Dada rose,mimi ni fun wako wa muda tu na nimeona shuhuda za watu hapa ambazo zimetutia moyo sana na mimi kisa kilichomtokea mtoto wa mama yangu mkubwa nimeona ni bora nikuandikie upate kuiweka kwenye blog ili na wengine wakapate kujifunza kutokana na hicho.
Dada yangu huyu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu wa mtu kwa muda mrefu tu, kwa mwanzo ilikuwa ni siri lakini baadaye mapenzi yakamzidi mpaka familia yao ikajuwa, baadaye yule mke wa jamaa akafahamu akapeleleza mpaka akamjuwa dada yangu na mpaka namba yake ya simu akaipata, nakumbuka siku akatuadithia yule mke wa mpenzi wake alimpigia na kumwambia kwa uzuri tu kwamba aachane na mumewe, dada yangu akamkatia simu.
Mke wake yule mpenzi wake akaja kumpigia tena siku nyengine, na kumwambia aachane na mume wake kwani anaifanya ndoa yake iyumbe kwa upole tu basi dada yangu akamtukana kwamba kama ungekuwa unamfaa angenifwata mimi na maneno kibao dada yangu akamkatia simu tena, na kila akimkatia simu huwa anampigia mpenzi wake na kumwambia mkewe anamtukana na baadaye yule baba anaporudi nyumbani panakuwa hamna amani nyumbani, anarudi na visa na mwisho tu huishia kugombana alafu akirudi tu kwa huyu dada yangu anaanza kumuhadithia alivyowasha nyumba moto jana yake.
Dada yangu wala hakumuacha yule mume wa mtu na wala hakuyasikia maneno ya yule mkewe, basi mapenzi yakawa motomoto sasa mpaka wazazi wa dada wakajuwa wakamkanya lakini wapi??? yule mke wa mtu akampigia tena mara ya tatu na akamwambia kama umekataa kumuacha mume wangu utajuta na utanitafuta sitakaa kukupigia tena!!!!!
Basi jumamosi moja dada yangu aliamka usiku akaenda chooni ambacho kipo nje ya nyumba alipokuwa anarudi anasema alisikia kama amemwagiwa kitu cha baridi sana na kuanza kuwashwa mwili mzima, yani alikuwa anajikuna sana akaanza kupiga kelele watu wakaamka na kumkuta anajikuna sana na kulia anawashwa sana na kuomba watu wamkune mpaka na brush ya viatu basi wakawa wanamkuna yani hapakulalika mpaka kesho yake kwenda hospital wakampima lakini hawakuona kitu, mama yangu mdogo mmoja akasema ni heri twende wampeleke kwa mganga akapelekwa na kusuguliwa na dwa kama yamajani ndipo kujikuna kukapungua sio kuisha akapewa na dawa za kuendelea kujiosha kila siku, lakini jana ikagundulika kama anamatatizo mara kagoma kuvaa nguo, hataki kuoga, yani anataka kukaa tu ukimlazimisha anakuwa mkali mpaka anataka kukupiga.
Aliendelea hivyo kama wiki ndipo walipoamua kurudi tena kwa mganga, yule mganga alipomuangalia ile hali akamwambia kwamba huyu dada sina dawa ya kumtibia bali ni msamaha tu ndio unaweza kumtibu, msamaha wa nani? yule mganga akawaambia kuwa anatembea na mume wa mtu na alishaonywa lakini hakusikia sasa wamemchezea ndio maana yupo hivi, kwahiyo ili kupona amtafute yule mke amuombe msamaha.
Kwakuwa hawakujuwa namba ya yule mama na shoga ndio kawa kama kachanganyikiwa ndugu mmoja akshauri kwanini wasimpigie yule baba ikabidi wachukuwe simu yake na kumtafuta ilikuwa ngumu maana simu moja inawapenzi sita, alimsave yule baba kama mpenzi kidumu wakampigia na kuanza kumuuliza kama alimfahamu yule dada wakamuhoji kwa uzuri ili asiwe na hofu mpaka walipogundua kweli ndio yule mume wa mtu.
