Wednesday, May 2, 2012

Chonde Chonde mtoto wa Mwanaume Mwenzio Huyo...

Jamani hizi ndoa sasa huko tunapoelekea sijui, kwanza ningefurahi kama wengi wanaosoma humu ni wanandoa, ama anatarajia kuingia kwenye ndoa lakini sio kwa wewe ambaye bado hupohupo sana maana kuna mada nyengine zinaitaji moyo humu kusoma na kuzielewa.

Leo kuna baba wa aina fulani humu nataka niongee nao, na wewe mwanamke wa nje unayekuwa na mume wa watu kwa upashkuna wako na hashuo zako unajifanya kushadadia na kutaka kumchukuwa huyo mume wa watu awe wako, ebo inahusu nini kwani alikuwambia anavyokuja kwako mkewe hampendi????? ama unadhani yanayomtoa nje wewe unaweza kuyatimiza??? Jamani kweli kuna ndoa nyengine zinavituko ambavyo havivumiliki hata baada ya mmoja kutaka suluhisho na mwenzake ajirekebishe na kushindikana hapa ndipo watu wanatafuta pumziko nje kwani nani anataka kufa kwa ugonjwa wa moyo....

Jana nimekutana na rafiki yangu tukakaa na kuongelea maswala ya ndoa zetu na maisha yetu kwa ujumla na watu tuliokuwa nao yeye aliolewa mwaka 2006 ndoa ya fahari jamani siunajuwa labda kama mmelazimishwa lakini ndoa za kutaka wenyewe ni tamu tena mwanzo mapenzi motomoto..basi wamekaa pamoja ikapita miaka mitatu yule dada hakubarikiwa kupata mtoto akazunguka kote kwa madaktari hadi kwa waganga bila mafanikio, bila huruma yule mumewe akachoka kila siku akawa anampa maneno ya kashfa akirudi nyumbani yani kero hamna amani asubuhi ikifika yule dada akimuomba mumewe hela ya matumizi maana yeye alikuwa tu mama wa nyumbani basi yule baba alimpa maneno ya kumnyima raha akisema yani mimi natoa hela za chakula humu ndani hamna hata siku narudi nakukuta unalamba kipande cha ndimu, ama kuniambia unajisikia kichefuchefu kwani kwenu hawajakufunda mikao ya kupata mimba!!!!!!!

Wakati wote huo alikuwa tu anavumilia na kusali tu MUNGU ampe mtoto japo mmoja, japo wakati wote alikuwa akipimwa hakukutwa na tatizo lolote linaloweza mfanya asibebe mimba, madaktari wakamshauri apime na mumewe lakini kila akimwambia mumewe hataki tena wakiongelea tu hivyo ni ugomvi mpaka yule baba harudi nyumbani siku hiyo baasi akaachaga kuongelea hilo swala, akabaki kuwa mtumwa wa ndoa maana hamana tena hamani wala ndoa mnaishi tu kama kaka na dada.

Ikafika 2010 yule kaka siku moja karudi nyumbani na kubeba nguo zake zote na kumwambia amepata mwanamke ambaye amembebea mimba, kwahiyo kumbe alikuwa na mwanamke wa nje kipindi hicho basi akaondoka pale kwa maneno na vurugu kwakuwa nyumba walikuwa wamepanga akamwambia kodi ikiisha rudi kwenu, na kweli yule dada kesho yake akawataarifu kwao kwa huzuni wakampokea yule dada akaanza kuishi tena maisha ya peke yake kwao.

Hapa kunakitu wanandoa mnaotoka nje ya ndoa msichokielewa ama mnaelewa lakini hamtaki kuwaelewesha manokuwa nao huko nje, ni kwamba wewe umeoa unaenda kuwa na mwanamke wa nje ambaye hajaolewa unategemea utakuwa peke yako katika maisha yake??? kwa taarifa yako wengi huwa ni namba tatu ama nne yani kuna yule anayempenda na kuomba amuoe, kuna wewe unayekuwa kwake kwa kumuhudumia tu maana hutaweza muoa, halafu kuna na yule anayehudumia wewe ukiwa hupatikani..hata mimi nilipita hukohuko kabla sijaolewa naelewa how we play those games.

