Thursday, May 31, 2012

Usiombe ukutane na Magumegume Utajutaje....

Kweli nimeamini magumegume yapo jamani tena mijicho imewatoka wasione umefanikiwa wao roho zinataka kuwachomoka, hawalali usiku na mchana wanakuombea mabaya, wakikuona ndio unamume anakupenda basi utawaona wanavyojichekesha shemeji sijui nini basi tu ilimradi wakuharibie shemeji akimchekea kesho anatuma msg nimekumiss nipe basi ofa ya beer inahusu!!!!! hukumuweza kabla hajaoa akishaoa utamuwezea wapi kutwa kumfwata nyuma kama kitoto cha paka aibu mwanamke.

SIKIA HII..

Kuna dada mmoja ameolewa lakini hakuwa na mtoto kwani walipanga na mumewe watafute kwanza hela mambo yakikaa sawa ndio wazae, basi wakawa wamepanga nyumba moja hivi mabibo, wenyewe walikuwa wanapendana basi kutwa wakiwa pamoja wanagandana kama smaku miye nawajuwa kwasababu jirani zangu.

Kwenye hiyo nyumba waliyokuwa wamepanga ni nyumba inatazamana na nyumba ya mama mwenye nyumba yani zote zipo kwenye uzio mmoja, huyu dada yeye sio mtu mzima kama miaka 25 na kwenye nyumba ya mama mwenye nyumba yao yule mama alikuwa na watoto lakini kati ya watoto wake kunammoja amelingana naye umri ambao walitokea kuwa marafiki ajabu, walipika na kupakuwa, walishona nguo sare, siri ya huyu ikawa ya yule, kila unapomuona huyu na yule alikuwepo kila mtu akawa anajuwa urafiki wao na mumewe wala hakuwa na tabu nao.

Miezi ikaenda cha ajabu yule mtoto wa mwenye nyumba akaanza sasa kumzoea na mume wa shoga yake, story kila kaka anaporudi kazini, mara wote wapelekwe bar wakalewe mara wanaenda wote mziki, mpaka majirani wakaanza kushangaa, kumbe bwana shosti kampenda shemeji akajitongozesha shemeji naye sijui vupi kaingia mkingi mapenzi sasa yakaanza, yakawa motomoto mara nyingi wanaonekana pamoja hata mtaani mkewe akiambiwa anasema tu mtu na shemeji yake kwani kuna tatizo gani wakiongozona?

Watu wakawa mpaka wanawaona gesti ya nyuma ya mtaa wanapokaa yani watu wakawa wanakasirika lakini wakimwambia mkewe wala habari hana, wakachoka na kuamua kuwaacha basi ikafika yule mumewe akamnunulia simu hawara yake, na yule hawara kwasababu alishachanganyikiwa na mume wamtu na ndiye mwanaume aliyemtoa bikra akawa haambiwi asikii mpaka usiku wa manane anapiga simu na kutuma msgs basi tu amuharibie mwenziye asikae kwa amani.

Hasubui ikifika yule mke wa mtu anamfwata shoga yake na kumuhadithia kwamba kuna mtu anapiga sana simu ya mume wangu usiku nadhani mume wangu atakuwa na hawara ngoja akirudi nitafute ile namba tumtukane (bila kujuwa hawara mwenyewe ndiyo huyo shoga yake anayemuhadithia) basi mke akapata namba ya simu akamletea shoga yake kuipiga haipatikani shoga akachukuwa simu na kuandika msgs ya matusi kumtukana hawara anayemsumbua shoga yake (anajiandikia mwenyewe)!!!!!

Huyu hawara alikuwa mwanfunzi wa chuo, chuo akawa haendi tena kutwa anashinda nyumbanina kipindi hicho wazazi wake wakawa wameshajuwa ukweli kwa kuambiwa, walivyombana akakiri ukweli akasema nampenda yule kaka na hamna mtu yeyote atakayeweza kuniachanisha naye hata kama ni mkewe, wazazi walichanganyikiwa wakaona cha kufanya ni kwenda kushtaki polisi ili achukuliwe hatua yule kaka.