Wakamuhadithia yote yaliyotokea na kumuomba awaunganishie na mkewe aombe msamaha, huwezi amini yule baba alikataa na kusema hataki familia yake iingie matatizoni, kwamba hayupo teyari, atafute tu tiba sehemu nyengine lakini aachane na mkewe, ndugu walijitahidi sana kumbembeleza lakini haikuwezekana yule baba alikataa kabisa.
Mama mkubwa ndipo alipozidi kuchanganyikiwa, ikabidi wampeleke kanisani kwenye maombi, wakamuhadithia mchungaji yote, mchungaji pia aliwaambia Mungu husamehe makosa yetu na hata kama akiombea atubu ni vyema pia akamuombe yule mama msamaha ili aweze kufunguliwa, basi akaombewa na kuombewa na kuombewa na kila mara akawa anaombewa.
Wakati ameanza kuombewa alichobadilika ni kwamba akaanza kuoga na kubadili nguo ila mpaka umkumbushe na kumpeleka mpaka bafuni, lakini akili yake bado haijakaa sawa, ukiongea naye unajibiwa tofauti yani amechanganyikiwa sema tu ni msafi ukimuona kwa mara ya kwanza huwezi kugundua.
Basi mpaka leo ndio yupo hivyo, yule baba hata kwenye simu hapatikani tena, binti mzuri ameishiwa kuwa chizi fresh, yupo tu nyumbani kwao na mama yake, kweli nimeamini mume wa mtu sumu!!!
Agnes
wewe ndio umegundua leo kama mume wa mtu sumu kwani hukusikia ama hukuona kwenye gazeti yule dada aliyetolewa alikuwa analiwa na mume wa mtu siku hiyo katoka naye gesti mara wapo njiani demu anarudishwa kajikuta anafungua mlango wa prado na kukaa njee mara akaanza kuvua nguo zake zote na akajinyea na kuanza kujichezea na uchafu wake sehemu zake za siri? shauri leno na yatawakuta sana
ReplyDeleteJamani SOMO hebu tuwekee na ile story anayoisema anonymous wa kwanza, maana wengi tumeona tu picha na kichwa cha habari, please naomba tubandikie story ya yule dada hapa, maana kweli Bongo kunatisha jamani. Tuwekee mummy ili nasisi tupate somo la kujifunza.
ReplyDeleteSasa afadhali huyu wa kuwashwa yule wa kufua nguo barabarani ndio inatisha. Halafu sasa sijui huyo mume alirudi kwa mkewe au alimuokota hawara yake akaondoka nae? Maana ni hatari jamani. Na wanaume nao wanaoiba wake za watu wafanyiwe sio wanawake tu.
Mpenzi, naitafuta hiyo story halafu nitawaekea humu, tafadhali nipeni tu muda ila nitaituma huku..
DeleteSikuhizi wake za watu wamechachamaa jamani, chezea kuwekwa ndani halafu unajitia mjuaji kuharibu ndoa za watu..utatikiswa kama chupa ya mbilimbi..
Agnes pole sana kwa yaliyomkuta ndugu yako na asante sana kwa story yako. Ni kweli mume wa mtu sumu na shoga alikanyaga pabaya. Mi nawashauri muendelee na maombi, ipo siku Mungu atasikia maombi yenu. Inawabidi muwe wavumilivu katika hili na muwe na imani kwani hakuna lisilowezekana kwa Mungu.
ReplyDeleteEh . Rose tuwekee hiyo stori mwaya...labda vimada watatia akili wakiona wenzao wananyolewa...Mi si mshirikina ila sina huruma na hawa wavunja ndoa za watu...kwanza wengi wao wanaongoza kwa kutumia ndumba.
ReplyDelete