Tuesday, August 28, 2012

Heka Heka Imenikuta Miye Leo..

Jamani mmhhh haya mambo ya kutuma hela mikoani kutaka house girl halafu hatuwajui walipotoka mbona kasheshe maana najuwa ningejuwa wazazi wake ningewauliza maswali kuhusu binti yao.

Maichana wangu wa kazi amekuja kwangu ana mwezi na wiki mbili sasa, kama kazi anajitahidi kufanya anapenda sana kufua yani nguo chafu huwezi kuzikuta kwenye tenga, na kupika ndio usiseme yani sijawahi kupata msichana wa kazi anayejuwa kupika kama huyu, mapenzi kwa watoto sio sana anajitahidi lakini sio wa kumsifia kwamba anapenda watoto hakuna kitu ambacho hapendi kufanya kama kudeki!!!!! vumbi kila kona atafuta lakini nyumba kwa wiki mbili naona inadekiwa mara moja.

Chakushangaza zaidi hapendi kabisa kula, yani tukikaa kula chakula anachopakuwa ni kidogo hata mwanangu khloe hawezi shiba, nimeumiza sana kichwa kufikiria kwanini hapendi kula nikimuuliza anasema hawezi kumaliza chakula kingi sasa hata hicho kidogo anachopakuwa kumaliza ni lisaa lizima.

Wiki moja iliyopita nilikuwa na mke mwenzangu kwangu nikamuita dada amuhudumie kinywaji dada alivyokuja tu na kumuhudumia alivyoondoka nikamuhadithia mke mwenzangu kuhusu huyo dada akaniambia hebu muite tena na ujifanye unamtuma akamuangalia na kuniambia msichana wako mjamzito!!!mmhh wala sikumuamini nikamwambia labda kwa vile mnene tumbo ndio maana kubwa basi tukaishia hapo.

Sasa juzi watoto wangu pamoja na dada wameenda kwa bibi yao kwa wiki mbili siku ya kwanza tu walipofika maana sikuwapeleka mimi mama akanitumia ujumbe kwamba msichana wako ana mimba kubwa tu!!!! akili sasa ndio ikanikaa sawa kwamba kweli yule mjamzito.

Ndio nikapata jibu maana bafuni kwa dada kunasehemu ya kuwekewe sabuni na vikorokoro vya chooni vyote nikiangalia pads za bafuni hapo bado zipo kama nilivyozinunua maana nakumbuka nilimuuliza mwanzo wa mwezi akaniambia bado labda kipindi hiki hajapata, sikumuuliza sana nikajuwa labda kwasababu kabadilisha mazingira na kuna namba ya simu kila siku lazima ipigwe mara nne au tano namba hiyohiyo kila siku!!!!nikimuuliza oohh kaka yangu, jamani kwani siye makaka hatuna kila siku kaka yako unaongea naye nini mara tatu au nne afadhali ungempigia hata mama yako.

Jamani haswa wa mama nataka nihakikishe kweli ni mjamzito sawa mama kwakuwa ni mtu mzima anajuwa nafikiria nimpimie nyumbani hii ni sawa maana nikimwambia twende hospital akikataa je?

yani nikifikiria hekaheka za kutafuta msichana wa kazi nasikia kuchanganyikiwa.

No comments:

Post a Comment