Dada Rose, leo naandika kwako nikiwa na furaha tele na nikizidi kumshukuru MUNGU kwa kunitendea miujiza, na ushuhuda wangu huu leo nataka niwashuhudie na kumpa moyo kila aliyekuwa ama anayemuomba MUNGU kitu fulani katika maisha yake kama ni chema na kinampendeza yeye aliye juu mbinguni basi asikate tamaa ipo siku na yeye atajibiwa kwa wakati wake hata kama miezi imepita, miaka lakini siku tu MUNGU atasema imetosha mwanangu na kukupa.
Mimi niliolewa mwaka 2000 na miaka mitatu baadaye nikabahatika kupata mimba ambayo kwakweli mpaka nilipoipata nilimshukuru MUNGU maana nilisemwa sana na mama mkwe na mawifi, kila akipiga simu lazima aongee na mimi na kuniuliza lini ningempa mjukuu, hao wifi zangu ndio balaa maneno kibao kila tukikutana kwenye shughuli za familia lakini sikukata tamaa bado niliamini kwamba ipo siku nami nitakuja kuitwa mama na mpaka pale nilipobeba ile mimba.
Nilifurahi sana, na kumshukuru MUNGU na mume wangu na ndugu zake pia walifurahia sana, ikafika miezi tisa na muda wa kujifungua, basi siku hiyo tukaongozana na mume wangu hospital moja maarufu, mama mkwe naye alishakuja ili anikande maji niiumwa uchungu kweli masaa yakapita bado mtoto kagoma kutoka naumwa tu, katikati ya kuumwa uchungu presha ikanibana daktari akaniandikia dawa, nilipewa dawa zile huku bado nikiwa na uchungu lakini mtoto hatoki, baada ya kusubiri masaa mengi wakaamua kunitundikia drip ya uchungu ili imsukume mtoto atoke, basi ikachanganya sasa nikajisikia kama nataka kwenda haja, ndipo wakaniambia mtoto anatoka kwahiyo nisukume.
Nikajitahidi kusukuma japo nguvu zilikuwa zinaniisha na kujisikia vibaya sana, jitahidi hapa na pale huku madokta wakinisaidia ndio baadaye mtoto akatoka, wauguzi wakamchukuwa na kumsafisha ili aweze kulia kama inavyokuwa mtoto akitoka lakini mwanangu hakulia, wakajaribu mara kwa mara sikumsikia mwanangu akilia ndipo nilipoambiwa mwanangu amekufa!!!!!!!! sitakaa kusahau niliomba tu waniuwe na mimi maana ninaraha gani huku nikilia kwa uchungu sitakaa nisahau nikazimia, nilipozinduka nikajikuta chumbani wodini sasa ndugu zangu na wamume wangu wote wakiwepo wakinisubiri nizinduke.
Neno la kwanza nilipoamka nilimwambia tu MUNGU kwa nini mimi, nilikuomba ukanipa sasa umemchukuwa kwanini hukutuchukuwa wote, mume wangu na ndugu wote walianza kulia baada ya kuniona na kunisikia nikilia hivyo kwa MUNGU, basi baada ya masaa nikaruhusiwa kurudi nyumbani, mama mkwe na mama wangu wakawa wananikanda na kunipikia kama mzazi hicho ndio kitu kilikuwa kinaniuma sana nakandwa maji, maziwa yananiuma, sina mtoto...
Miezi ikapita, bado namlilia MUNGU anipe mtoto, ikapita mwaka, wa pili, watatu, wanne, maneno yakaanza tena yani binadamu sisi, wa tano nao ukapita mwaka wa sita ulipofika sina mtoto mume wangu sasa akaanza kunibadilikia kwamba kama sizai aniache aowe mwengine ama azae nje nichaguwe moja, kwakweli nilikuwa na wakati mgumu sana mara akaanza kuwa harudi nyumbani, na akirudi basi anarudi saa kumi za usiku, nikimpikia hali chakula na kilichokuwa kinanuma zaidi akawa hataki kabisa kukutana nami kimwili akawa anasema nampotezea nguvu tu wakati mimba sibebi kwahiyo haoni umuhimu!!!!!!!!
Mwaka wa saba nao ukapita, nyumba imewaka moto yani mpaka wazazi wangu na ndugu wakaniambia nirudi tu nyumbani nisije kufa, lakini moyoni niliamini kwamba ninamuomba MUNGU asiyeshindwa basi nyumbani sintorudi nitayavumilia yote, mwaka wa nane ukapita na watisa ukaja ambao ni mwaka jana mwezi wa pili ukapita sikupata siku zangu, na watatu pia nikaamua kwenda hospital kupima doctor akanifanyia ultrasound na kuniambia nina viuvimbe viwili ndio sababu na kunipa dawa za kunywa na nilipomuuliza kama zinasababisha period kutokuja akaniambia kwasababu unamawazo sana ya kupata mtoto ndio maana hupati period lakini ukinywa tu hizo dawa utapata..
Nikafika nyumbani kila nikitaka kunywa zile dawa roho inakataa nasikia mtu kama anaongea na mimi na kuniambia usinywe mwanange, sikuzinywa zile dawa, wiki tatu zikapita siku hiyo nikajisikia kuumwa malaria nikaenda hospital kweli nikakutwa na malaria doctor akanipa dawa lakini pia nilivyofika nyumbani nikasita kunywa bado nilikuwa nasikia ile sauti, basi sikunywa siku hiyo nikaumwa sana tumbo kwa chini yani mpaka nikashindwa kuvumilia kwakuwa ilikuwa usiku nikasubiri niende hospital asubuhi.