Siku hiyo mke mtu yupo nyumbani anapika anasikia mlango unagongwa polisi ndani, wanamtafuta mumeo akauliza kwa nini ndio kumpasulia jipu akadondoka na kuzimia hapohapo, alipoamka akakataa kuamini akalia sana na kumtafuta yule shoga yake kumuuliza akakiri na kumwambia na hapa ni mjamzito wa miezi miwili yule mke wa mtu akamuwasha bonge la kofi na kumtukana sana, alichofanya baada ya hapo nikuchukuwa vitu vyake na kuondoka maana hakutaka hata kumsubiri mumewe arudi maana alikuwa anahisi atamuua.

Shoga yake aliyemuamini na kufanya naye kila kitu kumbe ndiye mbaya wake (kweli fadhila mfadhili mbuzi utamla mchuzi binadamu anamaudhi) nguo na kila kitu walichokuwa wanavyosare akavichoma moto hakutaka kabisa kubaki na ukumbusho wowote wa yule dada.

Yule kaka alikamatwa na kupelekwa polisi lakini baadaye akasema angemuoa yule mtoto wa mwenye nyumba na kweli akamuoa akazaliwa mtoto wa kike, lakini kweli ya MUNGU mengi yani tokea yule kaka alivyooa kwanza kazi akafukuzwa, hakawa hana kazi anashinda nyumbani tu (ukikutana naye barabarani anakuomba hata 5000 ya kulisha familia nyumbani) kwavile nyumba ni kwa wakwe hakudaiwa kodi, akawa anatapatapa akitafuta kazi lakini hakufanikiwa mtoto wao sasa anamiezi mitatu yule mkewe wa pili akachoka mateso ya kuishi bila hela maana sasa walikuwa wanawategemea wazazi akamfukuza yule kaka tena kwa aibu mpaka majirani wakasikitika.

Kijana yupo anatangatanga mtaani sasa, amekuwa kibaka hatari yani watu wa mabibo wamempania siku wakimkamata..........

Mkewe anaishi bado kwao anafanya kazi na kwa sasa anasema hataki shoga, urafiki na wanawake ni salamu tu mengine kafie mbele......





4 comments:

  1. asante sana dada rose kutuletea hii habari loh! ni kama movie vile kweli sisi wanawake hatupendani kabisa unawezaje kutembea na bwana wa rafiki yako? na mwenzie alikuwa amemwamini sana mahali roho yangu imeniuma ni pale alipomwambia kuhusu cm anayopigiwa mumewe iliwamtukane huyu mwizi wa mumewe kumbe jizi ni yeye rafikie kweli rafiki ni mia fisi hili ni somo tosha kwa watu waliolewa na amboa hawajaolewa kumwanini shoga na kumshirikisha na mumewe asante sana dada rose kwa kutuwekea kisa hichi endelea kutuletea mambo mimi ni fan wako mkubwa kila siku siachi kukutembelea nione umeweka kitu unajitahidi sana kwa kutuletea visa na mikasa ubarikiwe sana

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli usisikie mume anauma wanawake wenzangu hasa ukisalitiwa na mtu ambaye anakujua in and out unatamani umfinyange ummalize kabisa. Wanawake tupendane, tuheshimu ndoa za wenzeetu iweje leo wewe uliye msiri wangu ninayekuamini unanigeuka? Na hao wenzi wetu wa jinsia tofauti ni wepesi sana kushawishika sijui wameumbwaje hawajali ni maumivu gani mwanamke utayapata? wanawaza starehe tu kwa kweli ni viumbe wa ajabu sana. Mungu tusaidie.

    ReplyDelete
  3. kwa kweli nimejifunza kitu hapa, mimi ndio maana sina shoga mwenzenu nayajua haya. nasalimia na wanawake wote lakini sio mengine hapana. ona sasa familia ilivyoharibka, halafu watu hawajui mke anakupa baraka zote ndio maana unafanikiwa akichukia yeye hakuna kitu

    ReplyDelete
  4. Mhhh jamani, hii ni kama movie, am totally speechless

    ReplyDelete