenyewe nikiwa najinoma akaniuliza kama mimi huwa ni mpenzi sana wa papai nikamwambia sana..nilichoambiwa baada ya hapo nilichoka safsi na roho eti ya kwamba kula sana papai kunapunguza hamu ya kutaka kuchuma tunda!!!! nikamwambia itakuwa ngumu mbona nayala sana na kila mume wangu akibeep nampigia akaniambia siku zinavyozidi hamu nayo itazidi kuisha nikamwambia labda inakuwa hivyo kwasababu ya umri unategemea niwe na miaka 60 bado purukushani na kupinduliwa huku na huko kama unakaanga samaki zitakuwepo tena nguvu sizitaniisha??? akabaki anacheka
Je wewe unayefahamu haya je ni kweli papai ukila sana na ukiwa na utamaduni wa kulitumia sana hupunguza hamu na nguvu ya kuchuma tunda??
No comments:
Post a Comment