Siku hiyo nikaamua kubadilisha hospital nikamwambia doctor nasikia kuumwa sana tumbo kwa chini na akanishauri nipime mkojo angaalie labda nina infection, basi nikafanya kama nilivyoambiwa majibu yalipotoka nikayarudisha kwa doctor, akaniambia infection huna ila unamimba!!!!!! nikamwambia doctor ninamimba nakumbuka nilirudia kama mara tatu kuuliza mpaka doctor akanihoji huitaki????????loohh nikaanza kumuhadithia story yangu, nikajikuta namshukuru MUNGU kwakupiga magoti chumbani kwa doctor nilishindwa kujizuia na baadaye nikaondoka.
Furaha niliyonayo kwanza nikampigia mume wangu na kumwambia akanijibu tu sawa yani kama hakuamini na akakata simu, roho iliniuma lakini nilikuwa sina muda wa kukasirika nikampigia mama yangu simu alifurahi na kumshukuru sana MUNGU akaniambia nisimwambie mtu mwengine yeyote zaidi ya mume wangu watakuja tu kuniona tumbo likikuwa.
Mume wangu hakubadilika tabia yake kwani hakuamini kama nilikuwa kweli nina mimba, kwahiyo miezi yote mitatu nilikuwa tu peke yangu na ninamshukuru MUNGU mimba haikunisumbua hata kidogo na wala sikuchaguwa chakula mume wangu wakati akirudi nyumbani waka hakuwahi kuniangalia kwa karibu kugundua tofauti mpaka mimba ilipofika miezi mitano ndio siki moja alikuwa amekaa sebleni nikawa natoka jikoni naenda kukaa ndipo akagundua ukubwa wa tumbo langu, akaniambia nimfungulie nguo aangalie alipoona kweli nina mimba alinikumbatia na kulia kwa uchungu sana, alilia huku akiwa amenikumbatia mpaka nikahisi ananiumiza basi akaenda kujifungia chumbani na kulia hakutoka mpaka saa moja jioni.
Alipotoka cha kwanza aliniita na kuanza kuniomba masamaha kwa aliyonikosea, na kwakutoniamini kama nilikuwa na mimba, nilichotaka kujuwa ni kwamba kama alizaa nje akaniambia akilikuwa na wanawake nje lakini hakuzaa nje, basi japo roho inaniuma nikamsamehe tu, akaniomba jumapili iliyofwata niende naye kanisani akatubu dhambi zake na kweli akaenda kanisani kwao katoliki na kutubu dhambi zake, kwanzi siku hiyo tulliiishi kama ndio tumeoana jana, kila siku kwetu ilikuwa ya furaha.
Mwezi wangu wa kujifungua ulifika, nikajifungua sema wakati huu doctor alinishauri nipasuliwe basi nikajifungua mtoto wa kike ambaye ni kila kitu kwetu, tukatoa na shukrani kwa MUNGU kanisani tulivyoenda kumbatiza, na mpaka leo mwanangu ndio furaha yangu na ninamshukuru MUNGU na sintoacha kumshukuru milele maana amenitendea maajabu, ndugu, wakwe, mawifi mapaka leo wakiniona walionisimanga huinamisha vichwa chini lakini mimi nimewasamehe wote.
Mama Cathy
HONGERA SANA DADA MUNGU AWAJALIE MUENDELEE NA FURAHA YENU DAIMA ASANTE KWA USHUHUDA MUNGU NI MWEMA HAKIKA.
ReplyDeleteyou are invited tom follow my blog
ReplyDeletehongera dada kwakufanikiwa kupata mtoto uliye msubiri kwa muda mrefu posipo kukuta tamaa hakika unaye yesu siku zote mwanadamu awaye yote hatakiwi kukata tamaa kwa jambo lolote lile mm pia nina hushuhuda ya maisha yangu ambao mungu amenitendea miujiza ambayo siko tayari kutaja miujiza gani lakini nikienda kuwa tayari nitaweka wazi ila nilisha mshukuru Mungu sana na ninaendelea kumshukuru na bado anaendelea kunitendea miujizi ananionyesha magumu ambayo sikuwahi kufikiri kama nitayaweza ktk maisha yangu hakika Mungu ni mwema sana ukimwamini na kumtegemee hakika hatakuacha uwaibike alimradi umwombe kwa bidii pasipo kukata tamaa atakujibu kwa wakati wake aliyopanga mwenyewe Mungu hachelewi na wala hawai ubarikiwe sana uliyeleta ushuhuda huu na uendelee kumwani yeye kwa kila jambo ubarikiwe sana
ReplyDeletePraise be to God Almighty father....hongera sana mama cathy na asante sana kwa kutupa ushuhuda wako. Pole kwa yote yaliyokukuta, kweli Mungu ni mwema, haachagi watu wake waaibike. Ubarikiwe wewe na familia yako.
ReplyDeleteBaada ya kumaliza kusoma hii habari nimetokwa na machozi ya furaha. Hii habari na iwape moyo wote wenye matatizo ya kuzaa. Mungu wetu ni mkubwa
ReplyDeleteKweli Mungu hashindwi na kitu hii story imenipa moyo sana
ReplyDelete