Sunday, December 11, 2011

habari zenu, natumaini wote ni wazima leo naleta mada hii kwa niaba ya baba yangu naombeni ushauri wenu ili niweze kumshauri yeye, sisi ni waislamu na tunajuwa dini yetu inaruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja, sasa baba yangu na mama yangu walitengana na kuachana kwa talaka mwaka juzi, mwaka jana baba yangu mkubwa akaja nyumbani na kumshauri baba kuliko kula haramu ni afadhali aoe mke mwengine, na tena akamshauri kuoa mke mdogo ambaye amelingana na mdogo wangu wa tatu kwakweli sisi hatukupenda afadhali angeoa mtu mzima kuliko kwenda kuoa huyo mtoto lakini kwakuwa hatukuwa na lakufanya tukanyamaza kimya.


baba yangu kujijini wakawa wamemuandalia mke huyo mtoto, akaenda akaoa tena kwavile alikuwa bado mbichi akamlipia mahari kubwa sana, wameishi sasa ni mwezi wa nane yule mwanamke anataka kuachika anasema hataki kuolewa na mtu mzima, halafu tunasikia alikuwa mjamzito akaenda kuitoa mimba ili aachane naye bila mtoto wake. baba yangu anashamba ambalo ndio anaenda kushinda huko hata wiki kwahiyo anapoondoka huyu mwanamke ndipo anapata nafasi ya kujivinjari maana wanakijiji wanadai hata ile mimba aliyoitoa ilikuwa siyo ya baba yangu.


sasa ndugu wa baba yangu wanaenda kudai mahari yao kwa wazazi wa yule binti, yani ni aibu jamani sasa ndugu wa baba yangu wanamshauri baba yangu kurudiana na kwenda kumuomba msamaha mama yangu na mama ameshawaambia kwamba hataki yani baba yangu amekuwa na huzuni na kukonda mpaka anatia huruma. afanye nini?


Warda

0 comments:

Post a Comment