Wednesday, October 5, 2011

HUYU NAE VIPI JAMA..




kwa utamaduni wetu wa kiafrica mwanaume anapoamua kuoa inamaana ameshajipanga kimaisha maana yeye ndiye kichwa cha familia kuibeba familia ambayo MUNGU anaenda kumpatia, kwahiyo yeye anajukumu la kuitunza na kuhudumia familia yake kwa lolote.


lakini kwasababu ya maisha siku hizi kuwa magumu japo ni jukumu la mwanaume kuhudumia familia yake sisi kama kina mama tumeona ni vyema kusaidia katika majukumu hayo sio tu inaleta kuheshimiana zaidi bali tunasaidiana ili tuweze kuendelea zaidi.


sasa basi inakuwaje pale wewe na mke wako mmepangiana majukumu ya kifedha halafu mama yeye akawa kila jukumu lake analifwatilia na kulipia kwa uangalifu halafu wewe mwanaume majukumu yako hutaki kufanya kila siku unasema hela huna unasubiri mpaka MUNGU atakapokufungulia milango (wakati kila mtu anajuwa ni uongo hela unazo sema ya dunia yanakuponza, na kupenda starehe kuliko uwezo uliokuwa nao na ukirudi nyumbani huna hata thumni) asubuhi unaenda tena kazini unarudi kwako kila siku usiku wa manane, umelewa lakini kila unapotakiwa kutoa hela ya majukumu uliopangiwa unasema huna hela???? na siku ukiamua kutoa unatoa umekasirika unakunja mdomo.. duh (ndoa jamani sio mchezo wa kuigiza hukufikiria haya yote kabla ya kutaka kuoa????)


mkeo ukimwachia hela ukaambiwa haijatosha kwasababu matumizi mengi, mwanaume anakasirika na kwenda kumwaga mkeo mbele ya marafiki zako kwamba hajui kutumia hela vizuri na kuanza kupeleleza majumba ya watu na matumizi yao..(utadhani mahitaji ya kila nyumba yanalingana) sasa mwanaume ameamua atakuwa ananunua yeye mahitaji yote ya kupia vitunguu, nyanya, carrots n.k maana anadhani mkewe anamuibia.


mambo kama haya jamani ni aibu, mkeo anaposaidia na yeye nyumbani usimvunje moyo kisa umeona anakazi unataka kila kitu alipie yeye, na ni muhimu kila mwanaume akatambua jukumu lake katika nyumba yake sasa ukiwa unatakiwa kutoa fedha ukaanza kununa mpaka watu unaoishi nao wanakushangaa hii si aibu..


1 comment:

  1. Hongera dada Rosemary kwa kuboresha blog yako na kuweka posts mpya!

    ReplyDelete