Tuesday, September 13, 2011

UTU HUNA HATA MOYO WA HURUMA PIA HUNA?????

Rosemary

kweli nimeamini nyie wanawake hamna huruma hata kidogo kuna mama mmoja hapa mtaani kwetu huyu mama ni mtu mzima mwenye heshima zake, na pia ni shoga mkubwa sana wa mke wangu hapa katikati yule mama alikuwa mjamzito na cha kushangaza ile mimba eti ilikuwa inampenda sana mke wangu kutwa yule mama utamkuta nyumbani kwangu mpaka jioni mumewe anaporudi ndio huenda kwake sikuona kuwa ni jambo baya mwanzoni kwani mwaname anapokuambia mimba imempenda mtu fulani mimi kama mwanaume sielewi naona sawa tu kwani sijawahi kubeba mimba kwahiyo sijui kitu.

na kipindi hichohicho mke wangu naye alikuwa mjamzito walipishana kama mwezi hivi maana baada ya mke wangu kujifungua tulikaa wiki tatu tukasikia na huyu dada amejifungua mtoto wa kiume na mke wangu yeye alijifungua mtoto wa kike.

kabla hajenda clinic sikumoja akaumwa kweli na kulazwa katika hospital ndogo moja hivi karibu na kwetu, ndipo alipopima na kugundulika na huu ugonjwa wa kisasa, ikawa siri yake hakuna aliyejuwa zaidi yake na mumewe, baada ya ile mimba kutimiza mitano yule mama akaanza kwenda clinic yani nyie wanawake wengine kweli ni mashetani yule mama hospitali akaandikisha jina la mke wangu kama ndio lake alipoulizwa anapoishi akaandikisha nyumbani kwangu.

sasa baada ya miezi saba au nane nadhani wamama wajawazito huwa wanapewa dawa ili wasimuambukize mtoto, na huyu mama kweli akawa anakunywa hizo dawa kama alivyoagizwa kumbukeni mpaka wakati huo mimi na mke wangu hatuelewi chochote alichokifanya, sasa baada ya kujifungu huwa hawa waudumu wa watu wenye huu ugonjwa huwatembelea wagonjwa majumbani na kuwapa misaada na dawa pamoja na kujua hali zao na huku kwetu wameshatembelea nyumba kama tano yani mpaka mtoto wa latatu ukimuuliza atakwambia hao ni nani kwajinsi wanavyojulikana.

huku ninapoishi huwa najulikana sana kwani nimekaa hapa mwaka wa kumi na tano sasa kwenye hii nyumba niliyopewa ya urithi na baba yangu kwahiyo ni mtu ninayejulikana sana huku kwetu, sasa hawa waudumu wakaja wiki iliyopita wakawa wanapaulizia nyumbani kwangu kwamba mke wangu kajifungua juzi juzi kwa kweli mtaani watu walishangaa sana kujua mke wangu ni muathirika na kumalizia kwamba hata mimi nitakuwa nimeathirika, wakawaelekeza kwangu na kufika, na kukutana na mke wangu ndipo waliposhangaa kumuona mbona siye tunayemtafuta??? wakamuadithia hiyo story ndipo alipotajiwa jina la hospitali yao akagundua ni yule shoga yake aliyetumia jina lake kwani alimuarifu huwa anaenda huko clinic.

tukawaelekeza kwa yule dada aibu ikabaki mtaani na mshangao watu kujua kwamba sisi ni waathirika na kujua ile familia pia wameathirika, nikipita barabarani watu wananiangalia kwa huruma wakati mimi sio mgonjwa kila nikijitahidi kuwahadithia liliotokea wanalipokea kama hawaniamini, basi nimeamua kuishi na aibu yangu, kwakweli natamani hata kuama mtaa lakini siwezi sijui hata la kufanya.

mke wangu nimemuonya nisikae kumuona yule dada kwangu hata salamu asinipe barabarani na mumewe tulikuwa tunacheza wote pool sasa na hiyo bar imenibidi niame kwa aibu...

Robert

1 comments:

  1. pole sana kaka kwa yaliyokukuta inaonekana huyu mwanamke anaroho mbaya sana yaani tatizo lake anataka liwe lamwenzie yani huyu mama ingekuwa niuwezo wake angewaambukiza huu ugonjwa kusudi asife peke yake sio ajabu hata amejitahidi kufanya hivyo ikashindikana. sasa nije ktk ushauri inaoneka kwa jinsi gani watu bado hawajafahamu elimu ya ukimwi wewe kaka unasema unataka kuhama mtaa kwa sababu watu wanakunyooshea vidole ya kwamba una ukimwi unanichekesha kweli kweli kwani mtu akisema unaukimwi na huku unajiamini huna wewe unawasiwasi gani au unao nini nenda ukapime ujiamini maana naona hujiamini mimi watu wakiniambia nina ukimwi nahuku najijua sina stakuwa hata na presha hata punje nahawo wanao kunyooshea vidole wao wamepima wakajua afya zao binadamu wanashangaza kweli hawo wanaokunyooshea vidole wambie ukimwi hukuanza wewe na hutamalizia wewe kuna walioanza wwna wamesha tutoka na kunawaoumwa na kunawanaoendelea kuambukizwa kila watu kumi mmoja ana virusi vya ukimwi eti unataka kukimbia mtaa wako kisa umesingiziwa uanaukimwi na huku unajimini huna hainiingii akilini kabisa huyu alikwenda kutaja jina la mke wako na wewe pia mnavituko sana

    ReplyDelete