Kuna siku dada mmoja alinitumia mail kuhusu ile mada ya mimba ya miezi saba na sio ya mume wake nadhani mtakuwa maikumbuka ipo hapo chini upande wa kulia kama hujaisoma. watu wengine wakamsema wengine wakamshauri mpaka leo wanaendelea kumshauri na ninajuwa waliomsema yule dada vibaya watakuwa ni wanaume mtanisamehe lakini wanaume na hapo kwasababu katenda mama je ikiwa wewe baba umetenda unategemea nini?
SIKIA HII...
Mwaka 2009 nilipata kusimamia harusi ya rafiki yangu wa karibu sana, aliolewa na mwanaume ambaye walishakuwa kwenye uhusiano kwa miaka minne kwahiyo walikuwa wanajuana vizuri mpaka kuamua kuoana, kabla ya kuoana walishazaa mtoto wa kiume ana miaka mitatu sasa.
Kipindi huyu dada anabeba ujauzito alikuwa anasoma chuo mwaka wa kwanza kwasababu mimba yake ilikuwa inamsumbua sana akaamua kuacha chuo kwanza ili azae akishalea mtoto akitimiza hata mwaka na nusu ndio aende chuo maana alikuwa anasoma mzumbe morogoro kwahiyo hakuweza kwenda na mtoto.
Basi yule dada ameamua kwenda chuo huko mzumbe kaanza nadhani ni mwezi wa tisa mwaka jana, huku mumewe yupo peke yake maana mtoto ilibidi apelekwe kwa bibi sinza maana baba yake asingeweza kumlea yule mtoto, lakini mama mtoto kama shule haijambana weekend nyingi anakuwa anarudi nyumbani na kama mara mbili nimeshakutana naye kwenye hizo weekend anazokuwa anarudi maana namtaniaga wewe endekeza shule uache mume, maana wanaume ukiwepo karibu tu wanakula nje sembuse wewe wa morogoro kaa huko urudi ukute mwenzio ndani jifanye unasoma wamesoma wangapi leo hawapo? lazima utafute muda wa kuja kuwa na mumeo na mtoto wako na kwakweli alinisikiliza japo nilikuwa na mwambia maneno makali lakini kila mara alipoweza alikuwa anarudi ama mumewe anaenda morogoro.
Baaaaasi, kumbe shemeji bwana alikuwa anapiga mechi za nje, kipindi ambacho shostu haji ama yeye hawezi kwenda, sasa kapata kihawara chenyewe kimenogewa na penzi la mzee mara tii mimba, na hawara amegoma kutoa mimba kwa madai kwamba kwao ni mwiko kitoa mimba utakufa ndio anavyomwambia shemeji.
Shemeji sasa kachanganyikiwa hajui la kufanya hawara kakomaa mimba haitoki, jana ananipigia simu na kuniambia hayo na kutaka nimshauri.
Kwanza wewe mwanaume unaendaje mechi za nje bila condom mkeo yule ama kwavile unaona usha...zaidi ya mara mbili ndio unajifanya unamuamini huyo hawara yako pumbafu kama anaukimwi hata kupima mmepima? unajuwa ndoa nyingi sana unakuta ukimwi unaingia kwa namna hii unajuwa mwanamke mpaka atoke nje ya ndoa ni ngumu sana na hata kama akitoka na bila condom huwa lazima wakapime kwanza sio kama nyie mnavamia tu ona sasa mtu anavyoumbuka.
Nikamuuliza sasa mkeo asipokusamehe itakuwaje ananiambia nimbembelezee kwakuwa mimi nilikuwa matron nimueleweshe ilikuwa bahati mbaya kwamba mtoto akizaliwa atamchukuwa aishi naye hamtaki yule hawara anataka tu damu yake, anasema anamuhudumia kwa kila kitu mpaka atakapojifungua.
Sasa basi mwanamke kama mndio wewe imekutokea hivi utafanyaje? na mwanaume utamuelezaje mkeo akuelewe? hebu mshaurini huyu kaka jamani nilimwambia nitapost humu kwa ushauri zaidi.maana mkewe anakaribia kuja nyumbani, ila nilichomshauri mimi asubiri mpaka mkewe akimaliza chuo mwakani ndio amwambie asije akamfanya dada wa watu akafeli mitihani na kujiharibia maisha kisa chovyachovya ya mumewe.
kwanza dada rose umemshauri vizuri kumwambia asimwambie kwanza mkeo kuhusu hii habari maana itamchanganya na kushindwa masomo yake umefanya vizuri ni wazo zuri sasa nakuja ktk kumshauri huyo kaka kama ulivyomshauri na mimi nihivyo hivyo aimwambie kwa sasa asubiri amalize masomoyake ndipo amwambie atakapo mweleza amwele za mbele ya washenga wake na wazazi pia wa pande zote mbili na akiri hatarudia tena na akubali kupima kama hajapata maambukizi kabla hajajamiana na mkeo nafikiri kwakufa hivi mkeo ataweza kumsamehe na ikibidi na huyo aliyepewa mimba awepo pia aelewe kila kitu kila kitu ajaribu kuweka wazi posipo kuficha wala kuogopa maana siku zote ukweli utakuweka huru ni hayo tu na huyo kaka aache tamaa maana hata kama hamwweshimu mkewe na magonjwa je? aache mchezo huo mara moja ni hato tu asante sana dada rose kwakutuwekea kisa hiki
ReplyDeleteHivi kwanini kila siku wanaume ndio wanapenda wao wasamehewe?
ReplyDeleteMimi ningemshauri huyo dada na yeye abebe mimba ya mwanaume mwingine ili wawe even, maana hapo kila mmoja wao atakuwa na mtoto wa nje, basi watalea watoto wao kwa raha mustarehe.
Mimi nikikuta mume wangu amezaa nje vyovyote iwavyo namtwanga talaka tu, hakuna msamaha hapo wala nini. Tena nakutumia salaam kabisa ukae ujue I will strip you of everything kisha ninakuacha mweupee kama nilivyokukuta, sasa uoe hicho kimada chako mlee mtoto wenu.
Subira Feruz