Mtanisamehe nyie mnaoenda kuwatembelea hawa waganga kwa namna moja ama nyengine, ni kweli kuna wengine huwaamini sana hawa kwamba ndio kila kitu kwao yani wanaamini chochote wanachokitaka wakienda kwa waganga basi lazima wapate na siku hizi waganga wanakula sana hela kwa kuendekezwa na wanawake kwa fikra zao mbovu kwamba kwasababu wanataka penzi la fulani basi ataenda kumpulizia kwa mgana..As for me mganga no way tukipendana is pure love from my heart and soul lakini uganga never and never will tena MUNGU aniepushie mbali.
Kwanini leo naongelea haya yani kuna jambo limenikera yani mpaka nasikia kuumwa uchungu, kwa wamama nadhani nikisema haya utanielewa ni uchungu gani unaopitia na kwa wababa kama ulimuona mkeo anaumwa uchungu anapotaka kujifungua basi utaelewa jinsi roho inavyoniuma nikiongelea hili swala.
Kuna dada ameolewa pamoja na mumewe wanawatoto watatu wa ndoa ila huyu baba anawatoto wawili wa nje ambao mkewe hakuwajuwa mpaka juzi tu hapa.
Huyu baba alipata uhamisho wa kazi kwenda Arusha na kwasababu ilikuwa haraka aliacha familia yake dar kwa madai kwamba atawachukuwa mambo yatakapokuwa sawa kule, basi kweli yule mama akabaki huku akitunza watoto wake kipindi cha mwanzo kweli yule baba alihudumia vizuri sana familia yake miezi sita ikapita kila mkewe akimwambia vipi utatuchukuwa lini baba anasema bado kidogo mama kweli hakuchoka kumsubiria mumewe mara mwaka ukapita.
Nampaka imefikia huo mwaka yule baba alisharudi kusalimia nyumbani mara mbili akimwambia bado mkewe mambo yakijipa basi nitawachukuwa endelea tu kuvumilia yule baba akarudi tena Arusha, lakini kwa wakati huu yule baba alikuwa mzito sana kutuma matumizi ya familia yake na baadae akawa hatumi kabisa kila mkewe akimwambia anamjibu tu sina kwani wewe siunakazi zamu yako sasa support familia wewe mimi sina kabisa, yamani huyu mama anawatoto watatu, alipe kodi ya nyumba, matumizi ya nyumbani, ada za watoto kweli ataweza peke yake?
Yule mama baada ya kuona kweli mumewe kakomaa basi akaacha kumpigia simu akawa tu kidogo anachokipata ndio anaendesha familia kwavile hakumudu kuwaendeleza watoto shule hizi za academy akawapeleka kayumba, nyumba aliyokuwa amelipiwa kodi na mumewe akaama na kuamia kwenye chumba kimoja yani maisha yao yakabadilika na kuwa ya tabu sana lakini yule mama wala hakukata tamaa aliishi na watoto wake hivyohivyo na ndani ya moyo wake alikuwa na kinyongo na mumewe ambacho alisema ipo siku atamlipizia kwa aliyomtendea.
Kipindi hicho yule mumewe hata mawasiliano alikata kabisa kwa familia yake, yule mama naye hakujiangaisha kumtafuta mpaka mwaka mwengine ukaisha sasa kwavile hakujuwa kule arusha mumewe anakaa wapi hakuwa hata na muda wa kumfwatilia lakini mwenyewe japo alijuwa moyoni siku yake itafika ya kumlipiza kisasi mumewe.
Kumbe bwana yule baba kule arusha alishapata mwanamke, ambaye aliuteka na kuuchanganya sana moyo wake hadi akaona mkewe si kitu, kwahiyo akahamia kwa yule mwanamke na mpaka yule dada kubeba mimba na kujifungua watoto mapacha, kwahiyo sasa wakawa wanaishi kama mume na mke. Na kwa hela anayopata jeuri ya kutunza familia mbili hana kwahiyo akaamua atunze ili aliyekuwa nayo kwa muda huo.
Mwaka wa tatu ukaja mume hajarudi nyumbani wala habari hana, yule mama sasa akapata wazo la kwenda kazini kwa yule baba na kumueleza boss wake kila kitu labda atamsaidia kujuwa alipo mumewe, kwakweli anasema alipofika pale boss wa mumewe alisikia huruma sana baada ya kusikia hiyo story nzima hakusita kumuelekeza sehemu ya nyumba za office huko arusha na akampa hela ili aende huko na nyengine za kutunza familia yake, yule mama alifurahi sana.
Familia ya mwanamke ilikuwa haina cha kumshauri bali kuwa naye tu karibu katika maamuzi atakayoamua kuchukuwa basi akaacha watoto kwa mama yake akafunga safari kwenda arusha kama alivyoelekezwa na boss akafika kwenye hizo nyumba lakini alipewa taarifa mbona huyo mumeo hakai huku siku hizi alishahama halafu wakamshangaa wewe ndio mkewe mbona hapa tunamtambua mkewe mwengine na amezaa watoto wawili mapacha? yani yule mama anasema alihisi kuumwa tumbo la uchungu? mapacha? mke? sasa akawa amepata majibu sahihi kwanini mumewe alimpotezea muda wote huo.
