Monday, August 6, 2012

Hili nalo sasa...

Jamani imenibidi tu niandike hii story inayomuhusu rafiki yangu mwenyewe karuhusu niiweke humu apate kusaidiwa kimawazo nini la kufanya.

Agnes ni mdada wa miaka 33 mwaka jana alipata mchumba ambaye alikuwa anataka kumuoa, wakwe walishakutana na vikao vilishaanza nakumbuka nilipewa mimi tenda ya kupika chakula cha kikao cha kwanza (acha nijisifie kidogo!!!!) na vikao vilifanyika pale 92 Hotel Sinza Lego nazani wengi wenu wanapajuwa.

Yeye na mchumba wake walikuwa wanaishi marekani yani sisi tulikuwa tunafanya vikao huku then wiki mbili kabla ya ndoa walikuwa ndio warudi kwa ajili ya kuoana na wakati huo shosti alikuwa anamimba ya miezi miwili, kwa kabila hawa wote ni wachagga.

Tukiwa katikati ya kikao cha tatu tulipigiwa simu ya kwamba tuache kikao yani tusiendelee na vikao mpaka tutakapoambiwa tena, na alisema sababu angetoa baadaye yani atampigia simu mama yake then atuambie kwenye kikao, basi shosti miye nilivyokuwa mwingi wa habari wala sikutaka kusubiri mpaka mama yake aanze kusambaza habari nikamwendea mwenyewe hewani kupitia........ akaniambia kwamba jamaa haeleweki kabisa ameanza kumshtukia kwamba jamaa anamchukulia poapoa na anataka kwanza kufanya uchunguzi kabla hajaendelea na process za ndoa, basi nikaachana naye na kumwambia aniambie baadaye atakachokijuwa kuhusu huyo mchumba wake.

Wiki mbili baadaye akanipigia simu akiniambia kwamba amegundua yule kaka anamwanamke wa kikenya anayemzingua, alipomuuliza hakupewa jibu la kueleweka lakini jamaa tu alianza kupunguza mawasiliano na kuonana na Agnes, huku shosti akiwa na mimba na kwavile alikuwa anakaa na wadogo zake na dada zake huko basi walimwambia asiwe na stress atunze kwanza mimba yake, basi akafanya hivyo tokea mchumba alivyomuacha na mimba ya miezi miwili hakumuona tena mpaka baada ya kujifungua.

Baada ya kujifungua mtoto sasa anamiezi sita, alipokuwa na miezi mitatu akasikia kwamba yule kaka anataka kuoa yule mkenya, japo anasema roho ilimuuma lakini hakuwa na lakufanya ila balaa ilianza ile siku yule kaka alipokuja nyumbani kwa shosti na kudai mtoto wake kwamba anamtaka!!!!!!!!!akisema kwamba sisi wachagga huwa hatuachi damu zetu zikitembea ovyo barabarani.

Hakuna mwanamke atakayekubali uje tu from nowhere baada ya kuniacha kwenye mataa na mtoto halafu sasa kazaliwa eti akupe tu just like that!!! ebo unachanganyikiwa...basi ukawa ugomvi sasa ndugu nao wakaingilia kati mpaka wakwe kwa wakwe sasa huku Tanzania familia zikawa hazielewani tena wakati miezi kadhaa tu walipendana na kuheshimiana, yule kaka akadiriki kumwambia Agnes kwamba atafanya juu chini heri amuue mtoto kuliko kukosa damu yake!!!!!!!!akaondoka

Bado hajarudi tena, Agnes anaogopa akienda kuripoti anaweza anyimwe tena visa huko maana anakaa na visa ya studying wakati yule kaka anauraia wa pale marekani anaweza akamfanyia vurugu akarudishwa na wakati shule hajamaliza, na alikuwa na mpango atakapomaliza shule aombe kazi huko yani maisha yake yote ayahamishie marekani, wazazi wake wanamuambia bora amtume mwanaye huku Tanzania wamlee, bado ana hekaheka hajui la kufanya maana anasema sijui ataishije mbali na mwanaye na hivi bado ananyonya...wewe unaona Agnes afanyaje?

MMhhh


1 comments:

  1. Hapo huwezi pata jibu kamili maana umesikiliza kesi upande mmoja.

    Tayari umeshasema kaka ana uraia wa kimerekani na shoga yako ana student visa ya marekani. Inawezekana shoga yako alimpenda kwa sababu kaka alikuwa ni raia wa huko akajua hiyo tayari ni BINGO kumbe mwenzie alikuwa mpita njia.

    Kama ana uchungu na mwanaye mwambie arudi nyumbani na mtoto na kama elimu ni more important kwake basi atume mtoto kwa wazazi.Maisha ni mahali popote iwe marekani au Tz. Kama mtu utajipanga sawasawa na ukawa determined na kile unachokifanya katika maisha yako basi kwa nguvu za Mwenyezi Mungu hakuna lisolowezekana.

    Ivi majuzi kulikuwa na kesi ya kaka mmoja mtanzania aliyeenda marekani kwa kozi ya miezi 6 baada ya kumaliza kozi akataka kuendele kusoma huko alichofanya alitafuta mdada mtanzania ambaye alikuwa na uraia wa huko tena na watoto 3 akaoa. Bahati mbaya yule kaka alifariki. Hii story ni ndefu sana ila nimeishia hapo ili uone ni jinsi gani maisha ya USA yalivyo. Kwahiyo dada usisikilize upande mmoja wa story. Find out the other side of the coin.

    ReplyDelete