Kama unamatatizo ya ndoa yako na unataka kutoka nje tafuta mwenzako mwenye matatizo na ndoa yake halafu mliwazaze wenyewe tena mapenzi hayo ni matamu kwasababu kila mtu anapata anachokosa akirudi nyumbani, na aina hii huwezi kuta mtu anawatu watatu kwani nje ana wewe ndani anaaliyemuoa hiyo nafasi ya kupata mwengine wa tatu ataitoa wapi wakati watoto pia wanahitaji muda wa mzazi???? tafakari vizuri

Back to My story:

Basi yule kaka baada ya kuelezwa na mwanamke wake wa nje anamimba ndio kamchukuwa akahamia naye sehemu nyengine na baadaye kumuoa ndoa ya bomani, miezi tisa baadaye mtoto akazaliwa wa kike wakawa wenye furaha sana, mtoto akakuwa sasa anamiaka miwili lakini cha kushangaza yule mtoto hafanani na baba yake wala ndugu za baba yake anafanana na mama yake pua na macho lakini ni mweusi wakati hawa wote ni weupe, shaka ikaanza kumuingia yule baba lakini akiangalia alipotoka na alipo sasa angeanza wapi kurudi nyuma? na ataanzaje kuongelea swala la mtoto na huyu aliye naye kwani italeta mtafaruku wa hali ya juu.


Kwa akili za yule kaka akaanza tena kumtafuta yule mke wake aliyemuacha na kwavile alikuwa anapajuwa kwao akatuma watu kwenda kumuomba msamaha na kutaka kukutana naye japo amuombe msamaha ana kwa ana, yule dada kwa vile alimpenda mumewe akakubali kwenda akaombwa msamaha na kukubali ila kwa nia moja tu waende wote wakapime uzazi ndio warudiane ama hata uhusiano tu wakawaida aliouomba huyo kaka hilo ndio jibu ambalo angelipata yule dada baada ya kuteseka sana kwenye ndoa kisa hana mtoto na hata kuachwa.


Basi bwana kwavile kaka alitaka kurudi akakubali ndipo walipofanya vipimo wakagundua yule kaka anamatatizo ya uzazi aliniambia kama mbegu za mumewe zinashindwa hazina kasi sijui ya kufika kutunga mimba kwahiyo zinaishia juu na ndio maana mimba haitungi (Madaktari mtakuwa mnajuwa hilo ni tatizo gani) kwahiyo inabidi wakiwa kitandani mama aakikishe ameweka mto chini ya mapaja ili mbegu zinapoingia zisitoke kwani mapaja yatakuwa juu.


Kwa aibu kubwa yule baba alizimia, alipoamka alilia kwa uchungu kwanza kumuacha mkewe, pili kulea mtoto siyo wake kwanzia mimba mpaka miaka miwili kwahiyo baada ya hapo mapenzi yakarudi upya ila hawakuweza kuishi wote kwani kule napo alioa kwahiyo kimbebe alichonacho sasa wanalala hoteli na mkewe jioni kila mtu anarudi kwake yule mama amekataa kuvunja ndoa anasema kitanda hakizai haramu.


Akaniambia yani kinachomuuma mumewe mwenyewe analala naye gesti halafu anarudi kwa yule mwanamke lazima atakuwa kalogwa maana baada ya kugundua sio mtoto wake kisa ndoa anashindwa kumuacha mbona mimi aliacha ndoa kunakipindi yule baba akamwambia mkewe atafute nyumba waishi wote mara gafla anamwambia hawezi kuicha ile familia yani vurugu juu ya vurugu.


Nilichomwambia mimi as long as wanaendelea basi atulie wajaribu kupata mtoto wamlee hivyohivyo kama yule analoga wewe piga goti sali tuone mwisho wake utakuwa nini, kwasababu asikwambie mtu bwana mapenzi ya dawa yana pumbaza lakini yana mwisho na mwosho wake huwa ni mbaya balaa na kwanini uloge kama wako wako tu mpe muda ajitambue, hilo ni wazo langu tu sijui lako wewe..

1 comments:

  1. ukisikia utumwa wa ndoa ndio huo.kwa nini umng'ang'anie mwanamme kiasi hicho?kisa alikuwa mume wako.jee wewe hutaki kuwa na furaha katika maisha yako?na unajua kabisa,akitoka kwako,anaenda kulala kwa mwanamke mwengine.wewe unabaki muombe mungu tu.tusipende kumsingizia mungu kwa madhaifu yetu.kwani kuna ubaya gani,kuendelea na maisha yako bila huyo mume.jee akifa mtazikwa wote?.kazi yako ndio mume wako.

    ReplyDelete