Alichoshauriwa pale labda uende kazini kwake ndipo utakapokutana naye, na kweli next morning yule mama alifanya vile akafika pale asubuhi na kumuulizia akaonyeshwa yupo ofisi gani na kumfwata yani alipomuona mumewe tu yani alilia kwa nguvu tena kwa uchungu ndio mumewe kwa aibu akamchukuwa yule mama na kwenda naye nje kwemye gari yake yule mama akaendela kulia huku akimsema sana mumewe akiongelea kuhusu yeye kuoa na kuwa na watoto, baada ya kunyamaza kulia ili apewe majibu mumewe akamuambia ni kweli sikuweza kustahimili shida zangu za mwili nikapata mwanamke sikutaka kudumu naye lakini sikuachana naye mpaka akazaa niakjikuta sina la kufanya bali kuwa naye hajui kuhu nyie na wala hajui kama nilishaoa kwahiyo naomba uniache nimeanza maisha mapya nishamehe nilikupotezea muda lakini siwezi kuwa na nyie tena.
Yule mama akazidi kulia na kumwambia yani nilijuwa umekuja kutafuta maisha ili tuishi vizuri kumbe umekuja kuoa na kututelekeza, sawa nitaondoka lakini dawa yako ipo hayo macho yanayokufanya uangalie juu na kuona wanawake tu yatakuponza na yatafunga hutaona tena utajuta, na huo uume wako unaokufanya uingie kila uke unaouona utakufanya ukose raha na amani na kujuta kuzaliwa mwanaume mama akafungua mlango na kuondoka kurudo hotelini kwa uchungu sana akajikaza na kurudi zake siku ya pili kituo cha kwanza TANGA..
HAPA NDIO BALAA LILIPOANZA
Hakumjuwa mtu yoyote Tanga lakini kwa kuulizia mganga gani anasifika aliweza kufikishwa na kwenda kumuona mganga akamuuelezea story yote mganga akamuuliza unataka nifanyaje bila huruma, mama akasema nataka uzibe macho ya mume wangu asione na uume wake usisimame daima, basi mganga akafanya kama alivyoambiwa na kweli hicho ndio kilichotokea mpaka leo ninavyoandika hapa yule baba haoni kawa kipofu na kusimamisha kwisha, mke aliyekuwa naye hakuweza kumtunza mtu akawa kama mzigo akabeba mapacha wake na kuondoka bila kumuaga na kumuacha kwenye nyumba peke yake.
Baada ya kutofika kazini siku tatu wakaamua kumfwatilia na kumkuta nyumbani anakaribia kukata roho maana alikuwa hajala wa kunywa maji yani alikuwa kwenye hali mbaya ikabidi wamkimbize hospital kwa matibabi siku ya pili walipoenda kumuangalia ndipo akawahadithia hii story.
Kwasababu hakuweza kufanya kazi tena ilibidi arudishwe dar, ndugu zake wakampokea wakaa naye lakini baada ya miezi mitatu kupita ndugu za huyo baba wakamtaka akamuombe yule mkewe msamaha yule mama alimsamehe kwasababu mpaka wazazi wa yule kaka walimpigia magoti na kulia, hakuwa na lakufanya zaidi tu ya kumsamehe japo kwa shingo upande wakamuomba aende kwa yule mganga amfungue mumewe kesho yake akafunga safari kwenda Tanga kwa yule mganga kwasababu alikuwa anapajuwa akaenda tu moja kwa moja hadi nyumbani kwa mganga na kumuulizia mganga akaelekezwa kufika pale hakumkuta yule mganga aliyeenda kwakwe mwanzo bali alimkuta mwanaye alipomuulizia baba yake aliambiwa ameshafariki!!!!!!!!!
Amefariki!!!!! sasa nitafanyaje akajikuta anaongea na yule mtoto wa mganga, kwani kuna nini mama akauliza, basi yule mama akamuelezea yule mganga kila kitu, akamwambia yani hilo swala ni gumu maswala mazito kama hayo bado sijafikia kuyatatua hayo aliyaweza mzee tu mama kwahiyo hakuna la kufanya labda uzunguke kwa waganga wengine kama itawezekana lakini sidhani, yule mama kusikia hivyo ikabidi akawaeleze ndugu wa mumewe ikabidi sasa wahahe kwa waganga wa kila aina huko na kule bila mafanikio mpaka sumbawanga, walipofika huko wakakutana na mganga mmoja mkongwe yeye akasema anauwezo tu wakuusimamisha uume wake lakini sio kutoa upofu alio nao.
Yule baba akamwambia mganga na ndugu zake kama sitaweza kuona basi hamna haja hata ya kuuponyesha uume wangu nitaishi hivi tu, basi wakaondoka na mpaka leo ni mwaka wa tatu yule baba haoni wala hasimamishi kisa mke wake.
Hili ni funzo aisee
ReplyDeleteINASIKITISHA SN WANAUME MSIJIFANYE VDUME KUACHA FAMILIA ZENE, MKIENDELEA YATAWAKUTA MENGI, POLE BABA NAWE MAMA KAMA UMEACHWA UNGEPATA MWANAUME MWNGNE HAIKUWA NA HAJA YA KUMLOGA KM MTU KAKUCHOKA HAMNA JINSI
ReplyDeleteKuna mganga mmoja tu hapa duniani, toka nazaliwa namsikia na hata kabla sijazaliwa alijua kuwa ntakuwepo...yupo siku zote...wapendwa nawaomba tu msiache kumuomba Mungu wenu
ReplyDelete